Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa katibu wa wizara ya elimu mstaafu "Maimuna Tarishi " akisema kama umesoma private school hupati mkopo.
Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hiko . na tukasema sio fair sababu .
1.gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8,au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia Ndoto zao kabisa.
2.pia nakumbuka tulihoji kuwa uwezo wa mzazi haupo constant, mfano. Kipindi mtoto akiwa anasoma private mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa ,kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefirisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake.
3.pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ,ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe .ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools. Sio fair.
4.tulihoji pia wapo waliosoma kwa kuresit mitihani kutafuta credits Mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools,wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao.
Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama.
Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho
Kama kipindi hiki, tuwaasi bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai.
Kama Bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo"ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia Sana hii kama ikiwa inaeleweka.
Abdul Nondo.