Habari za jioni ndugu zangu wa jamiiforum, kuna kitu huwa nakiwaza sana na kwa muda mrefu kidogo bila kupata majibu sahihi, nikaona ngoja niwaulize nyie ndugu zangu labda mnaweza kujua au kutoa ushauri (Narudia tena ni mawazo yangu tu)
Hivi kwanini mpaka leo MICHUZI blog inatumia blogspot badala ya kutumia extension au domain za .co.tz au .info
Mimi naona italeta tija zaidi maana huwa anatoa taarifa nyingi sana kuhusu serikali na ni blog ambayo inaaminika sana... Naona sasa ikiwa website kamili itapendeza na italeta heshima kubwa sana.
Naomba kuwasilisha