Mimba hizi hazikubaliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba hizi hazikubaliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Katika ukurasa wa tatu gazeti hili leo kuna habari kuhusu wanafunzi zaidi ya 400 wa shule za msingi na sekondari mkoani Ruvuma kukatisha masomo kutokana na kupata mimba kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
  Habari hiyo inaonyesha dhahiri kuzidi kukwama kwa juhudi za taifa za kumkomboa mtoto wa kike kwa kumpatia elimu, zinasema kwamba mimba hizo zilipachikwa kuanzia Februari 2009 hadi Februari mwaka huu, kati yao 301 wakiwa ni wa sekondari na 98 kutoka shule za msingi.
  Hali hii inaonekana kuzidi kuwa mbaya siku baada ya siku kwani takwimu zilizopatikana mkoani humo zinaonyesha kwamba wilaya ya Mbinga ndiyo imetopea katika vitendo vya upachikaji mimba watoto wa shule kwani hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu, wanafunzi 149 walikuwa wamekatisha masomo yao baada ya kubainika kuwa wamepata ujauzito.
  Janga hilo katika Wilaya ya Songea Vijijini limekumba wanafunzi 106; Tunduru wanafunzi 77; Namtumbo 41 huku Manispaa ya Songea wakikatiza masomo wanafunzi 26 kwa sababu ya mimba.
  Takwimu hizo kwa vyovyote itakavyochukuliwa ni mbaya kwa maana nyingi, kwamba pamoja na mwamko wa hivi karibuni wa taifa hili kujenga shule nyingi za sekondari na kuandikisha shule kwa wingi watoto wenye umri wa lazima wa kuanza elimu ya msingi, bado kuna changamoto za kujitakia katika kuwakomboa watoto wa kike ambao wameachwa nyuma kielimu ama kwa sababu za kimfumo au mila potofu.
  Kubwa zaidi, hali hiyo inaendelea kutokea nchini wakati kukiwa na kampeni za kitaifa kuhakikisha kwamba wote wanaohusika na upachikaji mimba watoto wa shule wanachukuliwa hatua kali za kisheria, kwa sababu vitendo vyao vinazidi kupalilia nguvu za adui mojawapo wa taifa, ujinga!
  Hali hii kwa kweli haikubaliki na haiwezi kuachwa tu hivi hivi kana kwamba ni mapenzi ya Mungu; ni kwa maana hiyo tumeguswa kwa ndani sana na hali hii na kwa kweli tunahamasisha wadau wa elimu wautazame mkoa wa Ruvuma kwa darubini kali zaidi ili kuleta mabadiliko ya kweli kuhusu haki za mtoto wa kike kupata elimu hadi mwisho wa uwezo wake, na kikwazo kisiwe ni mimba.
  Ni jambo la bahati mbaya kwamba wakati taifa likihamasisha uwajibikaji wa jamii katika kukabili janga hili la kuzalisha watoto wadogo na hivyo kuzidi kuwafunga kwenye minyororo ya umasikini wao na wale wanaowaleta duniani achilia mbali kuhatarisha maisha yao kwa kubeba mimba katika umri mdogo, kuna njama za kufifisha mapambano ya kutokomeza mimba kwa wanafunzi.
  Kwa mfano, taarifa ya elimu ya Mkoa wa Ruvuma ambayo wiki chache zilizopita iliwasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC) inaeleza kuwa kuna mapungufu ya namna kesi zinazohusu watuhumiwa waliowapa mimba wanafunzi zinavyoshughulikiwa. Kasi yake ni ndogo sana.
  Watuhumiwa wa udhaifu huu wa kasi ndogo walitajwa kuwa ni maofisa watendaji wa kata na hata mahakama kwa sababu kesi zilizoko mahakamani nazo hazijapatiwa ufumbuzi, hali inayowafanya ‘mafataki’ kuendelea kutamba mitaani kana kwamba wamefanya jambo la kishujaa katika jamii wakati wanafunzi wakiharibiwa maisha yao.
  Tunaamini ingawa hali hii haiuweki mkoa wa Ruvuma katika nafasi ya kutembea kufua mbele kwenye harakati nzima za kumkomboa mtoto wa kike, unabakia kuwa kielelezo na mfano tu wa jinsi changamoto ya mimba shuleni ilivyo kubwa katika jamii yetu. Ipo mikoa mingine, hasa ile ya wafugaji ambayo hali si tofauti sana na Ruvuma.
  Jamii bado haijawa na mwamko wa kutosha juu ya kukabili tatizo hili, kuanzia ngazi ya familia, kwenye taasisi za umma kama shuleni na hata vyombo vya dola katika kuelekeza nguvu zake kutokomeza janga hili la kutengenezwa na tamaa za mwili wa binadamu.
  Ukweli wa mwamko mdogo unajidhihirisha kwenye madaawa yaliyofunguliwa kuhusu mimba za wanafunzi hawa, taarifa zinaonyesha kwamba hadi sasa ni mashauri 10 tu yamefikishwa kortini, 16 yangali polisi na 58 yanashughulikiwa katika ngazi za kata na vijiji. Kwa maana hiyo yapo mashauri 84 tu sawa na asilimia 21 ya uhalifu wote uliofanywa dhidi ya watoto hawa. Tunasema jamii ni lazima ikatae hali hii sasa.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Jamii itakataa vipi sex ambayo in moja ya 'basic needs'? Cha msingi hapa ni kutoa elimu ya uzazi au ngono (sex education) kwa watoto wote ambao wanapevuka. Watoto wenyewe wa kike wanapata hamu ya ngono wanapopevuka sasa ni kosa la mtia mbegu au mpokea mbegu? Au kosa hili liwe kama lile la rushwa, wote wawili wanashitakiwa?

  Kwanza nafikiri mwenye kosa kubwa ni mtoto wa kike kwa kuachia geti wazi kwa hiyari yake na watu kupita pita.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mtoto anaweza kufanya makosa lakini hili zaidi linatokana na utoto wake na sio uzembe au kutojali. Hivyo si haki kumlaumu mtoto hasa kama ujauzito huo amepewa na mtu mzima. Sheria inatambua kuwa mtoto hawezi kutoa 'informed' consent katika suala la kujamiiana.
   
Loading...