Mimi ni Divergent suala hili linanipa sana tabu

Gota8s

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
203
189
Habari zenu wana jamvi. heshima kwenu wote

Kuna suala hili huwa linanifanya nijione mimi ni wa tofauti sana. yani huwa sijawahi kukutana na aina hata moja ya watu ambao nimeendana nao. jambo moja la msingi ni kwamba siwezi ku-fit in kwenye demo'

hebu ngoja nieleze zaidi. kwanza mimi huwa sina Hobby. kila jambo ambalo yeyote huwa analifanya kama hobby mimi kwangu ninapolifanya huwa ni kama activity tu. yaani sina kitu hata kimoja ambacho naweza kusema nisipokifanya sijiskii amani, au sijiskii furaha.
Mimi ni mtoto wa kiume, kijana kabisa wa early 20s, sasa mimi sio shabiki wa mpira, sio mlevi wa pombe, sio mtu wa viwanja, sio mtu wa starehe hata kidogo, sipendelei sana wanawake (najua naeleweka hapa), mziki, movies vyote huwa navifuatilia pale napoamua tu, ila hata ninapoacha kufuatilia, sipati ile 'alosto' kama namna ninavyoona wenzangu wanakuwa.

sasa tukienda kwenye masuala ya kielimu, sijawahi kuelewa kabisa mimi napenda nini na kipi sipendi. kwanza mimi sio 'jiniaz' no, ila namudu chochote nikiamua kukifanya. kwa nfano, nilipokuwa nasoma O-level nilikuwa namudu masomo yote. biashara, sanaa na sayansi kwa kiwango sawasawa. yaani ukiona nimefail somo fulani ilikuwa kwa sababu sijaamua kujisomea tu. ilikuwa inafika wakati nazigawa Terms, nasema labda Muhula wa kwanza nitakaza kwenye sanaa, na wa pili ntakaza sayansi. hata matokeo ya mwisho CSS yalipotoka ilikuwa inconclusive. yale niliyonuia kufanya vizuri nilifanya hivyohivyo nilivyotaka.

A level nilisoma combination nisiyoitaka (kuna situation zilipelekea) nikasusia kuisoma mpaka mwezi October tangu June. Muda wote tangu naripoti nilisusia kusoma sanaa, nikawa niko PCM, mwalimu wa darasa akanitimua kuwa hanitambui, nikahamia PCB nikakaa wiki mbili ikaja ile mid-term ya September, nikapata Div II. ikaja mikanganyiko, nikaondolewa PCB nikaambiwa niende HKL ambayo ndio niliyokuwa Allocated. mpaka November 17 ndo nikaenda HKL kuanza kujiandaa na mtihani wa November. Guys, nilikaa kidogo matokeo ya mtihani yalipotoka nikaongoza Combination zote za Arts ujue kila mtu alikuwa ananiona wa ajabu ila mm nikawa naona kawaida tu. nilikuwa sio mtu wa msuli hata kidogo ila ndo nilikuwa tu wa aina hiyo.

sasa hilo lisikushangaze, kwenye suala la dini sijawahi kujua nifuate imani gani. mimi najua misingi ya dini zote. ukristo na uislamu. nasoma Qur'an na nasoma Biblia. nimesoma vitabu vingi sana vya imani zote mbili, vya unabii na vya theolojia. linapokuja suala la kusema nichague imani napata wakati mgumu achilia mbali kuchagua dhehebu. yaani mimi najikuta niko tofauti mno mpaka najiskia vibaya.

zamani nilikuwa mcheshi sana na mzungumzaji lakini saivi imenibidi niachane na hiyo attitude. kwa sababu sasa naonekana 'Much know' kwa kila nachokizungumzia. sasa tatizo jingine kubwa ni kuwa naweza ku control attitudes na feelings zozote. mimi naweza kuzimudu hisia na mihemko ya aina zote, iwe hasira, furaha, huzuni yaani hali yoyote. sio kwamba sipati hizo, no. ila naweza kuzi control. kwa mfano nikipata msiba, huwa naumia ndio hata nikimpoteza mtu wa karibu mno basi nahuzunika sana ila akili yangu inaniambia kuwa ninfahamu ninachotakiwa kukiwaza, akili inaniaminisha kuwa hisia hazipiti maarifa na uelewa, basi hapohapo kimoyomoyo najiambia imetokea na yeyote itamkuta, kwa hiyo ni kawaida. ndugu zangu mimi huwa siwezi kabisa kuwa kama wale wenzangu huwa wanagalagala na kupoteza fahamu. ikitokea hivo ujue nafanya huku najielewa, na nafanya kama kuigiza tu. huwa najishtukia.

Nitaendelea baadae kisha mtanipa ushauri nifanyeje
 
mhh sijaelewa ila najua tu kuna movie inaitwa hivo. mtoa mada ulikuwa unamaanisha nini?
nadhani pia kuna movie inaitwa hivo. Divergent nimemaanisha kuwa sifungamani na kundi hata moja, yaani mimi makundi nyote naingia
 
Wako wengi kama ww, Hawajui wanataka nn, ila akiamua kuwekeza muda na nguvu zake mambo yanakwenda vzr kabisa.
Wengi wao huamua kuamini mipango ya mungu, maana yy kila kitu chake kinanyooka tu hasa akimuomba mungu na akaweka juhudi kwenye jambo husika.
 
ni kweli. hata mimi najitahidi sana. naamini nitaweza.
Asante
 
Inaendelea... 02

Suala lingine linalonichanganya ni kuwa kwenye suala la kulala. mimi ndio wa kuamua nilale au nisilale. wakati mwingine huwa najielewa hata usingizini. hata nichoke namna gani ninaweza kuazimia kukaa macho usiku mzima na kesho yake nikaamka nafanya shughuli za kawaida. Zamni nilipokuwa nasoma chuo kikuu, nilikuwa nalala hostel sasa siku moja tukakurupushwa kuna mtu alikuwa anaiba simu na computer chumba jirani yetu. aliyepiga makelele ni mschana alikyekuwa upande wa pili ndiye alimuona mwizi akapiga makelele (wenyeji wa mabibo hostel wanajua proximity ya Block C mpaka Block B. hasa vyumba vya Block C 201 mpaka 204, na vyumba vya Block B namba 274 mpaka 280. hizo wings zinatazamana) sasa kwenye tukio hilo mimi kama kawaida yangu nilikuwa nimelala usingizi, nikaski mtu anaita kuwa tunaibiwa. nikaamka haraka nikatazama upande kelele zilipotokea nikaelekezwa kuwa ni room next. nikawaamsha wenzangu haraka nikatoka nje chumba kinachofuata. (ni kitendo cha sekunde kama 20 tu) sasa natoka nja nikamkamata yule mwizi huku akinikosakosa kile ki-stendi cha feni. nikamdaka na begi lake nikamrudisha chumba alichotokea.

ile kufika chumbani nakuta wakazi wote wa kile chumba ndo wanaamka halafu wamelewa usingizi, mara wajigonge ukutani, mara wafikiche macho, yaani bado network haijasoma. baada ya kama dakika tano ndo nikaona karibu wote akili zimetulia. tukamchukua mwizi wetu kumpeleka pale Aux.Police. nikarudi room kwangu nikakuta bado wenzangu wote wamelewalewa na usingizi, mmoja tu ndo anasimulia wenzie kuwa anadhani amesikia makelele.
Kipindi hicho ilikuwa ni mwanzoni mwa semister, kwa hiyo watu hawakuwa sana na vitu vya kujisomea
 
Tanzania bado hakuna watu wa kushauri watu kama sisi bro... tuko mbele ya muda sana... kaza tu

nahisi tunafanana kiaina mi niko kwenye kila kitu nikiamua.... sina upande mmoja maalumu hata mahusiano siwezi kukaa na mtu mmoja...

umezaliwa mwezi gani mzee
 
nahisiBinadamu wote wanauwezo Kama wako,wewe umejikuta unautumia.
Nguvu zote zipo KICHWANI mwako,Mimi kila nnachokifanya hapa Duniani akili yangu inaniambia nishawahi kukifanya,nikienda sehemu yoyote ngeni kumbukumbu zinanijia kuwa hapo si pageni kwangu na sipotei hata Kama sijawahi fika!

Naenda sehemu nakutana na mtu ananiuliza vitu ni Kama tushawahi kukutana before,yaani huwa naduwaa sana,yanatokeaje haya?!!!!
 
Utakosa uelekeo kimaisha, maisha kwa kiasi kikubwa yanaitaji kufocus na kuwa selective.... uamue sasa unaitaj nani uelekeze nguvu zako huko na brain utatii...
 
Hili linaweza kuwa tatizo lakini pia linaweza lisiwe tatizo inategemea na bahati itayo kutana nayo huko mbeleni.

Maana kuna msemo husema mtaka yote kwa pupa mwishowe hukosa yote… unahitaji kujifanyia upembuzi hakinifu juu ya utambuzi wa kipi bora kwako kisha usonge mbele nacho. Ukiendelea kuhaha haha huku na kule utapoteza energy, resources, muda etc…

Kwenye hili aliefanikiwa ni mmoja pekee ambaye ni unga wa ngano…

Akitaka kuwa andazi haya
Sambusa
Chapati
Bia
Kaukau
You name it
 
Habari zenu wana jamvi. heshima kwenu wote

Kuna suala hili huwa linanifanya nijione mimi ni wa tofauti sana. yani huwa sijawahi kukutana na aina hata moja ya watu ambao nimeendana nao. jambo moja la msingi ni kwamba siwezi ku-fit in kwenye demo'

hebu ngoja nieleze zaidi. kwanza mimi huwa sina Hobby. kila jambo ambalo yeyote huwa analifanya kama hobby mimi kwangu ninapolifanya huwa ni kama activity tu. yaani sina kitu hata kimoja ambacho naweza kusema nisipokifanya sijiskii amani, au sijiskii furaha.
Mimi ni mtoto wa kiume, kijana kabisa wa early 20s, sasa mimi sio shabiki wa mpira, sio mlevi wa pombe, sio mtu wa viwanja, sio mtu wa starehe hata kidogo, sipendelei sana wanawake (najua naeleweka hapa), mziki, movies vyote huwa navifuatilia pale napoamua tu, ila hata ninapoacha kufuatilia, sipati ile 'alosto' kama namna ninavyoona wenzangu wanakuwa.

sasa tukienda kwenye masuala ya kielimu, sijawahi kuelewa kabisa mimi napenda nini na kipi sipendi. kwanza mimi sio 'jiniaz' no, ila namudu chochote nikiamua kukifanya. kwa nfano, nilipokuwa nasoma O-level nilikuwa namudu masomo yote. biashara, sanaa na sayansi kwa kiwango sawasawa. yaani ukiona nimefail somo fulani ilikuwa kwa sababu sijaamua kujisomea tu. ilikuwa inafika wakati nazigawa Terms, nasema labda Muhula wa kwanza nitakaza kwenye sanaa, na wa pili ntakaza sayansi. hata matokeo ya mwisho CSS yalipotoka ilikuwa inconclusive. yale niliyonuia kufanya vizuri nilifanya hivyohivyo nilivyotaka.

A level nilisoma combination nisiyoitaka (kuna situation zilipelekea) nikasusia kuisoma mpaka mwezi October tangu June. Muda wote tangu naripoti nilisusia kusoma sanaa, nikawa niko PCM, mwalimu wa darasa akanitimua kuwa hanitambui, nikahamia PCB nikakaa wiki mbili ikaja ile mid-term ya September, nikapata Div II. ikaja mikanganyiko, nikaondolewa PCB nikaambiwa niende HKL ambayo ndio niliyokuwa Allocated. mpaka November 17 ndo nikaenda HKL kuanza kujiandaa na mtihani wa November. Guys, nilikaa kidogo matokeo ya mtihani yalipotoka nikaongoza Combination zote za Arts ujue kila mtu alikuwa ananiona wa ajabu ila mm nikawa naona kawaida tu. nilikuwa sio mtu wa msuli hata kidogo ila ndo nilikuwa tu wa aina hiyo.

sasa hilo lisikushangaze, kwenye suala la dini sijawahi kujua nifuate imani gani. mimi najua misingi ya dini zote. ukristo na uislamu. nasoma Qur'an na nasoma Biblia. nimesoma vitabu vingi sana vya imani zote mbili, vya unabii na vya theolojia. linapokuja suala la kusema nichague imani napata wakati mgumu achilia mbali kuchagua dhehebu. yaani mimi najikuta niko tofauti mno mpaka najiskia vibaya.

zamani nilikuwa mcheshi sana na mzungumzaji lakini saivi imenibidi niachane na hiyo attitude. kwa sababu sasa naonekana 'Much know' kwa kila nachokizungumzia. sasa tatizo jingine kubwa ni kuwa naweza ku control attitudes na feelings zozote. mimi naweza kuzimudu hisia na mihemko ya aina zote, iwe hasira, furaha, huzuni yaani hali yoyote. sio kwamba sipati hizo, no. ila naweza kuzi control. kwa mfano nikipata msiba, huwa naumia ndio hata nikimpoteza mtu wa karibu mno basi nahuzunika sana ila akili yangu inaniambia kuwa ninfahamu ninachotakiwa kukiwaza, akili inaniaminisha kuwa hisia hazipiti maarifa na uelewa, basi hapohapo kimoyomoyo najiambia imetokea na yeyote itamkuta, kwa hiyo ni kawaida. ndugu zangu mimi huwa siwezi kabisa kuwa kama wale wenzangu huwa wanagalagala na kupoteza fahamu. ikitokea hivo ujue nafanya huku najielewa, na nafanya kama kuigiza tu. huwa najishtukia.

Nitaendelea baadae kisha mtanipa ushauri nifanyeje
Absolute the same to me,mi hata chuo na si advance tu,nimehama faculty Zaid ya mbili na vyuo Zaid ya vitatu,hua tunashindwaga kufanya maamuzi KWA kutaka vyote ama kuweza vyote,hata kwenye ununuzi wa vitu hujikuta tukishindwa kuchagua KWA kuona vyote vyafanana/viko sawa
 
Back
Top Bottom