'Mikopo kwa wanafunzi bado ni tete'

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,070
253
UPATIKANAJI wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchinio, bado ni tete na jana wanafunzi kadhaa walivamia ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi jijini Dar es Salaam wakilalamikia kucheleweshwa kwa fedha hizo.

Habari zilisema hadi kufikia jana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro, Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam, walikuwa bado hawajapata mikopo.

Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na gazeti hili walisema kitendo hicho kimewaathiri kisaikolojia na hata kulazimika kukopa fedha kutoka kwa watu.

Mwanafunziwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwesigwa Christian alisema kuchelewa kwa mikopo hiyo kumemfanya ashindwe kuhudhuria masomo.

"Mpaka sasa hatujapata pesa zetu, jambo linalotufanya tushindwe kuingia darasani kwa kukosa nauli na njaa," alisema Mwesigwa.

Alisema kwa jumla wanafunzi, wamechoshwa na utaratibu wa bodi hiyo katika kutoa mikopo na kuiomba serikali kuingilia kati jambo hilo.

"Kila tukija tunapangiwa tarehe na kupewa sababu zisizokuwa na msingi mara hatujajaza fomu, mara majina hayaonekani hatuelewi kwa kweli,"alisema Jonh Revocatus.
 

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,194
1,432
.....nilisikia wakati fulani kabla ya uchaguzi kwamba vyuo vya elimu ya juu vitachelewa kufunguliwa hadi 5/11/2010 (wiki 1 baada ya uchaguzi mkuu) ili bodi ya mikopo ya wanafunzi ikamilishe malipo,what went wrong? je, dhana ya kuogopa wanafunzi hawa ambao wengi hawaifagilii CCm ina-prove true? CCM bana!!!!!!!!!!!!!!!


/
/
 

mfarisayo

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
5,161
2,001
Wakomae tu watamaliza kiubishiubishi. Kwa wale wa UDSM watakumbuka tulikula sana RB 600 ( Rice and Beans kwa tsh 600) na tulilalia sana mikate.
 

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
696
12
Mmmmmh wawape tu hela hawa vijana maana huku mtaani sasa wanagawa kama pipi kwa watu wenye nazo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom