Mimi ndiye mwasisi wa msemo "HAPA KAZI TU"

Mimi ndiye mwasisi wa msemo "HAPA KAZI TU"

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,612
Bila maslahi yeyote ni kiri kuwa mimi ndiye niliyeliandika neno hapa kazi tu baada ya majina matano kuchujwa na JPM kupita.

Msemo huo ulikuja kichwani mida ya usiku baada ya kufuatilia mchakato wa majina matatu yaliyopewa aka ya BAJAJ
1,B_Benard Membe
2,A_Asha Rose Migiro
3,JA_ January Makamba
4, J_ John Pombe Magufuli.

Hakika nilikuwa nikivutiwa sana na uchapakazi mkubwa sana wa Magufuli toka akiwa Naibu Waziri, mpaka uwaziri ktk wizara mbili tofauti..

Nilimuona ni mtu wa kazi sana ndio mana nikampost kwenye mtandao wangu wa facebook na kuandika kuwa
"Magufuli 2015 Hapa kazi tu"

Neno hapa kazi tu lilikuwa sana na kufika kila kona ya nchi nikiri tu nilifurahia hatua hiyo though sipendi kusifiwa wala kutajwa.


LEO NINAKUJA NA MSEMO KWA AJILI YA MAMA SAMIA ;

MAMA SAMIA, "TUMAINI JIPYA KWA WATANZANIA WOTE"

Mama Samia ni tumaini jipya kwa watanzania kwakuwa ;

1, Uwepo wake madarakani ni wa mpango wa Mungu na wala si bahati
2, Kuna mengi mazuri ya kuyaendeleza ambayo yalianzishwa na JPM
3, Kuna waliopunguzwa makazini bila hatia tumaini lao ni kwa mama Samia
4, Kuna waliopoteza biashara zao tumaini pekee ni kwa Mama Samia
5, Kuna waliokimbia nchi tumaini lao pekee ni kwa mama Samia
5, Kuna elimu bure na tumaini la maskini ni kwa mama Samia
6, Kuna miradi muhimu sana kwa taifa kama vile Standard garge railway, Stigler's na mingine ambapo tumaini letu pekee ni kwa Mama Samia
7, Kuna waliofungwa bila hatia nao tumaini lao ni kwa mama Samia
8, Kuna waliofukuzwa chama nao tumaini lao ni kwa Mama Samia
9, Kuna walioogopa kuja kuwekeza Tanzania nao tumaini lao la pekee ni kwa mama Samia
10, Kuna wengi waliokosa ajira kwa muda mrefu nao tumaini lao pekee kwa sasa ni kwa mama Samia.

Hakika mama Samia anatosha kwenye hiyo nafasi na wala hatuna shaka naye ila tusiache kumuombea kwa Mungu amfanyie wepesi ili aweze kuyatimiza matumaini ya watanzania kwani
"MAMA SAMIA NI TUMAINI JIPYA KWA WATANZANIA"

[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipenda kauli ya Jaji Mkuu kwa Raisi wetu Muheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwamba ana bebwa na mabega ya watangulizi wake, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Hayati Magufuli, hivyo anauwezo wa kuona mbali zaidi, na kujifunza kutokana na makosa yao.
 
Kama kuna makosa yalifanyika kipind cha hayati , yawe ya kidiplomasia , kijamii, kiuchumi , kisiasa na kitechnolojia hakuna haja ya kuyafuata .....!!! Ndio mana tunasema kila mmoja na talanta yake na kila nabii na Zama zake basi....wamwache mama apige kazi
 
Muasisi wa msemo Hapa Kazi Tu ni Sir Juma Kasimu Kiroboto ( Sir Nature).

Sikiliza nyimbo zao Wanaume TMK utausikia sana tu, kama wewe uliutoa huko ukauhusisha na uchapakazi wa JPM sina tatizo na hilo.

Walau acknowledge Sir Nature kwanza kisha endelea kujipa ujiko.
 
Du mwanangu mmeanza kumsingizia marehemu mwenye kauli mbiu yake siyo? Mungu anawaona.
 
Msemo huo ulikuja kichwani mida ya usiku baada ya kufuatilia mchakato wa majina matatu yaliyopewa aka ya BAJAJ
1,B_Benard Membe
2,A_Asha Rose Migiro
3,JA_ January Makamba
4, J_ John Pombe Magufuli.
Mbona yapo manne, wewe unasema matatu!

Huo ni uongo wa kwanza..., ngoja tuendelee unasemaje huko chini!
 
Neno hapa kazi tu lilikuwa sana na kufika kila kona ya nchi nikiri tu nilifurahia hatua hiyo though sipendi kusifiwa wala kutajwa.
Wao waliliokota vipi toka kwako, walikupa taarifa kuwa wanatumia maneno hayo matatu kujitangaza?

Kwa vile hukuwa na hati miliki au nembo ya kibiashara ya maneno hayo, hukuwa na dai lolote kwa kulitumia kwao, lakini wangekuwa waungwana, si angalau hata wangekutambua tu, hata kwa maneno kwenye mkutano wa hadhara, au ukaalikwa kabisa nyumbani kwao kwa faragha, wewe ukiwa kama mgeni wao?

Na vipi umesubiri hadi mwizi wa kazi zako aondoke ndio ulete haya maneno hapa, itakusaidia nini?

Niseme kitu kwa ujumla, waTanzania wengi bado wanaishi kwenye enzi za Mjerumani, Mwarabu na Mwingereza.

Hatujui thamani na maana ya vitu vyetu.

Na mbaya zaidi, wewe mwenyewe hukuweka ushahidi/kumbukumbu yoyote kuwa hayo maneno kweli yalikuwepo kwenye mtandao wako wakati huo unaodai uliyaweka.

Kwa hiyo huna ushahidi wowote, na hapa unatuuzia maneno tu!
 
Nimeipenda kauli ya Jaji Mkuu kwa Raisi wetu Muheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwamba ana bebwa na mabega ya watangulizi wake, kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Hayati Magufuli, hivyo anauwezo wa kuona mbali zaidi, na kujifunza kutokana na makosa yao.
Siyo yake mkuu.

Huo ni msemo wa kila siku na wa kawaida kwenye lugha za mabeberu.

Labda useme ubunifu katika lugha yetu ya kiswahili sasa.
 
HAPA KAZI TUU IMEKUA KITUMIWA SANA NA TMK WANAUME FAMILY,, HASWA TEMBA MIAKA HIYO.. KUNA MAGARI YAO WALIKUA KWA NYUMA WANAANDIKA HAPA KAZI TUU KAZI TUU....
 
Back
Top Bottom