Mikoa yote ya Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikoa yote ya Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TODO, Jan 26, 2012.

 1. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nikifiri mara kadhaa juu ya namna mikoa yetu ilivobarikiwa kwa namna ya kipekee kiasi kwamba sifa ya mkoa mmoja kwa maana ya mali asili haufanani na mkoa mwingine.mfano sumbawanga kilimo cha nafaka kinakubali sana na maeneo yote ya jirani, arusha tanzanite kwa uchache, kanda ya ziwa dhahabu,kigoma mawese, mtwara korosho n.k

  kwa maana nyingine Tanzania inahitaji vitu vitatu mhimu ili iondoke kwenye kundi la nchi ombaomba.na vitu hvo ni better thinking,customer focus na excution.

  ni kweli elimu ni mhimu lakini mbona wasomi wetu wanatuangusha kwenye maswala ya kiutendaji.si ajabu kukuta taasisi fulani inakufa lakin ukiangalia cv ya watu walioko ndani unashindwa kuelewa elimu yetu inatusaidia vp kutatua matatizo yetu

  naendelea kufikili njia bora ya kumkomboa mtanzania je kuendelea kutumia elimu hii hii ambayo mfumo wake tuliachiwa na wakoloni au tukae chini tutafute mfumo mwingine wa kuelimishana? maana siku hizi usishangae kumkuta mtu wa miaka 23 ana masters.changamoto inakuwa pale ambapo ukikaa naye mtu wa namna hii hatoi matokeo yanayofanana na masters.

  kwa ujumla kama nchi tunakazi ya kutambua tunu zote kwa kila mkoa na kutoa maamzi nn kifanyike wapi na kipi kisifanyike wapi ili kwanza tutengeneze soko la ndani la uhakika halafu twende soko la nje kwa ziada

  kwa leo nimepata nafas ya kujadili haya.

  witi.Natoa wito kwa wenye uwezo wa kufikliri vizuri tusaidie nchi yetu tuondokane na matatizo tuliyonayo.wakati fulan mtu mmoja alisema uwezo wa kutambua tunataka nn tunao lakni uwezo wa kupata majawabu ya tunachokitaka ni tatizo, je ni kweli? swali hili ni langu na lako.
   
 2. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Todo na Wana JF,
  Hivi vitu vvyote ni Mwenyezi Mungu ametupendelea na kutujaalia, ndio maana wenzetu Nchi zilizoendelea ukiwaambia sisi ni Maskini hawatuelewi, Kikubwa ambacho tunashindwa kuendelea na tutazidi kushindwa kuendelea ni Kumwacha MUNGU, tunatumia akili zetu bana, na haya yote yanayotokea sasa (Maandamano, Migomo, Tsh Kushuka dhamani, Bei za vyakula kupanda, maisha magumu kwa mtanzania, Nishati aka Umeme n.k) MUNGU anajaribu kutuweka sawa na tusipojirekebisha atatupa pigo lingine kali kuliko sasa.
  Pili, Viongozi wetu wametoka kwenye mistari ya Uongozi, yaani maadili ya uongozi, miiko ya uongozi, kwa ujumla Sheria za Nchi hazifuatwi na kila mtu anasema aka kutoka kivyake, hakuna wa kumfunga nyau aka paka kengele. Wamesahau kuwa Uongozi ni Dhamana. Na hili ndio tatizo kubwa linalotukumba.
  Tatu, Uoga wa kufikiri na kufanya maamuzi, kidogo hili sasa hivi watanzania wanaanza kuamka na kujua haki zao za msingi na majibu yake tunayaona na kuyasikia katika baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Mbeya na kwingine.
  My Take: Kila kitu happen for a reason, tuzidi kuiweka Nchi yetu Tanzania kwenye maombi na tuanze kubadilika.
  Nawakilisha

   
Loading...