Mikataba ya Makatibu wa Kuu na Manaibu wakuu.

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
WanaJamii HERI YA MWAKA MPYA,

Kama kichwa hapo juu,nimeona tuangalie hili swala la makatibu wakuu na manaibu wakuu kula kiapo juu ya kiapo,kinachoitwa kiapo cha maadili.Binafsi sijaona maana yake ikiwa bado mfumo ndio wa kurekebisha na sio watu kazi na kuogopeshana.
Nakubaliana na raisi kuhusu kurekebisha sheria na sera ya manunuzi,hii sheria imelitia taifa hasara mno.(sawa).
Kingine,kama raisi magufuli anataka mabadiliko ya kweli,basi awashirikishe vyama upinzania katika hili maana pia wao wanaweza kumsaidia;lengo ni Tanzania mpya na sio uchama na ukanda.Raisi magufuli aachane mambo ya kuangliana uso na ukanda nk.Hawa watu walishafanya kazi,imetosha basi wapewe wengine kwani ndio waliosoma tu??double standards kama hizi huku tukitaka kusafisha nchi ni sawa na kutunga uwongo wa kujidanganya mwenywe.

Kumpa Maswi ukaimu kamishna TRA ni tusi kubwa sana kwa Bunge.Sisi watanzania tumwelewe vipi ni yake ya kweli kwa Tanzania.Kwahiyo Maswi naye ataapa kulinda maslahi ya nchi tena wakati alishakuwa na dosari?bila kumsahau Muhongo.Maadili hapa yako wapi ya utumishi wa umma?

Kusema ukweli,nathani nchi nzima inahitaji overhauling kwenye sheria na kuheshimu mihimili ya sheria maana hata raisi hayuko juu ya sheria na taratibu zake.
MwanaJamii ningependa tuone nilipi maoni yako juu ya kiapo cha maadili na wapi unadhani serikali ibadilishe mwelekeo kuleta matokeo haraka Zaidi?

Tanzania ina wasomi wengi sana nje na ndani ya nchi ambao wanauwezo kuliko hawa wanaolindwa na system na kubebwa kama mitume.This is non sense from our president.Nimeshaona kufell kwa magufuli asubuhi mapema kama ilivyokuwa kwa kikwete.Wanyonge na wasiokuwa na network ndio watakoma kama kawaida.

Tuijenge Tanzania sote bila kujali kabila,dini au kujuana na kwa kutumia akili na maarifa.
 
Last edited:
Ingekuwa vyema ukaweka viapo vyote hapa jamvini ili wadau waone contents zake.
 
ile katiba waliyoibaka ilikua na majibu yote kwa bahati mbaya sisi tuliipenda katiba mpya lakini ccm na six wakaipenda zaidi ndo hivyo tena imekua mwendo wa kuungaunga tu
 
Mambo yote waliyoyakataa ccm kwenye katiba Mpya yameonekana ndiyo njia bora ya kushughurikia watendaji wazembe na kudhibiti ufujaji wa Pesa za wananchi.

Jpm anatakiwa kuwaonyesha watanzania kwamba anachukia ubadhirifu kwa kutuachia katiba ya warioba.
 
Kama JPM ana nia ya dhati ya kuwapa watanzania katiba mpya asijishgughulishe na katiba mpya mpaka baada ya 2017 atakapopata uenyekiti wa chama. Otherwise, ccm maslahi watamchakachua tu
 
Kama JPM ana nia ya dhati ya kuwapa watanzania katiba mpya asijishgughulishe na katiba mpya mpaka baada ya 2017 atakapopata uenyekiti wa chama. Otherwise, ccm maslahi watamchakachua tu

ccm ni jipu moja kubwa sana mkuu.Tena la kwenye kikwapa.aibu!!
 
Back
Top Bottom