Huu ni mtazamo wangu binafsi kwamba brazil wameonyesha kiwango cha juu cha dharau na kukosa heshima uwanjani. Ijapokuwa ilikuwa ni mechi za kirafiki nimekuwa nikifatilia mechi zote mbili ya Zimbabwe na Tanzania na inaonekana wachezaji wa brazil wanajiona wao ni lulu na mnapocheza nao msiwakabe wala kuwazuia.
Kama mmewaangalia wakizuiliwa wanaanza kupiga vibao wachezaji wa timu pinzani na hilo lilionekana wazi Zimbabwe na jana pia. Vile kuna waliocheza jana walikuwa wanasema walikuwa wakitoa lugha chafu mbele yao. Sawa wao ni wachezaji wazuri na ni timu bora but mbona sio mabingwa wa soka duniani sasa???? Hata kama wao wameshinda mara nyingi haimaanishi wao ni mabingwa wa kutandika watu vibao na kuwatolea lugha chafu. Football kama ni nikimquote kocha wa ivory coast "is the game of contact" hatuchezi kidali po sasa kama hawataki kuguswa basi wangelikataa mwaliko.
Binafsi wameniboa sana na sijafurahishwa na tabia yao I am putting my money kwa Argentina, Ivory Coast, na England.
Nimeamua kutoangalia WC!
Mwenzio niliacha kuwashabikia tangu WC ya Marekani-1994! Hasa baada ya Rivaldo kuguswa na mchezaji wa Uturuki (simkumbuki jina), na kujiangusha kama gunia! Jamaa alipewa Red Card, hivyo Uturuki kupunguzwa makali maana walikuwa wakiwapeleka puta! Baada ya hapo, Brzil wakawa ni watu wa kubebwa (kwa mtazamo wangu), hadi wakawa mabingwa!
edwinito ilikuwa 2002 kule korea na japan,kweli dani alves anajifanya ana hasira sana,mimi toka kitambo brazil siwashangilii mwenzenu,ila nawafagilia baadhi ya wachezaji eg kaka,gilberto silva,cafu na lucio
U guyz are jokers..sasa kwani Brazil waliwaomba muwashangilie? si ni kiherehere chenu na cha serikali yenu ya majokers ndio inawashobokea? Sijaona causative yeyote hapo kwa Wabrazil..Wao wamelipwa hela kucheza, wamemaliza contract yao mbele kwa mbele..ndio ntolee hiyo..Wajinga wameliwa mchezo umekwisha.
Hata hivo yule mchezaji aliyemparamia Alves miguu miwili, kaa ingekuwa mie Alves ningemtegua kiuno kabisa achilia mbali kumpiga kibao. Kibao kitu gani ukilinganisha senseless tackling ambayo ingeweza simply kuwa leg breaking ?
Kama mliwalipa mabilioni kwa nn wasiwadharauπound:πound:πound:πound: