kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,734
Wadau.
Nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wetu kwa kazi nzuri ya utumbuaji MAJIPU inayoonyesha kuwa inataka kuleta nidhamu ya watumishi wa Umma wawapo kazini kwani inatupa faraja sisi wananchi wa kawaida
Lakini cha kusikitisha niweke wazi hadi sasa hali ya utoaji huduma Afya katika Mikoa minne hapa nchini ni tete kutokana na serikali kutopeleka fedha za Mfuko wa pamoja yaani Basket Fund, Mikoa hiyo ni Lindi, Tabora, Shinyanga na Kigoma. Kigoma nimeweka Red nina fununu kuwa wamepelekewa lakini sina uhakika kwani walikuwemo kwenye kundi hili.
Ifahamike wazi huduma bora za Afya katika maeneo hayo zinategemea sana fedha za Mfuko huo lakini cha kusikitisha hadi sasa serikali haijapeleka fedha katika Mikoa hiyo tangu mwaka wa fedha uanze yaani July 2015 na kutokana na hilo sasa hivi katika Hospitali nyingi za Serikali katika Mikoa hiyo hakuna Vifaa tiba, Dawa NK.kwani hadi sasa Robo 3 zimeishapita bila kuwa na fedha zozote Na hii inafanya jamii husika kutopata huduma stahiki za Afya kulingana na mipango ya Mikoa na halmashauri husika.
Tukumbuke Miongoni mwa Mikoa hii ni Mikoa ambayo anatoka PM na Naibu Waziri wa Afya lakini cha kusikitisha Mikoa yao imekosa fedha hizo muhimu lakini hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa hadi sasa na wao kama viongozi wamejikita zaidi katika utumbuaji wa MAJIPU huku jipu kuu linalosababisha huduma hizo kuwa mbovu katika Mikoa husika likiachwa.
Tumeshuhudia watumishi wa Idara ya Afya wakisimamishwa kazi kwa kudai Rushwa na wengine kwa kujihusisha na uuzaji wa vifaa Tiba kama vile Gloves kwa wagonjwa, sitalizungumzia sana suala la Rushwa kwani lipo wazi sana na ni kosa kubwa kisheria lakini turudi upande wa pili kwa hawa watumishi wanaojihusisha na uuzaji wa vifaa ni wazi inawezekana kabisa kutokana na Serikali kutopeleka vifaa hivyo ndio maana watumishi hao wanatumia mwanya huo kuyafanya hayo tunayoyaona na kuyasikia, tuelewe wazi ugonjwa hauji kwa kupanga muda sasa kama mgonjwa kafika Hospitali saa nane za usiku na hakuna Gloves, Sindano, maji(Drip) au dawa je mgonjwa huyo atakapo agizwa akanunue vifaa hivyo atavipata wapi? Je ataweza kupata huduma sahihi na kwa wakati? Ni wazi hawezi kupata huduma hiyo kwa wakati na yanaweza kutokea madhara makubwa ikiwemo na kifo lakini kwa mwenendo huu wa Viongozi wetu iwapo yatatokea hayo Mtumishi au watumishi hao wataitwa MAJIPU na kutumbuliwa eti kwa uzembe wa kusababisha kifo huku Mzembe Mkuu aliyeshindwa kupeleka vifaa hivyo akiachwa.
Nimalizie kwa kusema naomba viongozi wetu walione hili ili jamii husika katika maeneo tajwa ziweze kupata huduma stahiki za Afya na kupunguza MAJIPU kwani kwa kuendelea kuliacha suala hili ndipo hayo yanayoitwa MAJIPU yanaongezeka na ni wazi haya yanayotumbuliwa ni VIJIPU lakini jipu kuu ni hao walioshindwa kupeleka fedha katika Mikoa hiyo je ni hakina nani hao?.