Mikopo na watanzania

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
2,270
2,000
Kama tulivyosikia IMF watanzania wana tatizo la kulipa pindi wanapokopa. Wana jamvi tujadiri tatizo ni nini maana kwa uzoefu hata kati ya mtu na mtu utamaduni wa mtanzania ni kuwa tunapokopeshana kulipa inakuwa matanga tatizo ni nini.si watanzania wa nchini tu hata wale watanzania walioko nje wanaogopa kukopeshana kwa sababu mojawapo ikiwa hiyo hiyo .karibu tujadili
 

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
3,025
2,000
Ebu fikilia kwanini ulikopa ukipata jibu utajua ndio maaana kulipa tatizo

Kiufupi hakuna mtu anayependa kukopa, alafu akatae kulipa tatizo ni kwamba unakopa ukiwa na matatizo na unapopata ile pesa uliyotegemea kulipa unakuwa bado Upo kwenye matatizo

Ndio maaana tunashauliwa unapoitaji mkopesha mtua angalia haki ya kipato chake mda huo sio kisa mnajuna tu unampa pesa hapana.

Mfano unajua kabisa miye nadaiwa na watu zaidi ya wanne sijalipa deni, au na familia kubwa ambayo kwa kipato changu ni vigumu nikakukopa pesa alafu nikakulipa kwa wakati ikiwa hiyo pesa ndio pato langu kwa mwezi au wiki

Kwaiyo unapokopesha kuwa makini pia usipendi mazoea ya kwenye pesa na mtu, kuna watu wao matatizo hayaishagi kila siku anataka akukope wewe tu wewe tu wanini uyo mtu piga chini
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,267
2,000
watanzania wengi wakikopa hawana utamaduni wa kulipa ndio maana benki zetu zikatolewa bure halafu tunalalamika tumeibiwa ni kweli katika watu kumi ukikopa ni mmoja atakayekulipa bila mikwaruzano
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
4,002
2,000
watanzania wengi wakikopa hawana utamaduni wa kulipa ndio maana benki zetu zikatolewa bure halafu tunalalamika tumeibiwa ni kweli katika watu kumi ukikopa ni mmoja atakayekulipa bila mikwaruzano
Wakopesheni kwa riba za kibinadamu muone kama watashindwa kulipa.

taasisi za fedha nyingi riba asilimia 5-10 kwa mwezi, kwa mwaka ni hadi asilimia 100. Watalipaje? Bishara ngapi zina faida ya asilimia 100 kwa mwaka?

Benki chache ndio zinakopesha asilimia 20-30 kwa mwaka. Hii bado kubwa sana. Kwani kwa wastani biashara zina faida ya asilimia 15-20 tu kwa mwaka.

Hivyo wengi wanaochukua mikopo huishia kusababisha capital errosion. Sasa huu mchezo unafanya kazi mkopo wa kwanza na wa pili labda. Baada ya hapo lazima ufeli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom