Milion 2 au 3 inatosha kununua gari?

Milion 2 au 3 inatosha kununua gari?

Yusomwasha

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
2,092
Reaction score
844
Naomba kuuliza nikiwa na,mil 2 au 3 naweza kununua gar ndogo ya kutembelea?
 
Unaweza ila spana mkononi,
Litakupa stress, kila siku garage
 
Naomba kuuliza nikiwa na,mil 2 au 3 naweza kununua gar ndogo ya kutembelea?

Mimi ninayo chaser 4s tairi mpya imelipiwa road licence hadi Machi,2016 ni nzima kabisa ni kuweka mafuta na kuondoka inakwenda kwa mil 3 fixed price
 
Unaweza kununua Ila utatumia mda mwingi garage kuliko barabarani.
 
Mimi ninayo chaser 4s tairi mpya imelipiwa road licence hadi Machi,2016 ni nzima kabisa ni kuweka mafuta na kuondoka inakwenda kwa mil 3 fixed price

weka picha, milage, umeitumia miaka mingapi
 
mkuu kuna jamaa ana toyota carina inakwenda kwa laki tano kama uko siriaz na biashara nipm
 
Naomba kuuliza nikiwa na,mil 2 au 3 naweza kununua gar ndogo ya kutembelea?

Inawezekana kabisa ndugu kupata gari kwa bei hiyo na vile vile inategemea na gari uliyoipata maana kuna watu hapo chini wanasema utatumia muda mwingi garage! Ukitaka kununua gari za bei rahisi, kwanza unaangalia engine na gear box ni nzima? ukiona hivyo vitu ni vizima unaenda kwenye body na kama body inaridhisha unainunua. Mara nyingi gari za bei rahisi huwa zina madeni makubwa TRA ila sio yote. Mfano kwa hela yako unaweza kupata kama Chaser baloon, Chaser mayai, Collora na jamii nyingine ya toyota. Na vile vile kwa hela yako hiyo hiyo unaweza kupata Nissan March ile ya mwaka 1998 ingawa spea zake zipo juu kidogo. Katika maisha yangu nimetumia gari tatu na katika hizo gari tatu zoote zijawahi kununua gari zaidi ya shilingi 2,500,000/= na katika gari hizo nilizotumia hakuna gari hata moja iliyonisumbua kwa mafundi, nanunua gari mimi ni mafuta maji na oil na gari haijawahi kunisumbua kwa mafundi kwakuwa katika kununua gari ya bei rahisi hautakiwi kuwa na papara na ndio hicho mimi kinanisaidia. Ila katika gari hizo nilizonunua zilikuwa zinadaiwa tra, gari yangu ya kwanza Nissan March ya mwaka 1998 nilinunua ikiwa engine, gearbox na body vikiwa safi na tra ilikuwa inadaiwa 215,000/=, gari yangu ya pili ilikuwa nissan march ya mwaka 2004 ilikuwa inadaiwa 312,000/= na gari yangu ya tatu Chaser mayai ilikuwa inadaiwa 287,500/= kwahivyo kwa hiyo hela unapata gari saaaafi mkuu!
 
Safi kiongozi!
Umempa mwongozo mzuri..!
Nadhan hao hapo chini huwa wanakurupuka na
ndio maana ushauri wao unaishia...
spana mkononi mara kuw fundi mara garage!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom