Migogoro katika ndoa inavyoathiri watoto

Migogoro katika ndoa inavyoathiri watoto

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,234
Ndoa ni tendo na ni taasisi takatifu

Ndoa inahitaji kuvumiliana,kuheshimiana na kuthaminiana

Ndoa nyingi siku hizi zinakumbwa na migogoro isiyoisha.Baadhi ya ndoa wanandoa wakionekana kwa nje utadhani wanayo furaha katika ndoa zao.Lakini wakiingia katika mapaa ya nyumba zao hapakaliki.

Wengine ndoa kimsingi zimeshavunjika ila basi tu wanaendelea kulazimika kuishi katika paa moja

Ndoa zingine uvumilivu umekuwa na ukomo...Zimevunjika....baba na mama wametengana...hawapo pamoja tena.

Ni mateso makubwa sana kwa watoto.Kukosa malezi ya baba na mama....ni maumivu makubwa sana ya kisaikolojia yanayowapata watoto kutokana na hili.

Watoto wanaathiriwa na kuvunjika kwa ndoa ya wazazi wao.Kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba hata hao watoto wakikua hawataweza kumudu ndoa zao...Zitavunjika pia.

Binafsi nimeshuhudia maisha ya ndoa yenye matatizo ambayo hatimaye wazazi walitengana....kama mtoto kuna kitu kinakosekana sana...huwa sijisikii kama niko contained...naona kama nina kasoro ingawa nimekuwa mkubwa na naendesha maisha yangu.

Mbaya zaidi ninajiona kama sitaweza kuwa na uvumilivu wa kutosha kwa mwenza wangu pale nitakapompata...Naogopa kurudia kosa hilo hilo la wazazi...lakini sijui ntafanyaje...naona kama ni kitu kilichojengeka ndani......

Ndoa nyingi zina matatizo....hakuna amani....sijui nini kifanyike kuwaokoa watoto kutkana na matatizo wanayoyapata
 
Hii ni mada tete sana!!Hivi kuna umuhimu wa wazazi kuwa pamoja angali hawana maelewano?wanagombana,wanatusiana hata kupigana mbele ya watoto....Mimi sioni kama mtoto analelewa katika msingi ipasayo,actually anaathirika zaidi kuliko watu wanavyofikiria.Sioni umuhimu wa watu kuishi pamoja eti"FOR THE KIDS"wakati hao watoto hawapati manufaa yoyote zaidi ya bad influence!!
 
^^
Freeland tofautisha maisha ya wazazi wako na yako! Uwe wa kwanza kuwa na uzao wenye ustahimilivu kwa kuchukuliana ili watoto wako waige toka kwako. Usishindwe kabla hujashindana.
^^
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa, ila wewe jikaze tu unaweza ukabadilisha yale mliyoyapitia nyinyi mlipokuwa wadogo
 
Back
Top Bottom