Mikingamo vs mwanahalisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikingamo vs mwanahalisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jayfour_King, Dec 6, 2009.

 1. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa ukweli na uungwana na ili niwe mkweli (uzushi sio sera yangu) nimepata wazo la ku compose thread hii baada ya kuifuatilia na kuchangia thread ya mdau wangu Paka jimmy ambayo ilikuwa na heading ya "Umekaa kijijini wewe? mie nimekaa" (one of the best thread at its day).

  Kwa kweli baada ya kusoma dondoo za mtoa mada halafu michango ya jamvini (as usual) nimeona nije hivi:
  Hiyo miaka ya tisini nadhani kabla ya 1999(mwaka). Kulipata kuwa na kipindi RTD (Radio Tanzania Dar-es-salaam) ambacho kilikuwa kinaitwa MIKINGAMO.

  Kipindi hiki kama alivyosema mchangiaji mmoja kwenye thread ya JP amekifananisha na ilivyo JF, (big up).

  Ki-muhtasari majukumu ya kipindi hiki yalikuwa kuibua visa na mikasa ya viongozi waliokuwa wanatumia madaraka yao vibaya kama: Kutumia madaraka yao kuajiri ndugu zao,kujiuzia mali ya umma bila kufuata taratibu rejea,kutoa tender kwa upendeleo nk.

  Kwangu mimi leo tofauti ninayoiona kati ya MIKINGAMO (kipindi machachari cha wazalendo enzi hizo) na Mwanahalisi kama (gazeti) ni hivi:

  MIKINGAMO: Kilikuwa ni kipindi ndani ya redio ya taifa ambacho(kilianzishwa na serikali kuu) na kazi yake ilikuwa kuibua mambo yasiyokwenda sawa ki uongozi na utawala kwa juniour staff waliokuwa watumishi wa taasisi za huduma kwa wananchi wakati huo ili ku keep awareness ya serikali kuu kuhusu huduma inazotoa kwa jamii.

  Bahati nzuri kama wakati ni baraka (serikali kuu) wakati huo ilikuwa safi na ilikuwa inafuatilia yaliyokuwa yakiibuliwa. Kuna ushahidi wa watu waliopoteza kazi zao kutokana na uchafu wao, na mambo yalianzia MIKINGAMO.

  Kwa hiyo tofauti ya wakati huo na sasa kwa kiasi kikubwa imelala hapo (doro). Ingawa katika uibuaji huo sio wote walio athirika kutokana na ukweli halisi kwamba, pengine mtandao ulianza kujengwa wakati huo.Kwamba sio kila aliye ripotiwa aliathirika, (wengine walikuwa na ma godfathers wao).

  MWANAHALISI: Inafanya kazi: (kwa kushirikiana na wapendanchi) kuibua ukiukwaji wa matumizi mabaya ya madaraka ya umma.(Tofauti hapa imejengeka katika msingi kwamba, zamani, mikingamo iliibua kesi ndogondogo ambazo zinahusu taasisi zinazotoa huduma kwa jamii wakati serikali kuu angalau ni safi).

  Tatizo tulilonalo kama nchi ni: Na hii ni tafsiri ya wananchi kwamba serikali kuu ndiyo inayohujumu maslahi ya umma kwa kuingia mikataba mibovu isiyo na maslahi kitaifa na sio kwa bahati mbaya ni kwa makusudi.

  Bahati mbaya bila utashi mwema hii (serikali kuu) haina refa na mara nyingi imekuwa ikikanusha ili kujijengea imani kwa wananchi wengi ambao hawana vyanzo vingi vya taarifa (huu ni uhaini).

  TANZANIA TUSIOKUWA TUTOKE VIPI? BINAFSI SINA JIBU NAOMBA TUCHANGIE.
   
Loading...