Milipuko Dar: Masalia ya mabomu kulipuliwa LEO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Milipuko Dar: Masalia ya mabomu kulipuliwa LEO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, May 7, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,819
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Na Waandishi Wetu (Gazeti la mwananchi)

  WAKATI serikali ikijipanga kuongeza nguvu kuwasaidia waathirika wa mabomu wa tukio la wiki iliyopita Mbagala, jijini Dar es Salaam, kikosi cha wataalamu cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), leo kitalipua masalia ya mabomu ambayo hayakulipuka.

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba, lengo la kazi hiyo ni kuharibu masalia ya risasi, baruti, viwashio na mabomu ambayo hayakulipuka katika mlipuko wa awali uliotokea katika kambi ya JWTZ Mbagala Jumatano wiki iliyopita, na kusababisha maafa na hasara kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

  Jana wakazi wa Mbagala na maeneo mengine walishituka na kutaharuki baada ya kikundi cha askari kupita nyumba hadi nyumba kuwataka waondoke katika maeneo ya karibu na eneo hilo ili utekelezaji wa opareshini hiyo ufanyike.

  Hata hivyo kazi hiyo ambayo ilikuwa ifanyike jana ilisitishwa hadi leo, ili kutoa nafasi ya kuwafikishia taarifa wananchi wote.

  Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, dazani kadhaa za viwashio pamoja na za fyuzi (fuse) zake zitalipuliwa katika zoezi hilo.

  Dk Mwinyi alisema jumla ya mabomu 75 ya kutupa kwa mkono aina ya ‘stick hand grenades, yatalipuliwa katika zoezi hilo.

  “ Kazi hiyo itafanyika kwa umakini mkubwa ili yasilete madhara kwa wananchi,” alisema Waziri Mwinyi.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya jeshi hilo jana, JWTZ imeamua kulipua mabaki ya mabomu hayo ili kuliweka eneo hilo katika hali ya usalana na kuhusu uwezekano wa kambi hiyo kuhamishwa.

  “Unafahamu kwamba, mabaki ya mabomu haya bado ni hatari katika eneo hilo na yanaongeza hofu hata kwa sisi wanajeshi kwani, yako katika hatari ya kulipuka wakati wowote,” kilisema chanzo kimoja na kuongeza:

  “Kutokana na wasiwasi huo ni lazima yalipuliwe pili kuna uwezekano wa kambi hii kuhamishwa kwa sababu gharama ya kuhamisha kambi ni ndogo kuliko ya kuwahamisha raia na kama kambi inahama, haya mabomu hatuwezi kuyaacha na hatuwezi kuyahamisha kwa sababu yanaweza kulipuka tukiwa njiani hivyo dawa ni kuyateketeza kitaalam.”

  Dk Mwinyi alifafanua kuwa kazi hiyo itafanywa kwa utaratibu wa kutanguliza milipuko miwili midogo kwa ajili ya kutoa tahadhari kisha baada ya milipuko hiyo itafuatia milipuko mingine ya mfululizo ya nguvu kiasi.

  Alisema zoezi hilo linatarajiwa kuanza saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni katika kambi hiyo ya jeshi Mbagala.

  Hata hivyo, Dk Mwinyi aliwatoa hofu wananchi kuwa milipuko hiyo haitakuwa na madhara ingawa alitoa tahadhari kuwa wasikae karibu na sehemu ya tukio.

  “Wananchi wanaombwa wakae katika umbali usiopungua mita 500 kutoka eneo la kambi ya JWTZ Mbagala wakati zoezi hilo litakapokuwa linafanyika,” alisisitiza Dk Mwinyi na kuongeza kuwa wizara yake inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

  Alisema wizara yake inawashukuru wananchi wa Dar es Salaam, hasa wa Mbagala na vitongoji vya jirani, kwa uvumilivu na ushirikiano wao waliouonyesha hadi hivi sasa.

  Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati zoezi la ulipuaji wa mabomu hayo linafanyika.

  Lukuvi aliwatoa wasisi kwamba, mabomu hayo hayatakuwa na madhara kama ilivyotokea awali, lakini pia aliwaomba kufuata maelekezoya kukaa mbali na eneo la tukio.

  Hivi karibuni mabomu yalilipuka katika kambi ya jeshi Mbagala na kusababisha zaidi ya watu 24 kupoteza maisha na wengine wakijeruhiwa vibaya pamoja na kupoteza makazi yao baada ya nyumba kuharibiwa vibaya.

  Mpaka sasa serikali imeshatangaza kuwafidia watu waliothirika katika ajali hiyo, ikiwemo kuwajengea nyumba na kuwalipa baadhi ya vifaa vilivyoteketea katika ajali hiyo.

  Wakielezea hofu yao kuhusu kulipuliwa kwa mabomu hayo, baadhi ya wananchi walisema hawana amani na kudai kwamba, usalama wa maisha yao yako hatarini.

  “Kutokana shida niliyoipata siku ile kesho (leo) mimi siwezi kukaa eneo hilo lazima niondoke kabisa ingawa sifahamu nitakapokwenda; lakini nitamchukua mwanangu na kuondoka,”alisema Agnes Ngweli (20).

  Katika hatua, nyingine madiwani wa Manispaa ya Temeke waliungana na watendaji wa kata za manispaa hiyo kushiriki kutoa misaada kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu.

  Tangu zoezi hilo litokea kazi ya kutoa misaada imekuwa ikifanywa na maafisa watendaji wa kata na mitaa katika manispaa hiyo.

  Hata hivyo zoezi hilo lilingia dosari baada ya ofisa mmoja wa JWTZ kutoa taarifa za kuwepo zoezi la kulipua mabomu majira ya mchana.

  Taarifa hiyo iliyowataka wanachi wanaoishi katika maeneo ya jirani na kambi hiyo kutulia na wengine kuondoka katika maeneo hayo kupisha zoezi hilo zililazimisha kamati iliyokuwa ikishughuka na zoezi la kuthamini nyumba zilizoathirika kwa ajili ya kulipwa fidia kuahirisha zoezi hilo.

  Pamoja na hali kuwa hivyo madiwani na watendaji waliendelea na kazi ya kutoa misaada kwa waathirika wa mlipoko wa mabomu hayo.

  Kazi ya ugawaji misaada hiyo ilianza saa tatu asubuhi kwa madiwani hao wapatao 32 kujigawa katika makundi na kuanza kutembelea nyumba hadi nyumba ya mwafrika, huku wakitoa pole na misaada ya vyakula na vitu mbalimbali.

  Diwani wa kata ya Mbagala, Tito Osoro alisema wameamua kutumia siku mbili jana na leo kwa kushiriki ilikuongeza kasi katika ugawji wa misaada kwa waathirika.

  Mkazi wa eneo hilo, Said Mpando aliwashukuru madiwani hao na serikali kwa misaada wanayopewa.

  Hata hivyo watoaji misaada na waathirika zimeendela kutupiana lawama huki kila upenda ukililaumu kundi jingine kwa ufisadi.

  Watendaji wa kata na mitaa ambao ndio wasimamizi waliwatuhumu waathirika kuwa siyo waaminifu kwa kurudi mara kwa mara kuomba misaada kwa madai kuwa hawajapata.

  Mtendaji wa Kata ya Mbagala Juma Chacha alisema yeye anaoushahidi wa jinsi kundi hilo linavyojihusisha na ufisadi huo kwa kujiandikisha na kuchukua misaada na kurudi upya huku wakilalamika kuwa wananyimwa.

  “Usione watu wamefurika tena wakitulaamu eti misaada haiwafikia wakati asilimia kubwa wameshapata,” alisema Chacha.


  Habari imeandikwa na Jackson Odoyo, Tausi Mbowe na Geofrey Nyang'oro.
   
 2. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,490
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Jeshi limetangaza kuwa yatalipuliwa kwa utaalamu mkubwa, bila ya kuleta madhara yoyote.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  taarifa imekuja mapema naamini wakazi wa dar hawatakuwa taken by suprise. ila amini nakuambieni kwa jinsi ninavyowafahamu wakazi wa dar, kuna ambao watakimbilia kwenye tukio wakisikia milipuko ya mabomu. Ah ZIRAILI anaishi kwenye akili za watu kwa sana tu hapa bongo
   
 4. u

  urassa Member

  #4
  May 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taadhari inayodaiwa kuchukuliwa na Jeshi kwa kusema tuu, inapaswa ielezwe ni ya namna gani, sisi siyo wataalam wa mabomu, bali naamini mabomu yakishaanza kulipuka hakuna utaalamu unaoweza kutumika.waseme tutafanya abc ili pamoja na uelewa wetu mdogo tujiridhishe.
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  May 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,099
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  This' something very serious, imani ya watanzania kwa Jeshi letu imepungua, ni vema wengi kuwa mbali kabisa na kambi hii kwani chochote kinaweza kutokea na mkaombwa radhi kwani haikukadiriwa hivyo!
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii taarifa sidhani kama ipoeffective hasa kuwafikia wananchi wote husika kwa muda mfupi hivi. I doubt madhara mengine yaweza kujitokeza. Mungu wabariki na kuwalinda wananchi wa Mbagala.
   
 7. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,490
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Hivi mpaka sasa hivi zoezi linaendeleaje? wenye update tuhabarisheni...
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mpaka sasa hivi haujasikika muungurumo wowote wowote unaoashiria kulipuliwa kwa mabomu (labda kama katika utaalamu wao wameyalipua silently).
  Lakini kwa tahadhari, ingawa waliambiwa wakae at least meta 500 kutoka kambi ya jeshi, lakini wato karibu wote wa aeneo hilo wameyaacha makazi yao na kwenda mbali sana. Naambiwa kuwa tangu mchana eneo lilikuwa kama ghost town
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  walipata taarifa mkuu, wamekimbia wote
   
Loading...