Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Takriban watu 65 wamefariki katika milipuko ya mabomu kadhaa katika maeneo muhimu ya pwani yanayodhibitiwa na serikali ya Syria ,ripoti zinasema.
Milipuko ilikumba miji ya Tartus na Jableh.
Milipuko kadhaa ilisababishwa na walipuaji wa kujitolea muhanga,kundi moja la uchunguzi limesema.
Vyombo vya habari vya Syria vinasema kuwa vituo vya mabasi ni miongoni mwa maeneo yaliolengwa .
Ngome za Assad zalipuliwa
Hospitali moja pia inadaiwa kushambuliwa.
Mashambulio kama hayo si kawaida katika eneo hilo.Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza milipuko hiyo.
Chanzo: BBC