diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
MKURUGENZI Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii, Osi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rasheed Maftah ameagiza kuunganisha mifumo inayokusanya taarifa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kuwa mfumo mmoja, unaotoa taaarifa zote zinazohitajika katika kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Maftah amesema hayo wakati wa kikao maalumu cha kuwapitisha wataalamu na wadau kwenye mfumo wa MVC-MIS wa taarifa za ustawi wa jamii, unaowezeshwa na Taasisi ya MEASURE Evaluation. Kupitia kikao hicho, wataalamu wa mifumo hiyo waliweza kuwapitisha wadau kwenye mfumo unaoenda sanjari na MVC-MIS ambao ni USSD, unaowezeshwa na Taasisi ya Pact Kizazi Kipya. Maftah amesema ni wakati sasa wataalamu kukutana pamoja na kuona namna gani mifumo hiyo, ambayo inakusanya taarifa za ustawi wa jamii itaunganishwa na kuwa na mfumo mmoja, ambao utafanya kazi zote zinazofanywa na mifumo hiyo kwa sasa. Aliongeza kuwa kazi hiyo ni lazima ifanywe na wataalamu wa mifumo kutoka Osi ya Rais- TAMISEMI na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakishirikiana na wale waliotengneza mifumo hiyo awali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Measure Evaluation na Pact Kizazi Kipya.
“Ni wakati sasa wa wataalamu wetu kujengewa uwezo na kuifahamu mifumo hii kwa undani na kushiriki katika kuiunganisha ili hapo baadaye miradi itakapomaliza muda wake na kuikabidhi kwa serikali tuwe na wataalamu watakaoweza kuindeleza na kuisimamia,” alisema Maftah. Akichangia kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kutoka Osi ya Rais Tamisemi, Angelista Kihaga alisema hata kama mifumo hiyo inawezeshwa na wafadhili, lazima waangalie uwezekano wa kuwajengea uwezo zaidi watumishi wa serikali, ambao wataendelea kuihudumia baada ya mradi kwisha kuliko kuajiri watumishi wa muda au kuwajengea uwezo wataalamu wa kujitolea, ambao huondoka mara tu mradi unapomaliza muda wake.
“Sisi kama serikali lazima tuangalie namna ambavyo mifumo hii inakua endelevu na si siku wadau wakitukabidhi mifumo basi ndio inakua mwisho wa matumizi ya mifumo hiyo si sawa; Imeka wakati ambapo wataalamu wanatakiwa kufahamu kila kitu katika mifumo hii ili waweze kuiendeleza hapo baadaye,” alisema Kihaga