Mikel Arteta na mchakato wa Arsenal

Mikel Arteta na mchakato wa Arsenal

Joined
Nov 24, 2024
Posts
23
Reaction score
33
Tangu Mikel Arteta achukue nafasi ya ukocha Arsenal mwezi Desemba 2019,Safari imekuwa na hisia Kali kwa mashabiki na wapenda soka kwa ujumla.Kwa upande wa mashabiki wamelazimika kuendana na matokeo ya kushangaza yanayo ikuta timu yao. Lakini mchakato huu imekuwa na vipengele vikuu vinne. 1️⃣KUREJESHA IMANI. Mambo yalianza kubadilka Arsenal baada ya Arteta kujenga kikosi chake hasa akitegemea hasa vijana mfano:Bukayo saka, Gabriel Martinell na wengineo. Na ndoto ya Arsenal ilianza kuonekana kwa vitendo baada ya kutwaa ubingwa wa FA kwa kuifunga Chelsea magoli (2-1) pamoja na kuirudisha timu nafasi 4 za juu kwa uhakika zaidi. 2️⃣Maamuzi ya muda. Mpaka hivi sasa Arteta ana misimu minne na klabu ya Arsenal na ndani ya misimu yote amekuwa akitoa ushindani mkali kwa klabu zinazo wania taji la ligi kuu ya uingereza na si yeye kuiongoza Arsenal kushinda taji hilo.Swali ambalo muda unawauliza Arsenal ni muda gani timu yao itakuwa kwenye mchakato wa kujengwa. Misimu uliopita ulikuawa na mauzauza yakutosha mpaka kupoteza taji la ligi kuu kwa tofauti ya alama moja. 3️⃣Mtazamo wa tofauti. Baada ya drama za 2023/24 kuisha Arteta ni miongoni mwa walimu walio kuwa wakitizamwa kwa jicho la tofauti na wapenda soka wengi.Lakini Arsenal wamewasilisha kitu ambacho hakikudhaniwa kabisa. 4️⃣Taswira mpya. Arsenal inaanza kutengeneza taswira mpya ya kwamba ni timu inayo toa changamoto kwa mabingwa na si kutwaa ubingwa.
 
BUBU KASHANUNUA SIMU,WAMESHINDA NDIO HATA HIVYO MADRID WAPO HARIJOJO SANA KIPINDI HIKI.
 
Mimi shabiki wa Chelsea hata sijamuelewa kabisa yule kocha wetu Maresca, pamoja na wamiliki wa sasa wa hiyo timu kwa kuigeuza kuwa timu ya watoto.
Kwangu mimi naona ni upuuzi wa hali juu sana kwa timu kuwa long term plans pekee, pasipo kuwa pia na short term plans!
 
Back
Top Bottom