Milima ya Kitonga ni Milki ya nani?

Rene Jr.

JF-Expert Member
Jan 31, 2014
3,714
2,374
Salaam wakuu,

Kila siku huwa napita maeneo haya lakini sijawahi kujiuliza swali hili. Bahati mbaya au nzuri tulipita maeneo haya na mdau mmoja tukapata wazo fulani lililopelekea kujiuliza sehemu ya kuanzia.

Je, sehemu hii ya Bonde la Ufa iko chini ya milki ya nani? TANAPA wanahusika, au mamlaka nyingine, au ni mapori ya wazi tu, au kuna mtu/watu/taasisi inamiliki vipande vya ardhi?

Kuna shughuli tunaangalia uwezekano wa kuifanya kwenye maeneo haya ya kuvutia. Pia kwa vile Tanzania ni kubwa naomba mawazo yenu wadau, ni maeneo gani tena yaliyo na milima na mabonde makubwa na yenye kina kikubwa, kukiwa na maporomoko ya maji, mito, au kingo za ziwa/bahari ni nzuri pia.

Natanguliza shukrani.
 
nazani yata kuwa chini ya wizara ya maliasili na utalii kama mapori tengefu/Msitu, TANAPA hawahusiki na uhifadhi wa misitu so kitonga czani kama ipo chini yao.
 
Jaribu kwenda udzungwa national park njia ya ifakara kabla hujafika maeneo ya mang'ula palipo na makao makuu ya hifadhi hiyo ya udzungwa kuna sehemu panaitwa sanje hapo kuna maporomoko ya maji yanaitwa sanje water falls ila hayo maporomoko yapo chini ya hifadhi ya udzungwa so uwekezaji watu wanao ufanya n hoteli za kitalii na camp site... maporomoko mengine ni hifadhi za milima ya uluguru juu kule kama unaenda kwa mkuu wa mkoa.. au ukipanda zaidi kwenda morning site..
 
7187893.jpg
 
Salaam wakuu, kila siku huwa napita maeneo haya lakini sijawahi kujiuliza swali hili. Bahati mbaya au nzuri tulipita maeneo haya na mdau mmoja tukapata wazo fulani lililopelekea kujiuliza sehem ya kuanzia. Je sehem hii ya bonde la ufa iko chini ya milki ya nani? TANAPA wanahusika, au mamlaka nyingine, au ni mapori ya wazi tu, au kuna mtu/watu/taasisi inamiliki vipande vya ardhi? Kuna shughuli tunaangalia uwezekano wa kuifanya kwenye maeneo haya ya kuvutia. Pia kwa vile Tanzania ni kubwa naomba mawazo yenu wadau, ni maeneo gani tena yaliyo na milima na mabonde makubwa na yenye kina kikubwa, kukiwa na maporomoko ya maji, mito, au kingo za ziwa/bahari ni nzuri pia.
Natanguliza shukrani.



Ardhi yote TanZania ni mali ya Serikali na chini ya usimamizi wa Raisi wa JMTZ!
 
Pita njia ya iringa mjini kwenda Dodoma kupitia mtera ,utakutana na milima mikali inayoitwa Nyang'oro
 
Ardhi yote TanZania ni mali ya Serikali na chini ya usimamizi wa Raisi wa JMTZ!

Uongo mtupu
Soma Land Act vizuri
s. 4. All land vested in the President as trustee
(1) All land in Tanzania shall continue to be public land and remain vested in the President
as trustee for and on behalf of all the citizens of Tanzania.

Mzee Tupatupa
 
Uongo mtupu
Soma Land Act vizuri
s. 4. All land vested in the President as trustee
(1) All land in Tanzania shall continue to be public land and remain vested in the President
as trustee for and on behalf of all the citizens of Tanzania.

Mzee Tupatupa


Sasa nilichongoopa hapo ni kipi? Embu tafsiri hivyo vifungu vya sheria ulivyovinukuu wa Kiswahili kama Ukiweza/ukipenda!
 
Last edited:
Back
Top Bottom