Mimi Na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi Na Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Guga-Q, Apr 9, 2012.

 1. G

  Guga-Q New Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naipenda Tanzania, najivunia kuwa Mtanzania. Serikali yetu inamamlaka kisheria juu ya usimamiaji wa haki na usawa, mgawanyo wa raslimali zote za nchi kwa raia wake bila upendeleo. Kwa niaba ya wananchi serikali inamiliki dola, vyombo vya usalama, vyombo vya fedha (Mfano Benki Kuu, ukusanyaji wa mapato-TRA), Huduma za jamii (afya, elimu, ardhi) na mengine kadha wa kadha, nimetaja machache. Mihimili mingine ni Bunge na Mahakama katika kuwatumikia Watanzania.


  Hoja yangu leo inazungumzia zaidi upande wa serikali na wenye jukumu la kuiunda.Kwa takriban miaka 31 baada ya uhuru watu mwaka 1961, Serikali iliongozwa na mfumo wa chama kimoja. Mfuma wa vyama vingi unatimiza miaka 20 sasa.

  Mtazamo wangu juu ya wenye dhamana ya kuunda serikali.
  Leo chama kinachounda serikali kinazidi tetereka kimaadili, mtazamo, na dira. Mie si wa kwanza kuyasema haya, kiongozi mmoja maarufu ambaye sasa na mareheme, Mungu aipumzishe roho yak e kwa amani alishamea, "Sisiem haina dira" Yaliyo katika katiba na yanayotekelezwa na viongozi wa ngazi zote pamoja wanachama ni kinyume na katiba walioitunga na kuapa kuitetea. Chama tawala kimegawanyika katika makundi hasimu manne kimtazamo;

  Kundi linalopinga matumizi mabaya ya fedha za umma. (maarufu kama wapinga ufisadi).
  Kundi hili linaudwa na watu maarufu ndani na nje ya serikali na pia katika chama. Ni kundi lenye nguvu kubwa kiushawishi, wanajipambanua kwamba wapo kinyume na matumizi mabaya ya fedha za umma. Msimamo wao ni kutaka wote walioliingizia Taifa hasara mkondo wa sharia uchukue nafasi yake.

  Kundi la pili ni hilo linalopingwa na kundi liliotangulia hapo juu (Maarufu kama Magamba).​
  Ni kundi lenye ushawishi mkubwa wa kifedha, lina watu maararufu ndani na nje ya serikali na pia katika chama. Si wepesi wa kupanda katika majukwaa ya siasa, ila wanatumia mbinu nyingine kujiimarisha na kuteka wafuasi. Lipo kimya kwenye masuala yanayoikera jamii ikiwemo rushwa, kuongezeaka kwa pengo kati matajiri na maskini na mengineyo. manaabudu mali.


  Kundi la tatu ni la watu wa maadili na wanaopenda misingi na chimbuko la chama (maarufu kama asili)
  kundi hili lizaongozwa na watu mashuhuri, wengi wapo nje ya serikali lakini bado ni wanachama pia. Wanajitokeza hadharani kukikosoa au kukikumbusha chama misingi imara wanayoamini imetelekezwa. Wanabainisha kwamba chama cha wakulima na wafanyakazi masikini si hichi kilichopo sasa, hichi cha sasa wanakieleza kimetekwa na wafanyabiashara na mtajiri.

  Kundi la nne ni la wanachama wa kawaida walioko mijini na vijijini.
  Wengi wao ni wanachama wa kawaida, hawana nafasi kubwa serikalini, wamepigwa na butwaa hawajui msimamo na dira ya chama chao. Wale wa vijijini ndo hawaelewi kabisa kama kuna makudi yanayosigana, wanajua kuwa chama bado ni kile kile cha miaka ya nyuma. Wanagombaniwa na makudi nliyoyaeleza hapo awali wafuate mirengo yao.

  Uwepo wa makundi hayo ni moja ya vyanzo zikuu vinavyodhoofisha utendaji wa serikali. Kwani viongozi wa serikali wengi wao wamo ndani ya makudi hayo. Serikali iliyopaswa kuwatumikia wananchi inatumia rasilimali nyingi ikiwemo, rasilimalin watu, rasilimali fedha, rasilimali muda kujikita kupitisha hoja zao kimakundi pasipo kufikiria wananchi. Mihimili mingine ikiwemo Mahakama na Bunge imeathiriwa pia na makundi haya. Matokeo yake sote ni mashahidi, rusha kubwa zinaendelea hakuna anefikishwa kwenye sheria, haki inadhulumiwa, wageni wanazidi torosha hazina za taifa ughaibuni. Uchumi unakuwa lakini mgawanyo ni kwa wachache maendeleo hakuna, viongozi dhaifu kabisa, kulindana kulikopitiliza, mfumuko wa bei, ajira hakuna, vyomba vya usalama kuua raia nikawaida kabisa. Na matatizo mengi yanayoikumba jamii. Kwa kuzingatia muda nimetaja machache tu.

  Nini jukumu letu kama wananchi katika kutetea na kurejesha haki yetu stahiki?? Tuanzie wapi?

  Jiskie huru kuijali hoja yangu "Mimi na Tanzania" kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo. Utaifa na Uzalendo kwanza.
   
Loading...