Ushauri wa haraka haraka siku nyingine ukipata pesa nenda benki ya kiislamu ya amana kisha deposit pesa kama fixed account then tumia hiyo fedha ya akaunti Kama dhamana ya kuwaomba benki hiyo mkopo
Yani mfano, chukua milioni tano weka kama fixed deposit katika benki ya kiislamu ya amana, then waombe mkopo wa milioni mbili,
Faida yake ni kuwa mikopo yao haina riba,
Inasaidia sana wafanyabiashara wadogo wadogo katika suala la marejesho nashangaa watu hawaoni fursa ya unafuu wa kukopa wanabakia na mikopo pasa kichwa yenye kufirisi
Hiyo milioni tano ya dhamana nimesema kwa uzoefu wangu, kuwa ni vizuri kutumia akiba ama pesa ilivyo fixed account kama dhamana kuliko kutumia rasilimali kama nyumba na ardhi kama dhamana.
Akiba ya benki ni dhamana tosha ya Kuombea mkopo
Watu wengi wameng'ang'ana Kuomba mkopo kwa rasilimali zao, wakati wangeweza kujipanga kwa kuwa na fedha ya akiba huko mabenki maalum kwaajili ya Kuombea mkopo.
Ukishindwa kulipa mkopo kwa dhamana ya nyumba unapoteza nyumba
Ila Ukishindwa lipa mkopo wenye dhamana ya fedha ya akiba iliyoko huko mabenki basi benki wafanyacho ni kukata tu malipo yao juu kwa juu, Unakuwa haiumi sana kama vile kupoteza rasilimali yako muhimu kama nyumba ama ardhi.