SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kilipata nafasi ya pili katika nafasi ya Rais na idadi kubwa ya wabunge wa majimbo kuliko vyama vingine vya upinzani. Hii ilipelekea kipate ruzuku ya shilingi milioni 333 kwa kila mwezi.
Kwa muda wa miaka mitano yaani miezi 60 chadema itakuwa imevuna bilion 19.98 lakini ajabu haijafanikiwa kumiliki ofisi zake yenyewe zitakazotumika kama makao makuu, au mradi wowote, au ofisi hata ya chumba kimoja katika kanda nk
Hivi waungwana ikiwa chama hiki kinashindwa kufanya matumizi sahihi ya ruzuku yake wataweza kusimamia hazina ya nchi?
Mara kadhaa Mwenyekiti wao wa Taifa amenukuliwa akieleza wao hawajengi majengo kwa ajili ya ofisi bali wanajenga fikra. Swali ni kama hawahitaji Majengo kwanini watumie mamilioni kukodi majengo kwa matumizi ya ofisi za makao makuu? Je, hawahitaji kuwa na mradi kama kitega uchumi?
Ikumbukwe vita kubwa ndani ya chama hiki tangu wakati wa marehemu Chacha Zakayo Wangwe, Zitto Zubeir Kabwe, Prof Kitila Mkumbo nk ni ruzuku.
Najua hizi habari za matumizi ya ruzuku hazipendwi maana tunaoneana haya ila tunapenda kuhoji matumizi ya serikali kuu kwa madai ni kodi zetu bila kusahau hata ruzuku za vyama ni kodi zetu!
Sent using Jamii Forums mobile app