Migogoro ya Ardhi yaibuka tena Loliondo

kalambas

Member
May 12, 2014
22
0
Huu ni mgogoro wa ardhi baina ya vijiji viwili vinavyopakana kijiji cha Arash kata ya Arash na kijiji cha pilaya kata ys malambo. Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba wananchi wa vijiji husika waliingia kwenye migogoro hiyo siku mbili zilizopita.

Wanakijiji wa piyaya kwa msafara mkubwa zaidi ya magari mawili wakiwamo viongozi wa mila viongozi wa kijiji na viongozi wa mila Laogwanak na polisi walifika na kuhamisha ngombe katika eneo la olembuya mpakani mwa hifadhi ya wanyama ya Serengeti kwa madai kuwa hawataki kuona mifugo ys vijiji vya jirani katika eneo hilo.

Wananchi wa kijiji cha Arash kitongoji kinachopakana na Piyaya walifika kwa wingi wakitaka kujua suala hilo la kuhamishwa ngombe katika eneo hilo ambayao kwao pia walijua ni sehemu ya kitongoji chao. Lakini la kushangaza baada ya muda viongozi wa pande zote walipofika kwa mazungumzo na kutafuta suluhishi viongozi hao walishindwa kutokana na,kwamba upande wa Piyaya wao walidai kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni sehemu ya kijiji cha Arash lakini Mwenyekiti wa kijiji cha Arash Kiaro Orminis kwa miaka ya nyuma alifanya mazungumzo nao na kuwauzia sehemu hiyo ya kijiji jambo ambalo liliibuwa tafrani kubwa kwa wananchi wa kijiji cha Arash ambao ndoo wamiliki halala wa sehemu hiyo iliyimegewa ktk kijiji cha piyaya.

Bado suala hilo ni tata na mwafaka bado haukufikiwa.
 

kalambas

Member
May 12, 2014
22
0
Si swala la viongozi pekee ila jamiiisikubali kufarakanishwa kwa maslahi ya viongozi wanaolenga kutafuta umaharufu usio rafiki na maendeleo ya wananchi.
 

Meru Moja

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
256
170
Huyu huyu jana alikuja hapa akidai kuwa kuna bwana anataka ubunge,akampa sifa mbaya mbaya.

Nimepita Piyaya jana nikiwa na wageni,sijaona kitu kama hicho.

Mleta mada ni mchochezi wa kisiasa.
 

kalambas

Member
May 12, 2014
22
0
Meru moja unaelekea unataarifa za uhakiki kuhusiana na jambo husika tunaomba taarufa kamili, n@ kama umesom@ taarifa niliyoandika nimeleta jinsi tasrifa ilivyonifikia na wala sijui kilianzia na kilipoishia. Sijui pia unamaanisha nini kusema nataka kuwachingsnisha viongozi wepe, swala ni kwamba eneo hilo si la viongozi ni la jamii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom