Mimi ni mkristo na mpenzi wangu ni muislam na tunataka kuoana ila ndugu zake hawataki

Kajolijo

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,364
4,612
Kichwa cha habari cha husika,

Mpenzi wangu ni muislam na mimi ni mkristo sisi tuko tayari kufunga ndoa lakini ndugu zake wamekataa katakata wanasema niwe muislam nami siko tayari kwa hilo.

Naombeni ushauri na nampenda sana tuko kwenye uhusiano kwa miaka miwili.
 
Hili tatizo la dini lisha kuwa kubwa sana.
Yaani ukiamua kuona na mtu asiye wa dini yako kubalini kwanza yeyote anaye badili dini kati yenu kuna vitu atavikosa pengine familia yake , au hata heshima kwa jamii yake
So kama una mpenda kubalini ku loose some so you can gain some hakuna namna
 
Hakuna chaguo moja hata siku moja. Machaguo huwa angalau mawili. Na uzuri hapo yako mawili. Ama uoe au usioe. Pia ubadili dini ili uoe au usibadili dini ili usioe.

Lakini kama ni mwanaume kubadili dini ni ujinga uliotukuka na unaokaribia ujuha. Kwani
[HASHTAG]#Kutongoza[/HASHTAG] utongoze wewe
[HASHTAG]#Mahari[/HASHTAG] utoe wewe
[HASHTAG]#Mwanamke[/HASHTAG] ahamie kwako
[HASHTAG]#Matunzo[/HASHTAG] akutegemee wewe
[HASHTAG]#Usalama[/HASHTAG] upo mikononi mwako
Na kadhalika Na kadhalika
[HASHTAG]#Halafu[/HASHTAG] ubadili dini wewe? Fikiri upya na uchape lapa!
 
Hahahaaa
Ugumu wa mwanaume kubadili dini ni anapoteza heshima kuanzia kwao mpaka kwa rafiki zake.
Ila kama umependa unabadili tu
 
Hili tatizo la dini lisha kuwa kubwa sana.
Yaani ukiamua kuona na mtu asiye wa dini yako kubalini kwanza yeyote anaye badili dini kati yenu kuna vitu atavikosa pengine familia yake , au hata heshima kwa jamii yake
So kama una mpenda kubalini ku loose some so you can gain some hakuna namna
Tatizo mm najiona moyon siko tayar kabisa kubadili dini
 
ilisha wahi kunitokea.ila nilicho fanya nika nilipima kama mapenzi yanazidi breki ya meli.nilipo hona hivo.nikaendelea na safari.kama kakolea force.kama bunge limeingilia kesi ya makonda na madawa ya kulevya hapo msimamo wako
 
Achana nae huyo utapoteza mda wako bure wazazi wa kiislam ni wagumu mno kubadili msimamo hasa hasa ukute ni wale wa swala tano.Anza mchakato wa kuachana na huyo binti taratibu huku ukitafuta mbadala wake
Cha ajabu nampenda sana.. nae naona ananpenda kabisa kanisaidia vitu vingi sana na wala si limbukeni wa hela
 
Nakushauri mwambie kuwa umeshindwa, msipoelewana katika imani jueni ndoa yenu haitakuwa na furaha wala amani. Tafuta mwingine na mwombe Mungu akuwezeshe kupata mwingine. Waweza kubadili dini lakini inategemea na imani yako ikoje! Kuepuka usumbufu na shida pls tafuta mwingine
Sasa hivi nina miaka 32 ntampata nani nianze kumchunguza na kumjua kama huyu
 
Back
Top Bottom