Mimba ya matokeo ya 'Tukio la Ubakaji' - Unashaurije?

Chupaku

JF-Expert Member
Oct 15, 2008
1,091
401
Wadau,

Leo asubuhi wakati nimetoa mawazo mbali na matukio ya jana ya Arusha, nilifungulia 89.0 FM kipindi cha Early Morning Rise. Topic ya leo ilitoka kwa mwanaume ambaye ana ndoa ya mwaka mmoja na mtoto mmoja. Wiki nne zilizopita majambazi yaliwavamia na katika tukio hilo kama ilivyo ada wakambaka mke wake. :mad2::mad2::mad2:

Kwa maelezo waliyotuma hapo kwa mtangazaji mke wake amepima HIV na hana (ingawa sina uhakika na matokeo haya inategemea walipima lini na kutumia vipimo gani). Juzi vipimo vimeonyesha mke wake ni mjamzito. They are devastated.

Wanasema wao ni wakristo wazuri na wanaona kama kutoa mimba hiyo ni dhambi kubwa sana. Ila wana mashaka kumzaa mtoto huyo maana atakuwa anawakumbusha tukio hilo maisha yao yote.

Kama wangekuwa wamekuja kwako, ungewashaurije? Watoe mimba au wasitoe na kama wasitoe, wajipangeje ili wasije kumtesa bure mtoto asiye na makosa?

Karibuni.
 
Mtoto hana hatia lakini hiyo mie naona waitoe tu. Huyo mtoto atakuja kuteseka sana
na haswa ikitoke akawa na shida kidogo ya kawaida, itawakumbusha matukio ya nyuma
 
Wasitoe, mtoto atalelewa na mama yake mzazi na baba yake wa kambo.
 
Mtoto hana hatia lakini hiyo mie naona waitoe tu. Huyo mtoto atakuja kuteseka sana
na haswa ikitoke akawa na shida kidogo ya kawaida, itawakumbusha matukio ya nyuma

Umeshwahi kuona mtoto ana kosa dogo tu kama amejikojolea halafu anatandikwa kama punda? Ndiyo hayo basi unayoyassema. What if ni wa huyo baba mwenye nyumba?
 
Wasitoe, mtoto atalelewa na mama yake mzazi na baba yake wa kambo.

Baba wa kambo amlee? May be. Tatizo hawezi ku delete lile tukio la ubakaji toka akilini mwake, anasema mtoto atakuwa namkumbusha kila siku. Na ikitokea mtoto mtukutu usishangae siku moja akaambiwa - we mtoto wa jamb....!
 
Hata wakitoa bado watakumbuka!Tena wanaweza kufika mahali huyo mama akaanza kujutia uamuzi wake!!Wakati mwingine ni bora kua na kitu hapo anaweza hata kumpeleka kwa bibi yake...kuliko kutokua nacho ukakitamani!

Sidhani kama ni haki kumchukia mtoto kwa mazingira yaliyomleta duniani!Nna rafiki yangu alibakwa akiwa na miaka 14..akapata mimba leo hii ana mtoto na wala hajawahi kujutia..mpaka amemwita Miracle..anampenda kupinda maelezo!Sasa kaolewa na ameongeza wa pili!

Huwezi jua huyo mtoto atakuaje.
 
kutoa mimba ni dhambi ya mara moja, na kumnyanyasa mtoto maisha yake yote ni dhambi ya kila mara.mie naona watoe tu kuepusha mlundikano wa dhambi zijazo,pia siku akija gombana na mumewe atatumia hiyo kumnyanyasa huyo mkewe.

Kwangu mi nkutoa tu. mtoto akikuwa asije ulizia baba yakr bure
 
Ma dear do the right thing think twice and then follow your heart to ur ultimate goal
 
Wamejuaje kwamba mimba sio yao wenyewe? Walikuwa likizo kuchakachuana?? Kama kweli sio yao, basi nashauri wapitie msaada wa kitaalamu kwa watu wa saikolojia ili kuwaweka sawa wafike mahali wakubali kiakili kwamba mtoto ni wao wenyewe na wamlee kama wengine walionao. :amen:
 
Na msaada wa kiroho unahitajika zaidi hapo
 
kwa kweli sis hapa tutatoa ushauri tu, lakini huyo mama anatakiwa i make decision yake mwenyewe....
maana ye anajua anachokipitia, na anajua moyoni mwake anawaza nini.

Sasa yeye afanye kitu ambacho anaona ni sawa, na Mwenyezi Mungu yuko naye. Kwani alichopitia ni maumivu ya roho na kimwili.
 
Wakati mwingine ni rahisi kusema kutoa au kuilea, ila ukikivaa hiki kiatu mwenyewe ndo unaweza kuwa penye position ya kutoa ushauri mzuri zaid. ni kweli kila moja lina gharama zake mfano ukichagua kulea ni kwamba ni zaidi ya ku adopt mtoto kwani huwezi pata tena mimba nyingine wakati iliyopo haijazaliwa na pia kwa asili ya binadamu kama huyo mtoto atazaliwa kuna uwezekano mkubwa wa kuteswa na hata ndg wengine.

Pia kutoa mimba si kitu cha kukimbilia kama tu vile kunywa maji ya majani ya chai ili utapike, mama aweza kupoteza maisha yake ingawa pia ki-imani imekaa vibaya, cha msingi zaidi kuwatembelea wataalam wa ushauri wahusika wote pamoja (couple), wakati wanashauriwa wawe neutral na baada ya ushauri waulizane wao na kwa kauli moja waamue. Mungu awatangulie, na nawapa pole sana kwa yalowapata.
 
Hapo anahitaji msaada wa kiroho zaidi, Kama ni wakristo wamtafute mchungaji kwa ajili ya couseling na maombi mazito kwa ajili ya kusamehe na kuikubali hali hiyo iliyotokea...kibinadamu sio rahisi kukabiliana na ishu kama hii.
 
Hilo ni swala gumu kijamii na kiroho hivyo wanahitaji maombi mengi pia ushauri wa hali ya juu ila swala la kumtoa huyo mtoto kwa namna yoyote haiingii akilini kwani ni kwa mpango wa Mungu ameipata hiyo mimba Mungu asingeruhusu asingeliingia hivyo Mungu anamakusudi ya dhati na kiumbe chake.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom