Kabla sijaoa kwa nyakati tofautitofauti nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasichana wadogo, mmoja alikuwa Secondary form three, mwingine alikuwa form four, na kwa Mara ya mwisho nilitembea na mtoto wa form Six hii ilikuwa ni katika harakati za kukidhi mahitaji yangu ya kimwili hasa ikichukuliwa kwa kipindi kile ilikuwa ngumu sana kwa mimi kumiliki mwanamke serious.
Kutokana na hali niliyokuwa nayo kimaisha(Kiuchumi) ilibidi nijikite katika kutafuta mtu ninayeweza kumdanganya kwa vichips mayai vya hapa na pale na ilikuwa ngumu kwangu kufikilia kuoa maana nilikuwa naishi katika mazingira ya Gheto (chumba kimoja mnashea watu kadhaa) huku kila kukicha tukihangaika kusambaza barua za kuomba kazi, nadhani wengi wetu tumepitia hili baada ya kumaliza vyuo.
Lakini Baada ya kuoa kutulia na ndoa yangu na Mungu kunijaalia Katoto kazuuri ka Kike na baadaye katoto kengine kazuuri ka kiume, achilia mbali kwamba nilishaacha kabisa hayo Mambo, lakini huwa naumia sana nikiona mtu mzima ana mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa shule awe wa Kike au wa kiume hata kama yupo Chuo kikuu, roho inaniuma sana na naichukia sana hii tabia ya kuchukua mtoto wa shule maana naona ni uharibifu, hii imekaaje? Je mimi ni mbinafsi? Maana hii hali imenikuta miaka ya hivi karibuni baada ya Muumba kunipatia watoto, je hii hali imewakuta na wanaume wenzangu?
....a what goes around comes around........
hawa wawili wamesema kila kitu.KARMA IS REALLY A BITCH!!!!!!!!!!! Jiandae tu kwa matukaio! Ndo maana wakasema unsimfanyie mtu, usichopenda kuja kufanyiwa!!!!
hakuna utakakalofanya zaidi ya kufundisha wanao katika misingi iliyo bora ie kuwa financially independent na kuwa na hofu ya mungu....ukishirikiana na mkeo kny malezi,watatoka watoto wenye mfano wa kuigwa,isipowezekana pia mshukuru mungu kwa kila jambo....:disapointed:
Mkuu, pole kwa hayo, sijui kama unatubu ama nini, lakini maadamu una mtoto wa kike wa damu yake jiandae ikibidi kwa maumivu maana katika level hiyo hiyo ya form three ama kabla huenda watu watakuwa wanajivinjari kunako mwanao, ndivyo ilivyo mkuu ni principle malipo ni hapa hapa duniani. Ikitokea usiue mtu, ila omba sana na utubu kwa hayo ili kuondoa hiyo mikosi/laana ya huko nyuma. Ni mtizamo tu naomba usichukie mkuu Mvaa Tai.
hawa wawili wamesema kila kitu.
mtoa mada roho inakusuta ulivyochezeya watoto wa wenzio na sasa unaona wanao watachezewa. wahenga walisema ''mkuki kwa ________ kwa binadamu mchungu''
kuna mtu aliwahi kusema siku moja
WANAUME WALIOWAHI KUWA NA MAHUSIANO SANA NA WATOTO UNDERAGE,AKIPATA MTOTO WA KIKE HUWA VILE VILE!
mhhmh!
anza kuwaombea wanao ukate hiyo roho!
ehhehehe sasa sijui itahamia kwa nani!isije ikahamia kwa mamsap(sijui niseme natania)ah hivo hivo bana!
Acha utani bana mi nipo serious
Nadhani umefika sasa sisi wanaume tuambiane ukweli jamani tuache kuchukua watoto wa shule, tushirikiane hawa watoto wasome shule, nakichukia sana nilichokifanya enzi hizo nakiri lilikuwa ni kosa sana sitothubutu tena na nashauri tuachane na watoto wa shule
nafurahi kuona umegundua ni makosa kutafuna underaged. anzisha kamati ya mtaani kwenu kuwaeleza wazazi/vijana wenu, unaweza kupata watu wa kuunga mkonoNajua hicho kitu kinaweza kutokea hata kwa wanangu, ni kweli napata uchungu sana hata nahisi kuchapa mtu risasi nikiona anahangaika na watoto wa shule, ndiyo maana natoa wito kwa jamii hasa wababa tuachane na vitoto vya shule, tushirikiane kuwakuza, kama mimi nilishawahi kukosea hakunizuii kutambua kosa na kuhamasisha watu tusifanye makosa ya hivyo