Mimi Man Utd Mpaka nife:WAYNE Rooney | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi Man Utd Mpaka nife:WAYNE Rooney

Discussion in 'Sports' started by Junius, Nov 14, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WAYNE Rooney amesema kuwa atabbakia katika klabu ya Manchester United katika maisha yake yote.
  Mchezaji h wa England, Rooney amebakia miaka miwili na nusu katika mkataba wake wa sasa ambao analipwa kiasi cha pauni 110,000 kwa wiki lakini kwa sasa tayari kumekuwa na mipango ya mazungumzo ya kuingia mkataba mwingine.

  Amesisitiza kwamba hataki kufuata nyayo za mchezaji mwenzie wa zamani katika United, Cristiano Ronaldo ambaye amemtaka akajiunge naye Real Madrid.

  Rooney alisema: " Ni vizuri ikajulikana lakini ni fuaraha katika United. Hadi watakaponieleza vingine, siwezi kuondoka.

  " Nina miaka miwili inabakia katika mkataba wangu baada ya msimu huu, kwa hiyo ni uhakika kwamba kutakuwa na makubaliano katika miezi michache ijayo."

  SunSport iliwahi kusema katika gazeti lake la
  Septemba 1 kwamba Rooney atabakia Old Trafford kwa maisha yake yote, na jana alisema tena kauli hiyo wakati alipoulizwa kama anaweza kuendelea kuwepo United.

  Alijibu : "Yeah,ninaipenda sehemu. NI umbali wa dakika 30 kutoka nyumbani na familia yangu yote niliyonayo ninanafasi ya kutwaa makombe."

  Rooney anajua kwua anaweza kuwa mmoja wachezaji nyota wa United sambamba na wachezaji kama George Best, Bobby Charlton, Denis Law na Eric Cantona. Alisema: " Ni kolabu kubwa sana.

  "Wakati nilipokuwa nikikua ingawa nilikuwa shabiki wa Everton , nilikuwa nikipenda kuiangalia United ikicheza na kutwaa makombe.

  " Sasa ninashinda makombe mwenyewe na ninataka kushinda makombe mengio zaidi pale."

  Rooney alisema kwua alikuwa katika halia ya kujisikia vibaya sana wakati timu yake ilipofungwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea kitu kilichofanya atoe kauli kuwa mwamuzi alikwua ni mchezaji wa 12 wa wapinzani wao Jumapili.

  Kutokana na kujtoa kauli hiyo mchezaji huyo amepewa onyo na Chama cha Soka cha England (FA) kutorudia tabia kahiyo wakati alipomtuhumu refa Martin Atkinson kupendelea Chelsea.

  Rooney alisema "Kwa kweli, Niliangalia nyuma na pengine sikutakiwa kusema vile.

  "Lakini nilisikitika mwishoni mwa mchezo nilihisi kuwa tulistahili kupata matokeo mazuri.

  Alisema kuwa ingawa timu yao imekuwa ikicheza vizuri katika msimu huu lakini wamekuwa wakipata matokeo ya kusikitisha".

  source:news agencies
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tunahitaji wachezaji kama hawa ambao wapo tayari mpaka pumzi yao ya mwisho.
   
Loading...