Mikogo mingi humuogopesha uliyenaye/unaye mtarajia

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
MIKOGO MINGI UMUOGOPESHA ULIYENAYE/UNAYEMTARAJIA.

Katika mahusiano malingo, pozi na mbwembwe zinanafasi yake kuleta ashiki ya mapenzi. Lakini yanapozidi huleta hofu kwa mwenza/mpenzi.

MIkogo hizi ni pozi, malingo, mbwembwe na namna yoyote ile mwanaume au mwanamke uamua kujiweka kwa mpenzi wake. Mwanamke ni pambo na Mwanaume pia ni pambo, hatukatazwi kuwanogesha wenza wetu kwa mikogo kwani ufanya ujipambanue kitabia, kimahitaji, kijinsia na kimsimamo iwe hadharani ama faraghani ndio uleta radha na uelewa wa mapenzi, ila vikizidi mmh! uwa ni chefu, umshusha thamani mtu.

Kwanini mikogo inapizidi katika mahusiano huweza kumuogopesha uliyenaye au unayemtarajia, jifunze hapa:

Penzi kudumaa. Mpenzi mwenye malingo,pozi na mbwembwe za ovyo zisizo kuwa na mipaka wala utu. Ulifanya penzi lisikue, kila siku mnapokutana ni kama mnatongozana ama ni kama hamjafahamiana. mf: mtu sms kujibu mpaka ajisikie, ukimwambia jambo ni mpaka ajivute japo lipo kwenye mwili wake ama uwezo wake.

Wengine kila uamuzi "baba kasema" "dada kasema" hawezi kufanya jambo bila sauti ya watu. Hii inaonyesha wewe huna ujasiri kwa mpenzi wako, huna moyo na mwenza wako, bado huna hali na mahusiano yako. Chukulia leo umekesha na mpenzi wako mnachati na kupigiana simu alafu kesho, ghafla meseji hajibu na simu hapokei, yaani kaamua tu bila kosa.

Kukosa shukrani Kuna wapenzi wanapozi mchongoma yaani zinaumiza, unampa fedha, mali, kitu ama zawadi, anaipokea kama kashika uchafu, anaipokea hata neno la shukrani hakuna. Unapojitoa kumpa chochote hawezi kukiona kizuri mpaka aambiwe na marafiki ndio atakwambia kile ni kizuri.

Unamfanyia jambo ila hata kulithamini kama ni nguo kuivaa au chochote ulichompa kukitumia hatomuona katu nacho. kuna jamaa anasema alimpa sapriizi mpenzi wake ya simu, baada ya siku mbili, anarudishiwa kisa kuna rafiki wa huyo mpenzi wake anatumia simu kama ile hivyo, akamnunulie nyingine. Hii inaonyesha hauishi kwa ajili ya uliyenae bali watu, inaonyesha sio hadhi yako, ni mbinafsi na mtu mwenye tamaa. Thamani itashuka tu.


Utesaji Wapo wapenzi wanathaminiwa ila wana vitabia vya kununa nuna mara kwa mara na kufoka ovyo si wa kike si kiume. Mwenza anaona raha moyo wa mwenzie unavyoteseka kumbembeleza. Ajabu moja, unakuta wenza wamejamiana mpaka kama ni vyuma vingekuwa vimeisha ila ukiwa nae busu tu mbinde, yaani kila kitu kwake ni mpaka ukabe.

Salamu kuitika mpaka ajisikie, kwa wale wa gheto, anakuja alafu analeta minuno na si mara moja kila mara ndio pozi zake. Punguza pozi zenye kutesa hisia za mpenzi wako na kama unafanya isiwe mazoea, fanya kwasababu. Utaonekana hujali au umezidi kujishaua, sio poa.

Stara Sio kila mtu anaweza fanya unalotaka wewe, kuna mpenzi yeye ni mtu wa kujionyesha na hana aibu, hana faragha mko njiani anataka akubusu, akupe mate, akukumbatie au namna yeyote itayoonyesha mahaba. Mmekaa mahali kuna viti viwili anataka umpakate au akupakate ili iweje! Hajali rafiki, wazazi wala ndugu.

Hizi pozi sio utamaduni wetu wa afrika. Utaonekana mhuni, limbukeni, malaya na huna adabu. Stara ni msingi wa utu wako.

Kutotabirika Unapokuwa na mahusiano na mtu anayetabirika ujenga matumaini na ujasiri kuwa ni wako na mtafanya mengi ya maendeleo. Ila unapokuwa na mpenzi yupo kama jiwe, kila kitu uanze wewe, yaani wewe ndio mwenye shida sana kwake, huwa inatia mashaka ni wazi huna la muhimu kwake. Ukisema hiki anakitumia sana nimnunulie atasema kibaya usingenunua, twende tukafurahi mkifika kanuna mara kazua ugomvi.

Fedha yake na maisha yake hayako wazi kwako, hata kwa ndugu zake hujulikani na muna muda mrefu katika mahusiano, huwezi kutabiri hatima yako.

Utajifunza kuwa, sisi watu tunapoanzisha mahusiano, tunakutana watu tuliolelewa na wazazi tofauti hatufanani, unapokutana na mpenzi mwenye mikogo ya ovyo, unakosa kumuamini kama ni mtu sahihi kwako, kuwa na mtu anayesema anakupenda lakini mikogo yake inakutesa na kukuumiza ni wazi ni tatizo.

Lazima tujue mapenzi ni starehe na ni nguvu ya maendeleo na sio chumba cha mateso, lazima ujue mapenzi ya dhati hayapimwi kwa kumtesa mtu, huo ni ushetani acha, punguza mbwembwe na kujishaua kwingi wewe mwanaume/ mwanamke unaharibu, jitambue upo katika mahusiano kwa lengo gani, sio muda wote mtu huwa yule yule chizi anayevumilia maumivu uumpayo.

Na mwandish mmmuhumba
# mnogeshe umpendae#
# Acha unyanyasaji#
#Mapenzi bora ni afya ya akili#
#imarika#
 
Kuna wanawake wanaboa yaani utatoka kumkwichi kichi halafu mara mkiachana simu hapokei usiku wake,wake kesho yake na ukimfungia vioo ananza kupiga kama fire na weweusipopokea anaanza kujiliza liza hovyo kuwa simpendi
 
Wakati naanza kuusoma huu uzi in my head ilisomeka hivi"MIKONGO MINGI HUMUOGOPESHA YULE ULIYENAE/UNAYE MTARAJIA" kumbe sio hivyo daaah eniwei naunga hoja mkuu
 
Wakati naanza kuusoma huu uzi in my head ilisomeka hivi"MIKONGO MINGI HUMUOGOPESHA YULE ULIYENAE/UNAYE MTARAJIA" kumbe sio hivyo daaah eniwei naunga hoja mkuu
Karibu makala nyingine
 
Back
Top Bottom