Mimba na presha ya kushuka ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba na presha ya kushuka !

Discussion in 'JF Doctor' started by KYALOSANGI, Feb 2, 2011.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Jamani naombeni msaada ,.najua kuna wataalamu hapa watanisaidia .mke wangu ni mjamzito ila ana tatizo la presha ya kushuka ..je nini suluhisho la tatizo hili .je msaada wa kwanza ilikmtokea nifanye nn!
   
 2. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pole sana ndugu kwa tatizo hilo la shemeji? Ni ujauzito wa ngapi? kama si wa kwanza tatizo kama hilo lilishawahi kutokea kwenye mimba nyingine? Ujauzito una umri gani?
  Huduma ya kwanza; Akiwa amelala, hatakiwi kuinuka ghafla na kusimama inabidi akae kwa dakika takriban moja na nusu ndio asimame.
  Endapo atapata dalili za kushuka presha inambidi akae au alale chini mara moja la sivyo ataanguka.
  Mpe mchanganyiko wa glucose/sukari na chumvi kwa ratio ya 6:1 vikiwa vimechanganywa na maji.
  Waweza kumpa glasi moja ya Fanta ikiwa na kijiko kimoja cha chumvi (tea spoon).
  Mshauri aanze kwenda clinic (ANC) kwa ajili ya kuonana na wataalamu, na kushughulikia mwenendo mzima wa afya yake na huyo mtoto aliye tumboni.
  Mara nyingi dalilli hizi zinasumbua kuanzia wiki ya 28 ya ujauzito na by 32 weeks huwa zinaisha kabisa. Baba unatakiwa kumpa support sana mkeo kipindi chote cha ujauzito kwani tafiti zinaonesha kwamba dalili nyingi hupungua kwa akina mama ambao waume zao wako pamoja nao psychologically. Jitahidi kumpa vyakula vya kujenga mwili na kuongeza damu na pia anywe maji ya kutosha.
  Nakutakia kila laheri.
   
 3. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Ahsante sana Mganga wa Kienyeji kwa ushauri wako makini.Huu ni ujauzito wake wa pili.Nitatekeleza yote uliyoshauri.
   
 4. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nshukuru sana, japo mimi ni mganga wa jadi, sio wa kienyeji!!! Dont hesitate to ask any thing any time, JF is your extra brain.
   
 5. d

  docotera Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pia ni muhimu kwa Mkeo aende clinic(ANC) mapema na wacheki utrasound ili kujua matatizo mengine sababu huenda kukawa na pathological condition inayohitaji msaada wa halaka kuna hali zinazojitokeza kwa kipindi hiki tunaita Anterpartum haemorrhage au congenital heart defects(magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo),sasa hayo yote yanategemeeana na hali(degree) ili yajitokezee,kwa hyo suluhisho no hospital kwa wataalamu,ila huduma ya kwanza hapo juu ni muhimu
   
 6. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Pole sana na pia mpe pole shem!! Hili suala limekuwa ni tatizo sana siku hizi sijui ni kwa nini. Wataalamu wanasema maji ya madafu huwa yanasaidia sana katika suala kama hili.
  Ila kwa uwezo wa Mungu, kila kitu kitakuwa sawa.
   
 7. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Amina!
   
Loading...