Mifuko ya kustaafu iruhusu mtumishi kukopa 1/4 ya fao lake

NJALI

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
1,534
1,090
Kwa kuwa hii ni haki yake, kila mtumishi anaekatwa FAO la uzeeni aruhusiwe kukopa hadi robo ya pesa yake yote.MKOPO huu usiwe na Riba, maana ni pesa yake.

Pia kuwe na dawati la MKOPO kila mkoa, ambapo mtumishi atajaza fomu kisha zitapelekwa hazina kwa makato, kisha anapewa MKOPO wake wa bila riba.

Mikopo hii iwe na kiwango cha interval ya miaka mitano, toka mtumishi alipo kopa Mara ya kwanza.Ili kulinda uhai wa mifuko na uhakika wa kukopesha wengine.
 
Mkuu nina hasira sana, nimeacha kazi nataka mafao yangu wanasema hadi nifikishe 55, hivi hizi sheria huwa wanatunga wa ajiki ya nani hasa? Wanafikiri wote tuna akili ya kufanya kazi hadi kustaafu. Wamenikera sana PPF.
 
Ni kweli nashangaa wanatumia vigezo gani kukopesha watu binafsi na wanasiasa wakati wanaochangia hawafaidiki na lolote
 
Bora watukopeshe, tujiajiri ili serikali iajiri wengine.Pia ukijiajiri huenda ukaajiri pia, ukawa umepunguza tatizo la uhaba wa ajira.
 
Mimi nadhani itakuwa vizuri ikiwa 1/3 badala ya 1/4!!
Umeweka bandiko lenye mashiko sana!
 
Kwa kuwa hii ni haki yake, kila mtumishi anaekatwa FAO la uzeeni aruhusiwe kukopa hadi robo ya pesa yake yote.MKOPO huu usiwe na Riba, maana ni pesa yake.

Pia kuwe na dawati la MKOPO kila mkoa, ambapo mtumishi atajaza fomu kisha zitapelekwa hazina kwa makato, kisha anapewa MKOPO wake wa bila riba.

Mikopo hii iwe na kiwango cha interval ya miaka mitano, toka mtumishi alipo kopa Mara ya kwanza.Ili kulinda uhai wa mifuko na uhakika wa kukopesha wengine.

Ni wazo zuri lakini ninawasiwasi kama linaweza pokelewa na mamlaka za kisiasa ukizingatia mifuko ya hifadhi ya ya jamii ndiyo serikali inategemea kuwasaidia utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo

Hii inaweza kusababisha benki na taasisi nyingine za kifedha kuyumba maana zinategemea wafanyakazi na riba zao ziko juu
 
nikisoma huu uzi nikajua ni tamko la mwenyekiti wa mifuko wa hifadhi ya jamii amesema, kumbe ni mawazo yako mkuu...!!!
mimi naona mawazo mazuri sana, ila sioni nafasi yake kutokea...this is Tanzania
 
PSPF ambao kwa asilimia kubwa ni

ni mfuko unao changiwa na

watumishi wa ummaa

Hukuna budi PSPF kutoa mikopo

kwa watumishi wa ummaa, mikopo

ya kufanya biashara, kujenga

nyumba n.k, hii itawasaidia

kuongezea kipato chao na hivyo

kuongeza ufanisi kazini.

PSPF toeni mikopo ktk maeneo hayo acheni ubabaishaji,
Mtumishi anasubiria hadi afikishe miaka 55 mdio apewe mafao yake ni sawa na kejeli.!!!

Lifespan ya Mtanzania imeshuka sana hadi kufikia miaka 45, kwa sababu ya maradhi mbalimbali nk.

Tubadilike tusifanye kazi kimazoea.
 
Back
Top Bottom