Maguge Maguge
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 2,734
- 1,781
Ndg Wana Jamvi, neema ya bwana iwe nanyi nyote!
Mwenzenu yamenikuta, sijui hata ninakoelekea ni wapi.
True story:
Nilifungua biashara ya electroncs mwaka 2007, Mwaka 2009 nikawa nimemaliza kujenga ka kibanda.
Nikaenda benki moja kukopa, niliwalipa na kumaliza deni kabla ya muda,
Nikakopa tena, nikalipa nikamaliza,
Nilikuwa mteja bora nikapanda kiwango cha kukopa;
Nikajenga ka kibanda ka pili,nikanunua ka usafili
Maisha yakawa yanaenda vizuri,
Nimekopa hadi awamu 9.
Lakini ilipofika awamu ya saba mtaji uliyuma sana, biashara ilianza kwenda vibaya, nikikuwa naamini kwamba biashara yangu haieksipai lakini kilichonikuta,
Ziliingia kwa kasi bidhaa zenye usb port, flat screen, mara fununu za kuzimwa matoleo fulani ya simu,
cd na tape zikapuuzwa,
mara eti Tv za kisogo hazitafanya kazi,
Na hapo tayari nikawa nishachoka kabisa!! Na ni
ndani ya mda mfupi ambao nilikuwa na mzigo wa pesa nyingi, (hapo nimetoka nje ya nchi na mali ya kutosha) na nilikuwa muuzaji wa rejareja, kwa hiyo nikawa sipati hela ya kurejesha mwezi ukiisha, hivyo nikaanza kuwa nakopa kwa watu ili nikalejeshe!
Nikaanza kupiga mnada zile mali ili ziishe!
hii ilinifanya kuishi kwa kuhamishahamisha madeni,
Kwa kuwa nilikuwa siuzi vizuri hata fedha kwa ajiri ya watoto wa shule zikabaki ni za kukopa,
Nilianza taratibu kuwa nasikia moyo unalipuka katika mtindo fulani, nadhni ilikuwa kukosa utulivu wa Ki mawazo.
hali hii nilihisi itanipelekea kupata BP, nikaanza kufanya mazoezi ya kuipotezea.
Ilipofika mwezi wa pili mwaka huu, nilishindwa kabisa kurejesha pesa benki, nikiwa nimebaki na madeni ya 25,000,000/-
Nikauza kile ki usafiri.
Nikaendelea na mazoezi ya kuyachukulia poa matatizo yangu. Mwisho ile hali ikaisha, nikawa mpuuzi sana nikayaona kama hayakuwa na uzito wowote!
Sasa mziki ukaja, Nikawakabidhi nyumba moja benki wauze wenyewe kuepuka stres
pale nilipoamua nikakae nyumbani kuendeleza kiduka kilichokuwepo home, baada ya kufunga lile duka la electronics
Watu wana mazowea ya kukutana na tatizo kidogo, wananuna, ukimsemesha kidogo anakwambia niache, nina stres!
Wapuuzi sana hao!
Ndugu yangu,
Hali ni mbaya sana, mteja anaweza kuniambia nipe sigara tatu na kiberiti nikampa sigara moja halafu nikawa nimesahau kingine, mpaka aseme tena nimesema tatu na kiberiti ndipo akiri hustuka kidogo, akija mwingine, nipe sabuni ya unga ya mia mbili,ya kipande ya mia mbili, nampa vyote, (labda kanipa 2000) namuuliza na nn tena anajibu hamna kingine, pengine najikuta nimemrudishia chenji yake na hela aliyonipa, nasikia tu " hii ndiyo niliyokupa" yaani kila kitu sasa hakiendi!!
Na kwa sasa sina mtu anaeweza kuwa katika shughuli hii hata sielewi cha kufanya.
Na kwa hayo yote naamini yametokana na mikopo maana zamani sikuwa hivi!
Na nimefanya biashara miaka 26, hiyo biashara iliyofilisika haikuwa ya kwanza kwangu ila huwa nabadilisha biashara kutokana na wakati na mazingira pia
Sasa mwenzenu yamenikuta!!