Mil 2.5 za mahari zamkimbiza kijana

ikyenja

Senior Member
May 28, 2013
103
52
Wadau amani iwe kwenu.

Nina dada yangu aliekuwa na mchumba aliepatana nae wakiwa chuo kikuu huko Dar Es Salaam.
Baada ya chuo kila mmoja akaenda njia yake kurudi makwao likizo.
Bahati nzuri wote wakaajiriwa mwaka ule Mhe Magufuli anagombea kwenda Ikulu, mahali patakatifu kabisa.
Baada ya ajira na kujiridhisha kimaisha wakakubaliana kutambulishana rasmi kwa maana ya kijana kupeleka kishika uchumba.
Akafika nyumbani kwa wazazi wa binti na kupokelewa vizuri. Taratibu zikakamilika. Akaja kupewa jibu mahali ya binti ni sh mil 2.5. Kijana akakubali, akarudi kwao huko mkoa wa misitu. Baada ya muda akaleta mahari kama ilivyo kubaliwa.

Tukaja kushtuka mahusiano yao yanadorora sambamba na afya ya binti kudorora kwa sababu ya stress. Kuulizia kulikoni. Kumbe kijana anamfanyia visa mwenzie. Na uchumba wao kwishney. Hatujui sababu ni nini hasa!!!


Tuyaache hayo. Mimi mwenyewe sitaki kabisa kusikia habari za harusi, nimevuta binti awe mke wangu, kama tulivyokubaliana kwamba tukae pamoja angalau mwezi kabla ya kutangaza ndoa rasmi. Hii ni kwa sababu mimi nakaa mbali sana toka mkoa wa nyumbani. Binti mwenyewe ni yatima, hivyo maisha yake ni kutanga tanga tu, Mara akae huku, mara kule.

Sasa sekeseke limeibuka, wazazi walezi wa binti wamesikia binti yao yuko kwa bwana ikyenja. Wameanza kudai pesa ya kujionesha sh laki nne, baadae ndipo nitaambiwa kiasi cha mahari. Mimi nakataa kutoa pesa hiyo maana naiona kama mahari yenyewe, kwa maisha haya ya vijijini ingawa mimi ni mfanyakazi serikalini. Nina maana sinunui mke bali natanua ukoo na kuendeleza undugu, ya nini kusumbuana. Ingawa kwa utamaduni wetu nawajibika kulipa na nitalipa kweli bila kinyongo.

Sasa nataka kuwaambia wazazi wote wenye tabia kama hizi waache maana huwafanya binti zao kukimbiwa.
 
Kwahyo dada yako amemwagwa na jamaa japokua katoa mahar ama ni vip?
 
eti hadi siku hizi ukienda kuoa uluguruni bila milioni 1.6 hupati mke
fumbaf thana, mtu anaitamka kabisa 1.6 utadhani hata hesabu za desimali kashawahi kuzisoma.
wakafe mbele huko na 1.6 zao, kama vipi wawaoe wenyewe hao binti zao kama wanaona vijana wanafaidi.
 
Nyie mnataka kuoa,unategemea upewe mtoto wa watu bure?maana ya uanaume wako ni nini sasa?acheni woga toa mahari upewe mke,ww ndio muoaji,kama unataka usaidiwe kulipiwa mahari wanajamii wakuchangie mahari jamii nzima imuoe mkeo,itisha mchango tukuchangie,acheni kulia lia huku mitandaoni,lipa mahari gharamia mtu wako.
 
Mimi nimeambiwa milioni 1.215/25. Kwanza nilishangaa hizo cent mimi nazipata wapi? Na kwa nini walitamka hela nyingi hivyo? Nilipangiwa kulipa desemba. Hadi leo bado natafuta hiyo hela. Nawaza sijui niishie njiani
 
Hafadhali ya huyo 2.5 mi nimeambiwa Ngombe 25 kwa wasukuma huko sijui wanataka niwafungulie zizi au lakini binti yao nimempa tayari kibend watanitafutaaa tu
 
Mimi nimeambiwa milioni 1.215/25. Kwanza nilishangaa hizo cent mimi nazipata wapi? Na kwa nini walitamka hela nyingi hivyo? Nilipangiwa kulipa desemba. Hadi leo bado natafuta hiyo hela. Nawaza sijui niishie njiani
Ahahhaha umenichekesha sana Mkuu...
Na demu unahitaji usikimbie Chukua mwanamke then wapige Calendar watajua tu kuwa usawa unakaba.
 
Mbona 2.5 jamani sio nyingi,na hata kama huna siunatoa nusu mnakubaliana,kuna watu wanaolewa mpaka kwa M10-20
kama hali hairuhusu zungumza na mshenga wako wakaongee wataelewana tuu,msiwache kuoa eti kisa mahari nyingi..
 
Mbona 2.5 jamani sio nyingi,na hata kama huna siunatoa nusu mnakubaliana,kuna watu wanaolewa mpaka kwa M10-20
kama hali hairuhusu zungumza na mshenga wako wakaongee wataelewana tuu,msiwache kuoa eti kisa mahari nyingi..
Mkuu, sio nyingi lakini kwa mantiki ya mambo ya kuoana ni nyingi sana. Wakati natajiwa mahari, sikuona kama pesa wanayosema ni nyingi, lakini kuna mambo yanaambatana na mila za huko unakooa, unaweza kushangaa baada ya kutoa 2.5M ukatoa tena, hapo kuna blankets, mbuzi, kondoo, chakula.

Hapo bado sherehe hujaipigia mahesabu. Yaani ukimlipisha kijana mahari ya 2.5M maana yake enhanced na sio chini ya 7M toka mfukoni mwake hadi sherehe iishe.

Kwa usawa huu tunarusdishana nyuma.
 
eti hadi siku hizi ukienda kuoa uluguruni bila milioni 1.6 hupati mke
fumbaf thana, mtu anaitamka kabisa 1.6 utadhani hata hesabu za desimali kashawahi kuzisoma.
wakafe mbele huko na 1.6 zao, kama vipi wawaoe wenyewe hao binti zao kama wanaona vijana wanafaidi.
Uluguruni wagundua kutaja mamilioni siku hizi bro wangu ametajiwa mahari ya 1.9 m bila kupepesa macho
 
Yani utoe hayo mamilioni, na bado tena kuna yale mengine marupurupu kama vile: kanga za shangazi, pombe za wazee n.k yani ukija piga mahesabu unaweza jikuta umenunua Range rover sport.



Alafu huyo mwanamke akakuletee ujinga ndani. Si unaweza ukaua?





☆Steve
 
Back
Top Bottom