Mijadala gani hufungwa au kufutwa kabisa katika JamiiForums?

Status
Not open for further replies.
WanaJF naombeni msaada kwayeyote anayejua nanmna ya kufanya na kujiunga na CCP nipitie hatua zipi nina cheti cha kidato cha nne na kidato cha sita pia nina cheti cha JKT Na nina umri wa miaka 22 na pia ufaulu wangu ni mzuri naombeni kwayeyote anayejua namba zangu ni 0766103399
 
Baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kuupindisha ukweli ndani ya JF na kuanza kuwafanya watumiaji wa JF kudhani kuwa aidha wanaonewa au kuna jambo nyuma ya pazia. Ni wakati muafaka wa kuwafahamisha watumiaji wa JF (wanachama na wasio wanachama) nini hufanywa na moderators na kwa misingi ipi.

Kwanza tuziangalie kanuni/sheria za JF ambazo ndizo hutumika kuwahukumu watumiaji wote (si nje ya hapo!). Mara nyingi tumekuwa tukiwasisitiza wanachama (members) kuwa ni vema wakazisoma sheria hizi kabla ya kuanza kuitumia JF ili hatua flani zinapochukuliwa zisionekane kuwa zimewakandamiza, ni wajibu wetu kama watumiaji wa JF kuanza kuangalia sheria hizi na kupendekeza wapi pafanyike marekebisho na kivipi.

=============
SHERIA NA KANUNI ZA JAMII FORUMS

Tafadhali jiepushe na mambo yafuatayo:

Wadau wengi wamekuwa wakiivunja kanuni hii ambayo tulikubaliana tangu 2006; haturuhusu kwa namna yoyote iwayo kuvunjiana heshima kwa makusudi wala matusi kwa namna yoyote iwayo. Mfano: Kuandika neno fvck kwa nia ya kukwepa censorship ni kutukana kwa kudhamiria kabisa, tumelishtukia hili na mara inapobainika hoja husika huondolewa na mhusika kufahamishwa juu ya kosa lake, anapothibitika kuendelea kukaidi basi hufungiwa kwa muda au kufutiwa uanachama kabisa!
Hili nalo pia husababisha hoja za watu kufungwa, kufutwa au mhusika kupewa onyo.

Nadhani maelezo yaliyo juu yanajieleza wazi, natamani wengi wangeelewa maana ya maneno hayo juu! JF si sehemu ya kuanzisha uchochezi aidha wa kidini, kisiasa n.k.

Endapo itabainika umeanzisha hoja kwa nia ya kuibua uchochezi au ugomvi na mtu basi tunasikitika hoja hiyo itakufa HARAKA SANA.
Kuna wadau walikuwa na kawaida ya kuwasiliana na wenzao kwa mapenzi yao wenyewe au hata bila wao kuhitaji, namna pekee ya kuwasilisha PM au email ambayo unaona inaleta tatizo kwako si kuibwaga katika hadhara bali kuituma kwetu na sisi tukaifanyia uchunguzi na kubaini ubovu wa PM wenyewe au Email husika ili mhusika achukuliwe hatua za kinidhamu. Tunalichukulia suala la PM na Emails kuwa private, kulileta hadharani ni kutafuta magomvi na kudhalilishana.

Kwa bahati hili halijatokea sana JF, threads ambazo zinakuwa zinaonekana kuwa na links ambazo si salama huwa zinaondolewa haraka, aidha waanzishaji wa hoja husika hufahamishwa lakini wakionekana kukaidi hatuna sababu za kuendelea kuwasiliana nao badala ya kuwafungia kwa muda (kutokana na kukaidi) na kisha kuanza kuwa-monitor kadiri siku zinavyokwenda.
Wahusika mnaovunja sheria hii mnajua athari yake; tunaweza kuwa tunachukizwa na kitu flani kilichofanywa na kiongozi au mtu flani ndani ya serikali au kidini, kuanzisha shutma ambazo zinalenga kumchafua mtu bila kuwa na ushahidi wa kutosha ni kutaka kumchafulia jina mhusika.

JF si sehemu ya kuchafuliana majina, hatua za kinidhamu huchukuliwa kwa wale wenye nia ya kuitumia JF kwa maslahi yao binafsi.

JF haitatumika kama 'attacking tool' kwa wale ambao aidha wamesimamishwa kazi sehemu, wamekosa nafasi flani za kikazi katika taasisi/idara/wizara/makampuni n.k, wamechokana/achana au shindwa elewana kwenye ndoa/mahusiano, wameshindwa kuelewana katika biashara na mengineyo ya mwelekeo huu; tukibaini kuwa unajaribu kuitumia JF kwa malengo haya, tunasikitika tutaiondoa.
Tunaheshimu SANA hoja za kila mmoja, kuna wadau walikuwa wanadhani huenda wao si mali kitu hapa JF, tunatambua kuwa Mwenyezi Mungu katujalia karama tofauti, lakini wakati huohuo tunaamini kila mmoja anaweza kubadilika kadiri siku zinavyokwenda. Hakuna mwanachama wetu ambaye tunamwona "mbabe" dhidi ya wenzake, wote ni sawa mbele zetu na tunawapa heshima sawa.
Hii si sheria bali ni angalizo tu.

==========================

Other Rules to be noted:

Nadhani nimeigusia hii hapo juu, lakini ni msisitizo zaidi.


Maelezo ya hapo juu hasa yenye rangi nyekundu hupelekea posts nyingi kuondoshwa na pengine wahusika KUFUNGIWA kwa muda!
Niliyoiwekea rangi nyekundu mkuu MS aliianza, mdau mwingine (Shy) naye amekuwa akiweka links kibao kwenye post zake, sharing is caring... Lakini sharing inapofanyika hapa JF ni vema kuweka content husika kisha utoe CREDIT kwa chanzo cha habari, haipendezi kubwaga habari JF bila kuweka chanzo (credit) cha habari. Japo kuna vyombo huchukua habari zetu hapa bila kutu-credit lakini sisi bado tunasisitiza wanachama wetu kuona umuhimu wa kuthamini vyanzo vya habari zetu.
Hili tulilisisitiza kuwa endapo litawatokea wanachama basi wawasiliane nasi haraka. Wanaoonekana kutuma malalamiko ni wachache na hatua huchukuliwa.
Inajieleza


Mpaka sasa hatujapokea malalamiko ya kuvunjwa kwa sheria hii lakini ipo
Wengi wamekuwa wakiivunja hii makusudi kabisa; wanaanzisha salaam ndani ya topic na mods huchukua hatua za kuondoa kila post yenye kuwa nje ya hoja au wanapoona topic imejaa majibizano yasiyo na tija kwa jamii basi topic nzima hufungwa au kuondolewa kabisa. Aidha, kuanzisha mjadala wa kidini sehemu ya siasa wakati kuna jukwaa la dini ni kukosea, mods huhamisha mjadala husika kwenda jukwaa husika wakiwa wameacha redirection na ukibonyeza title ya topic husika utajikuta unaendelea kuisoma katika location mpya.

Ieleweke kuwa kila post ambayo inaondolewa kwenye public domain ipo; zinabaki kwa ushahidi siku za usoni maana wengine hukana kuwa walifanya makosa wanayoambiwa walifanya; hatufuti MOJA KWA MOJA, zinawekwa sehemu kwa ajili ya reference za makosa ya wanachama wetu.
Inajieleza wazi tu. "Member flani" kuna kipindi alikosea kulingana na mojawapo ya sheria lakini alipogundua aka-submit unban request nasi tukawasiliana na yule ambaye walikuwa wamekoseana na wakakubaliana kuwa yameisha na akafunguliwa. Tunatambua kuwa wote huwa tunajikuta tumepandwa na jazba na wakati mwingine kutoa kauli ambazo si za kiungwana, uungwana ni vitendo, ukigundua umekosea ukaomba radhi basi utasamehewa!
Inajieleza
Signatures za watu wengine huwa ndefu SANA, au zina maneno yasiyo na heshima kabisa. Huwa tunaziondoa na kumfahamisha mhusika, akionekana kuwa mbishi basi ananyimwa access ya kuwa na signature. Hii pia hujitokeza kwa avatars.
Inarejea kulekule, kuwa ni vema unapochukua content kokote haijalishi ni copyrighted au sio copyrighted, basi toa credit ya chanzo cha habari usiibwage as if ni wewe umeandaa hoja husika.
Hizo juu zinajieleza; ingawa nyingine ni kama zinajirudia

Na hii ndo huwapa mods kazi ngumu, wanajaribu kuzipitia threads kuangalia kama zinastahili kubakia katika public domain au zinavunja yale niliyoonyesha kwa rangi nyekundu hapo juu.... Inakuwa ni mtihani lakini kwa ushirikiano wa members wanaojali basi huzifanyia kazi accordingly.

IELEWEKE KUWA:

JF kamwe haitamsimamia au kumpendelea mtu kwa sababu ya DINI yake au ITIKADI YA KISIASA aliyokuwa nayo.

Tutaendelea kutoa uhuru, hatuwezi kumfungia mtu kwakuwa hupendi anavyopingana na mtizamo wako wa kisiasa au kidini; kama huwezi kujizibizana naye kaa mbali naye.

Hatutamwonea huruma yeyote anayeonekana kutaka kuvunja sheria kwa kisingizio chochote kile; endapo unaona kuna mtu kaenda kombo na sheria hizi usisite kuwasiliana nasi, unaweza kubonyeza CONTACT US au hata kutumia barua pepe kwenda support@jamiiforums.com ili hatua za haraka zichukuliwe.

Malalamiko ya baadhi ya comments au topics kuachwa bila kutoa ushirikiano kwa kuziripoti hoja zenyewe via REPORT Button yanatarajiwa japo tunaamini tumeweka button wazi kwa kila mtumiaji.

Naamini nimeyajibu maswali ya baadhi ya watu.
Point hizi kanuni nmezipendaa maana wanyonge tunao tolewa matusi na kashifaa mpka tunaogopa kupost sasa bora nmeiona hii!
 
Mimi nauliza, nikitaka kuedit taarifa zangu kwenye profile yangu Nifanyeje?
Nimejaribu nimeshindwa.
 
Naomba kuungwe kwenye kundi la Dini

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom