IHANGILO
Member
- Jun 23, 2013
- 55
- 10
Wana JF......
Kumekuwa na hali ya majibizano malumbambo kutupiana lawama ni nani alieruhusu kupitishwa tozo ya simu, je! hawakujua kuwa ni mzigo kwa wananchi, kauli nyingi zimesikika na viongozi wa kubwa wa serikali wakitoa kauli aidha za kukinzana wao kwa wao na kupongezana. Hivyo kupelekea kuamsha hasira na hisia, na mitazamo tofauti kuhusu tozo hiyo.
Hivi karibuni waziri mkuu Mh Pinda alikaliliwa na vyombo vya habari akisema wanao pinga tozo ya simu hawaitakii mema nchi yetu, na naibu waziri teknologia na mawasiliano Mh Januari Makamba alikaliliwa na vyombo vya habari akisema wao hawakuruhusu tozo hii na juzi raisi Kikwete katoa wito wa wahusika kukaa chini na kuzungumza kuhusu tozo hii.
Kwa nini serikali imeamua kuibua swala hili na kulishadidia kwa nguvu zote? hiki ndicho kilicho nisukuma na kuanza kutafuta kulikoni na kuna nini ambacho watanzania wengi wanapumbazwa na kusahaulishwa kwa sasa kwa kupitia mijadala ya tozo ya simu.
Kwa sasa Watanzania wako katika michakato ya kujadili rasimu ya katiba mpya ambayo ni dira ya taifa kwa miaka ijayo, ikumbukwe wakati tume ya katiba mpya ilipo tangaza rasimu ya katiba tarehe 4/6/2013 baada ya kukusanya maoni ya watanzania, vyama vya siasa na taasisi mbalimbali na watu binafsi zilitoa maoni na mitazamo mbalimbali juu ya rasimu hiyo.
Vyama vya siasa vilipewa kipaumbele sana katika kutoa mitazamo na michanganuo tofautitofauti.
Chama cha mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chama tawala hapa nchini kilikuja na kauli za kutofautiana na mambo kadhaa yaliomo ndani ya rasimu ya katiba mpya punde baada ya kutangazwa rasimu na balaza la katba.
Wanasiasa kutoka vyama mbalimbali hususan wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walikwishakaririwa wakieleza kutokubaliana nayo kwa madai kuwa haiendani na mfumo wa siasa za kileo na kwamba imelenga kuongeza mzigo wa uendeshaji wa Serikali
Rasimu ya katiba mpya ilionekana kuitesa sana CCM kwa kuhofia ndo mwiba kwao, na chama hicho kilionekana kuwa na mikakati ya dhadi kupinga mambo hayo ndani ya rasimu ya katiba mpya, ikapelekea kamati kuu yaani CC kukutana mjini DODOMA na kuazimia kuandika WARAKA WA SIRI kwa wananchama wao.
Ikumbukwe wakati kamati kuu ikikutana bunge la jamuhuri lilikuwa linaendelea na kujadili bajeti kuu ya serikali na ndani ya bunge kuna viongozi na wabunge wa chama cha mapinduzi, baada ya bunge kuahirishwa walikutana wabunge wote na viongozi wa chama cha mapinduzi, ndipo walaka wa siri ulipo gawiwa kwa wabunge na kuamrishwa kwenda kuwaeleza wanachama wao majimboni.
Nirudi kwenye dhumuni hasa la makala hii baada ya kukumbuka mchakato ulivyo anza wa kufifisha mawazo ya watanzania ndani ya asimu ya katiba mpya, ikumbukwe serikali ya CCM iliopo madarakani inampango wa kuendelea kushika hatamu ya uongozi ndani ya taifa hili lazima itatumia nguvu zote kuficha hoja kama sio kuzizika kabisa pale inapo onekana zinakwenda kinyume na matakwa yao.
Tujikumbushe matukio yalio kuwa yakiibuliwa na serikali kuficha uovu punde wakibainika.
Kashfa ya aliekuwa waziri wa maliasili na utalii Maige alikumbwa na kashfa alijitetea namna wizi huo ulivyofanyika na akaahidi kulifanyia kazi. Maige alipumua kwani kashfa nyingine kubwa ikaibuliwa nayo ni ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo, kukusanya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhonga wabunge na kutafuna wakati wa kupitishwa bajeti yao.
Katika namna ya kushangaza kikaibuka Kikombe cha Babu wa Loliondo kikafunika. Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile Babu akavuma haraka kwamba ana tiba ya magonjwa sugu.
Serikali ikahamia Loliondo kupata kikombe. Kina William Lukuvi, Maige, Terezya Huvisa walitinga Loliondo pamoja na Dk. John Magufuli aliyeahidi kujenga barabara chapuchapu ambayo haikuwa kwenye mipango ya serikali.
Wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi walijaza mafuta kwenda kunywa kikombe kutibu magonjwa waliyoyajua. Wananchi wakafurika, wakati serikari na mawaziri wake wamekumbwa na kashfa ya ufisadi mkubwa ndani ya nchi.
kikombe cha babu kilifunika matukio makubwa kiasi kwamba hata ripoti ya ufisadi wa Jairo iliyowasilishwa na Kamati ya Bunge chini ya Injinia, Ramo Makani, haikuwa na mashiko kwenye vyombo vya habari.
Habari za Jairo na utoroshwaji wanyama ziligusiwa tu mwaka 2012 lakini iliibuka kashfa nzito pale Muhimbili ikamngoa Katibu Mkuu wa Afya, Blandina Nyoni, haya nimatukio ambayo hayakuka katika kumbukumbu za watanzania wengi sababu serikali imekuwa ikihakikisha inazusha matukio ili funika kombe mwanaharamu apite.
Kwa mara nyingine serikali hiyohiyo yenye matukio ya funika kombe mwanaharamu apite imejitokeza tena muda huu wakati masikio ma fikra za watanzania wengi zikielekezewa katika kujadili rasimu ya katiba mpya.
Serikali kwa makusudi imekuwa bunifu sana na sasa imetuletea mjadala wa tozo ya simu maarufu #simcad tax, na kwa kiasi kikubwa viongozi wa juu waserikali kwa makusudi na muda tofauti wamekuwa wakitoa matamshi hata kwa kutofautiana wao na kuwaacha watanzania na maswali kama serikali hii inafanya kazi kwa pamoja na kama serikali hii inasauti ta pamoja.
Tusifikiri serikali haijui ugumu wa maisha wa watanzania na sio kweli kwamba pesa zitakazo kusanywa ni kwajili ya umeme vijijini bajeti ya nishati na madini ilipo somwa, miradi hiyo imezaminiwa na mashirika ya nje, vivyo hivyo kwa sekta ya maji.
Sikweli kwamba viongozi hawa hawafahamu wanacho kizungumza na sio kweli kwamba wanatofautianaa kauli za viongozi hawa ziko sahihi na wanafahamu ni nini wanacho kifanya ili akili za watanzania na media zihamishie mitazamo huko,kipindi hiki mijadala ya mabaraza ya katiba inaendelea huko.
Tumesikia tume ya jaji Warioba ikikutana na viongozi wa chama cha mapinduzi walipenyezwa ndani ya mabalaza ya yakatiba wakisoma waraka ulio andaliwa na ccm na sio maoni ya wanannchi, na hata baadhi ya maeneo tume hiyo imejikuta ikikataliwa na wajumbe wa mabaraza hayo kwa kiasi kikubwa ni wana ccm punde inapo wazuia kutumia waraka huo wa CCM.
Sio rahisi wananchi kuyangamua haya pasi kuwa na watu wa kuwakumbusha malengo na mwelekeo wataifa lao, tunaweza kukaa katika wimbi hili hadi watakapo hakikisha malengo yao yametimizwa, tiamaji tiamaji katiba imetoka na kuanza kujilaumu sisi wenyewe.
Nihitimishe kwa kuwataka Watanzania kutazama zaidai suala lakatiba ambalo kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukilipigia kerere ilitutengeneze taifa la watu wenye sauti katika nchi yao na sio watu wachache makaburu wenye kutaka kujineemesha wenyewe na familia zao.