Mimi Nasubiri Manabii Waanze Kuongea!

Mimi Nasubiri Manabii Waanze Kuongea!

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,773
Reaction score
6,904
Mimi nasubiri manabii tu waongee! Juzi kati nilishawahi kuanzisha uzi humu wa power tuliyonayo kuprophesy. Martin Luther King Jr alikuwa katikati ya written speech akaanza kuprophesy maneno ambayo leo mnaita 'I have a dream speech'.

Credit to TL, aliprophesy kwamba 'mkiendelea kukaa kimya, wakimalizana na sisi wataamia kwenu' (siyo nukuu ya neno kwa neno).

Kama mnataka nchi hii ibadilike kisiasa, kiuchumi, kiimani, kijamii, acheni kulalamika, PROPHESY!
 
Aaaaah ila kwa hii sirikali isiyojulikana ni kazi kweli kweli ukprophesy unakula ban
 
Mimi nasubiri manabii tu waongee! Juzi kati nilishawahi kuanzisha uzi humu wa power tuliyonayo kuprophesy. Martin Luther King Jr alikuwa katikati ya written speech akaanza kuprophesy maneno ambayo leo mnaita 'I have a dream speech'.

Credit to TL, aliprophesy kwamba 'mkiendelea kukaa kimya, wakimalizana na sisi wataamia kwenu' (siyo nukuu ya neno kwa neno).

Kama mnataka nchi hii ibadilike kisiasa, kiuchumi, kiimani, kijamii, acheni kulalamika, PROPHESY!
Kama ni mambo ya manabii, hata humu jf tunao manabii kibao, TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!.
Pia nikatoa wito maalum, tuwaepuke Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!
Hili la Watanzania tupunguze kulalamika pia niliwahi kushauri
2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tuu, Tung'ate!.
Umeshauri watu waache kulalamika, sasa wafanye nini?.

Paskali
 
Kama ni mambo ya manabii, hata humu jf tunao manabii kibao...........
Paskali

Nimaposema kuprophesy namaanisha kama maana ya neno ilivyo. Nitatoa mfano, kuna tofauti kubwa kati ya kusimama jukwaani, kwenye madhababu au mbele ya waandishi wa habari na kusema 'demokrasia imemimywa, sheria zinavunjwa, kuna udikteta, watu wananyanyaswa, kutekwa na wengine kupotea' (huku ndiyo naita kulalamika) na kuprophesy kuna kwa aina mbili:

  1. Kutoa hatarisho. Mfano nilioutumia wa kauli ya TL ni moja ya kauli kama hiyo. Nadhani ndiyo unamaanisha unaposema 'phophets of doom' lakini hilo hatarisho lina nguvu sana tu kwa sababu msemaji anapaint a clear picture ambayo kila mtu akisikia atataka achukue hatua hili lililosemwa lisitokee.
  2. Kutoa kauli ya matumaini. Hii ndiyo inafanana na ya MLK Jr ya 'I have a dream speech'. Mtu unaweza kusimama ukasema 'pamoja na yote tunayopitia, udhalimu na uonevu lazima vitakwisha. Siku inakuja ambayo watanzania watafurahia uhuru na maliasili zao......' Natumaini point yangu umeielewa. Statement kama hiyo ina power kubwa sana kwa sababu hata wale waliokata tamaa (kama huyo bwana hapo juu 'ankai') inawapa nguvu mpya na kuwa na matumaini kwamba kesho iliyo bora zaidi inakuja.
Kuna watu wengi wamekata tamaa na kujawa na hofu. Wengi wanaona hili lidumwana lililo mbele yao halishindiki, lina nguvu kushinda wao, nk. Wote hawa ni wa rika, tabaka na itikadi tofautitofauti. Wote hao wanajua kinachoendelea kwa hiyo kauli za kulalamika haziwasaidii kwa sababu unawaambia ambacho tayari wanajua. Ukienda mbele zaidi na kutoa aina ya kauli hizo mbili nilizotaja (prophesy) unawapa watu pumzi mpya ya kuendelea mbele.

Ndiyo, kila mtu anaweza kuwa nabii ila ili matamshi yako yawe na divine powers (kama tafsiri hasa ya prophesy inavyosema), hapo sasa ni habari nyingine. Ndiyo maana nikasema nawasubiri manabii (wale walio na divine powers) waongee.
 
Umeshauri watu waache kulalamika, sasa wafanye nini?.

Paskali

Nimesoma references zako zote ulizoweka. Ni kweli inaonyesha umewahi kukizungumza nilichokisema kwa muda sasa. Nadhani ni wakati kauli zetu zibadilike.

Narudia, Mungu anaweza kumtumia yoyote kutoa unabii. Kuna siku kwenye kona ya Msimbazi na Uhuru, atasimama mmachinga mmoja ataanza kuprophesy na kuna mtu atamrecord kwa simu na kusambaza clip itakayoibadilisha TZ overnight.
 
Back
Top Bottom