Microsoft yaachana na utengenezaji wa simu za Windows 0

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Kwa mara ya kwanza kampuni ya Microsoft imesema hadharani kwamba rasmi sasa hawatatengeneza wala kuendeleza tena mfumo wa Windows kwa simu janja (windows Phone OS).

Taarifa rasmi kupitia mtandao wa Twitter imeelezwa kuwa haina mpango wala matumaini yoyote ya kuongeza matoleo mapya kwa simu zenye programu endeshi ya Windows ambazo miaka ya nyuma zilitokea kupendwa kwa kiasi chake.

Windows10Mobile.jpg



Microsoft haitengenezi tena simu zenye kutumia mfumo endeshi wa Windows lakini itaendelea kutoa masasisho kwa programu tumishi zake ili kuimarisha uliznzi wa simu za Windows. Mwaka mmoja uliopita (2016) Microsoft iliacha rasmi utengenezaji wa simu za Lumia.

Sababu kubwa ya kushindwa kwa Mfumo wa Windows Phone ni kukosa watengenezaji (Developers) wengi wa App na hata wale ambao wameweka App zao hawazifanyii masasisho (Updates) tofauti na ilivyo katika Android na iOS.

Simu za Windows zina watumiaji wachache sana na hivyo kufanya kampuni kukosa mapato yatokanayo na simu hizo na hiyo kufanya vibaya kiujumla.

Jambo hilo limechangia sana kupungua kwa watumiaji wa Windows Phone na hivyo kupelekea hasara kwa kampuni ya Microsoft. Kulingana na takwimu za mwaka huu kwamba asilimia 99 ya watumiaji wa simu janja wanatumia zenye mfumo wa iOS na Android na asilimia moja ni Windows.

Baada ya Mkurugenzi mkuu Bill Gates kukiri kwamba anatumia simu ya Android, kadhalika nae Bw. Joe Bilfiore amesema anatumia sasa simu ya Android badala ya Windows. Windows 10 mobile ndio toleo la mwisho kwa simu janja za Microsoft.



chanzo: teknokona.com
 
Simu za windows hazijawahi kunivutia.....

Kumbe hata Bill anapenda uhuru kwenye simu....Sio wale wa tunda unanunua simu bei kubwa halafu wanakupangia matumizi....wizi mtupu.!
 
windows kampuni nyingi anazo nunua zinamfia
skype
linkedin
nokia phone
etc

zote hzio zimemfia yeye
 
Haha nimekumbuka mbali kdg, mzee wangu anapenda sana Nokia kama mimi, bas akanunuaga lumia 930, Mtihan ulikuja kwenye kuitumia bana, ilikua kuitafta ile icon ya call mpaka akae avae miwan, mana ilikua unaona tu zile tiles zikirotate kama vile uchawi, ilikua n raha tupu tiles ikzunguka na yeye anazunguka nayo, kiroho upande akainipa, kpnd kile ilikua inachezea 950k, mpaka leo hajawah penda smartphone. WP n nzuri sana kama ikimpata mtaalam wa kuzichezea, kutana na kitu cha 950 xl kama utaichukia
 
Simu za windows hazijawahi kunivutia.....

Kumbe hata Bill anapenda uhuru kwenye simu....Sio wale wa tunda unanunua simu bei kubwa halafu wanakupangia matumizi....wizi mtupu.!
halafu mwantumu wa kimala atakwambia iPhone simu za wenye hela.

Hata diamond sijawahi muona na iPhone,hivi vitu vinaendana na mapenzi aisee.
 
Kwakweli mimi kwenye hayo sijui ma-windows,os kwenye simu na n.k mie ata sijui ni midudu gani,mie natumiaga tu and sijui advantage na disadvantage zake.
 
Back
Top Bottom