Mihemuko ya Trump yamweka pabaya kuhusu kususiwa kwa Qatar, kesi ya Urusi, makubaliano ya Paris

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,415
22,026
Onyo alilokuwa akitoa Obama juu ya Trump kuwa hana sifa za mtu makini wa kuwa Raisi wa Marekani zimeanza kujionyesha wazi. Wamarekani wameanza kuona kuwa na Trump White House ni tatizo kubwa sana kwa nchi yao.

Kubwa la wiki hii ni kile ambacho Trump, anayejifanya kuwa hodari wa kutambua "fake news" amejikuta akijisifia kwamba yeye ndiye aliyesababisha Qatar isusiwe na nchi za kiarabu baada ya ziara zake huko Uarabuni. Sasa imegundulika kwamba ususiaji wa Qatar umetokana na "fake news" ambazo zilipandwa na hackers wa Urusi ili kuzigombanisha nchi za Kiarabu zenye uhusiano mzuri na hata kuwa na vituo vya kijeshi na Marekani.

Warusi walipandikiza fake news inayoonyesha Raisi wa Qatar akitoa matamko ya kuunga mkono vikundi vya kigaidi na kuisifia sana Iran, huku akionyesha mataifa yaliyoisusia Qatar kuwa mabaya. Taarifa hii ilikuwa kisababishi kikubwa kwa mataifa haya kuisusia Qatar - lakini FBI ya Markani ilituma wapelelezi Doha, Qatar waliogundua kwamba taarifa hii ilikuwa fake news toka Urusi.

Sasa Trump amejikuta mahali pabaya kwa kujisifia kwamba ziara yake ndio imesababisha Qatar isusiwe, kumbe ni fake news toka Urusi. Na mbaya zaidi ni kwamba, Trump anazipongeza nchi zilizoisusia Qatar huku akisahau kwamba Qatar ina uhusiano wa karibu na Marekani pamoja na kituo cha kijeshi cha Marekani chenye askari zaidi ya 11,000, kituo ambacho ni muhimu sana kwa Marekani kwa kampeni za Syria, Afghanistan nk.

Wamarekani wanajiuliuliza hivi Trump anafikiri kabla hajaongea kwenye tweet? Kwa hili Trump anaonekana amerikoroga sana! Kwa kifupi, Urusi inatumia fake news kuwavuruga rafiki wa Marekani. FBI ndio wanagundua ni fake news imesababisha Qatar kususiwa. Trump anajisifia ni yeye kasababisha Qatar isusiwe na bila kuzingatia Qatar ina kituo cha kijeshi cha muhimu sana kwa Marekani na NATO.

Si hayo tu. Trump pia anakabiliwa na tatizo kubwa pale White House. Amekuwa akigombana na watendaji wake na kuwashutumu pale ambapo wanaonekana kuweka maslahi ya taifa mbele kuliko ya Trump. Wengi sasa wamekuwa na nia ya kujiuzuru. Hii ni kutia ndani Mwanasheria Mkuu (AG) ambaye juzi alisikika akifokana kwa sauti ya juu na Trump pale White House. Kubwa linalomkabili ni hili la uhusiano na Urusi wakati wa kampeni, ambapo sasa inaonekana wazi alikuwa akitoa maagizo wasifuatilie upelelezi wake, kitu ambacho Mwanasheria Mkuu, pamoja na kumuunga sana mkono Trump, hakubaliani nacho.

Mkuu wa FBI aliefukuzwa kazi na Trump anatarajiwa kutoa ushahidi kwenye kamati ya senate ambao unaweza kumweka Trump pabaya.

Zaidi ya haya, kwa ujumla kumekuwa na hisia kwamba Trump pia ni kama ana hasira, kisasi na ushindani(obsession and inferiority complex) dhidi ya Obama, anataka aonekane bora kuliko Obama na hivyo kuwa na nia ya kubadili chochote alichoanzisha Obama, hata kama ni kizuri, na kupata shida sana kuja na mpango mbadala. Kubwa pia ni kujitoa katika makubaliano ya Paris, ambayo yanasemekana ni ya kujitolea (voluntary actions). Amekuwa akiulizwa, ikiwa Marekani iliingia makubaliano ambayo Marekani yenyewe ndio inaamua nini itafanya, na bado unayaona kuwa "bad deal", wewe unataka makubaliano gani yaliyo bora kuliko Marekani yenyewe kuamua nini itafanya? (Sawa na mtu kukubali wafanye pledge za mchango wa harusi kisha kusema mpango wa ku pledge michango ni mbaya kwake!)

Kuna watu maarufu nchini Marekani wameanza kusema yale yanayomkabili Trump ni makubwa na mabaya zaidi ya Watergate scandal iliyomwondoa Raisi Richard Nixon wa Marekani madarakani miaka ya 70. Raisi Nixon aliondolewa baada ya kugundulika alijaribu kuzima upelelezi dhidi yake pamoja na matumizi mengine mabaya ya madaraka akiwa raisi.

Mambo yaananza kujionyesha wazi kuwa Trump anaanza kuzidiwa na moshi wa jikoni pale White House, mambo yanamwendea mrama sana.

Watu wanajiuliza Trump atadumu kwa muda gani White House? Na akiweza kudumu, ni mangapi atayavuruga?

Ni tatizo kubwa pale inapotokea akili ndogo kuwa na mamlaka makubwa, katika nchi yeyote ile.
 
Tatizo mnajifanya mnajua kuliko Waliomchagua
Kasumba alizokataza Nyerere miaka ya 47. Bado unaona wazungu wana akili ya maisha ya kila siku kuliko wewe, hivyo lolote analofanya mzungu lazima ni sawa sie hatulielewi? Ndio maana mnaibiwa mchanga wa madini kirahisi kama kumsukuma mlevi, kazi kukimbilia kusaini mikataba kwa kuwa mmewekwa kwenye hoteli nzuri yenye kafriji ka vinywaji. Wake up black man.
 
Labda kama haumfahamu Trump....

Trump ni wakipekee

Ndiyomana hadi Leo anadunda

Na hakuna jipya

Hayo maboko hajaanza kuyatoa leo
Mkuu huwajui Marekani. Wao sheria ni sheria, sio kama hapa kwetu jambo kuu kwa kila waziri au kiongozi ni kujipendekeza kwa raisi. Richard Nixon aliondolewa uraisi wa Marekani kwa sababu hizi hizi kama zinazomkabili Trump. Unaona kwamba Trump anageukwa hata na wafuasi wa chama chake pamoja na waliomsaidia kampeni kwa kuwa wanataka kusimamia sheria na haki? Marekani sio Tanzania, kule viongozi wanaona nchi ni kubwa kuliko raisi au chama. Hakuna raisi nusu mungu kama hapa kwetu.
 
mwenye anajua story ya uyo raisi RICHARD NIXON aliyeondolewa ilikuwaje anipe kidogo tumuondoe uyu wa kwetu
 
mwenye anajua story ya uyo raisi RICHARD NIXON aliyeondolewa ilikuwaje anipe kidogo tumuondoe uyu wa kwetu
Kwa kifupi Richard Nixon alikuwa raisi wa Marekani wa chama cha Repblicans kama Trump. Sasa kutokana na ushindani na Democrats, Richard Nixon alihusishwa na kuvunjwa ofisi za chama cha Democrats ili kupata documents fulani katika hizo ofisi zilizokuwa katika jengo la Watergate - kwa mfano Raisi Magufuli atumie vyombo vya usalama kama TISS kuvunja ofisi za Chadema ili kuiba document za siri.

Sasa katika kufanya upelelezi juu ya uvunjaji wa ofisi za Democrats, Richard Nixon akiwa na madaraka ya uraisi akawa anatumia madaraka yake kujaribu kudhoofisha upelelezi. Pamoja na hayo matokeo ya uchunguzi yakaonyesha pia Richard Nixon alikuwa akitumia madaraka yake vibaya katika mambo kadhaa pamoja na kuwatumia FBI kupeleleza watu waliokuwa wakipinga sera zake (kama vile Magufuli atumie TISS au Polisi kufuatilia wasiokubaliana au wanaomkosoa katika mitandao ya jamii), sio hilo la kuvunja ofisi za Democrats peke yake. Hivyo akawa impeached na kulazimika kujiuzuru - ndio maana wanasema hali ya sasa ya Trump inalingana na ile iliyomtoa Nixon madarakani, na wengine wanasema ni mbaya hata zaidi ya Nixon.
 
Kwenye ule mkutano hao waarabu walimtaja Qatar kama mhusika wa hicho kitu
Trump hawezi Risk Military base yake pale Qatar kisa tu ana side na Saudi
Vyovyote vile lazima huyo Emir wa Qatar akubaliane na Matakwa ya kina Saudi
 
Mkuu huwajui Marekani. Wao sheria ni sheria, sio kama hapa kwetu jambo kuu kwa kila waziri au kiongozi ni kujipendekeza kwa raisi. Richard Nixon aliondolewa uraisi wa Marekani kwa sababu hizi hizi kama zinazomkabili Trump. Unaona kwamba Trump anageukwa hata na wafuasi wa chama chake pamoja na waliomsaidia kampeni kwa kuwa wanataka kusimamia sheria na haki? Marekani sio Tanzania, kule viongozi wanaona nchi ni kubwa kuliko raisi au chama. Hakuna raisi nusu mungu kama hapa kwetu.
Tueendelee kusubiri
Ila nakuhaakikishia Trump hawezi kuzamishwa kizembe na siasa za Washington.
 
Tueendelee kusubiri
Ila nakuhaakikishia Trump hawezi kuzamishwa kizembe na siasa za Washington.

Mkuu huoni kwamba hata hivi sasa yuko kwenye nyanja za kuweza kuwa impeached na issue ya Urusi?
 
Mkuu huwajui Marekani. Wao sheria ni sheria, sio kama hapa kwetu jambo kuu kwa kila waziri au kiongozi ni kujipendekeza kwa raisi. Richard Nixon aliondolewa uraisi wa Marekani kwa sababu hizi hizi kama zinazomkabili Trump. Unaona kwamba Trump anageukwa hata na wafuasi wa chama chake pamoja na waliomsaidia kampeni kwa kuwa wanataka kusimamia sheria na haki? Marekani sio Tanzania, kule viongozi wanaona nchi ni kubwa kuliko raisi au chama. Hakuna raisi nusu mungu kama hapa kwetu.

Mkuu hivi Obama bado yupo? Ulipomuandika ilinichukua sekundi kadhaa kumkumbuka maana kapotezwa kabisa, yaani hata Mimi nakubaliana na maneno yako, kwa kweli huyu Trump si mtu wa kawaida inabidi mbinu za ziada zitumike kumdhibiti. Kila ukimuibulia jambo yeye anazidi kwenda juu. Watu wanamtengenezea kashfa kumbe yeye anazigeuza kuwa ngazi za kupanda kwenda juu zaidi.
 
Kwenye ule mkutano hao waarabu walimtaja Qatar kama mhusika wa hicho kitu
Trump hawezi Risk Military base yake pale Qatar kisa tu ana side na Saudi
Vyovyote vile lazima huyo Emir wa Qatar akubaliane na Matakwa ya kina Saudi
matakwa ya kijinga hakuna nchi itakubali
 
Back
Top Bottom