DOKEZO Michezo michafu inayofanywa na watu wa Ardhi Bagamoyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna uovu unaendelea kwenye halimashauri ya bagamoyo na wizara ya ardhi ambapo kuna watendaji wanabiashara ya siri ya uchuuzi wa viwanja kwenye maeneo ya wananchi kwa kutumia migogoro hasa ya mashamba makubwa yaliyomilikishwa kwa hati zamani bila kufuata taratibu stahiki.

Picha yenyewe iko hivi kwa mfano hai wa kisa cha shamba namba 591 au 951;

Mtu mmoja alipewaga hati ya shamba kwa eneo kubwa (mashamba ya mamia ya ekari) bila mtu huyo kuwa amefuata taratibu husika za kupata eneo kubwa namna hiyo, ikiwemo mkutano mkuu wa wanakijiji na mkuu wa wilaya, na wala hata eneo halikupimwa kabla ya yeye kupewa hiyo offer ya hati. Yaani alipewa hati ya eneo la mamia ya ekari ambalo mipaka yake haikuwa inajulikana, na wanakijiji wala mkuu wa wilaya hakushirikishwa!!!

Jamaa akafariki ghafla, kwa hiyo hakuliendeleza na wamiliki halisi wenye maeneo yao hawajui kuwa kuna mtu amepewa hati huko halimashauri na wizara ya ardhi. Familia ya huyo bwana ikaja kudai maeneo ya watu based on hati aliyopewa mzee wao, ambayo kumbuka haikutolewa kihalali sababu ya kutofuata taratibu za msingi, wakati wananchi wenye maeneo yao kihalali wameshaendeleza saaana, umeme, maji na wengine maeneo yao walipimiwa kwa taratibu zote husika hadi kupata umiliki wa hati bila mgogoro wala pingamizi lolote!!

Hiyo familia inaonekana walikuwa wanakisia kisia tu shamba liko wapi hasa na mipaka yake ardhini maana watu wamekaa hapo miaka mingi kweli zaidi ya 15 bila changamoto yoyote wala kufuatwa na yoyote kuwa wako eneo la mtu!

Cha kushangaza, Halimashauri na watu wa ardhi wakaanza kusimama upande wa hiyo familia. Wao kama washauri wa awali wa maswala ya ardhi, wakafumbia macho miongozo ya ardhi kwa changamoto kama hizo na kupeleka mashauri kwa wafanya maamuzi in favour of that family (wakiita wenye maeneo yao halisi kuwa wavamizi). Kumbe hao watendaji wana yao, nia wafanye uchuuzi wa viwanja kwa mgongo wa hiyo familia wakitetea eneo ni la hiyo familia (mamia ya ekari!! Yaliyomilikishwa kwa mtu mmoja bila kufuata taratibu).

Watendaji husika wote wanajua kabisa utaratibu wa kumpatiaga hati huyo jamaa ulikuwa na mapungufu makubwa sana, alipewa hati kwenye maeneo ya watu bila kushirikisha wanakijiji wala wilaya, na tena bila hata kuwa limepimwa. Yamkini alidhani angekuja kumalizana nao kwa kuwanunua hapo baadaye, lakini Mungu Akaruhusu aage dunia. Migogoro ikaibuka maana Halmashauri wakawa wanawakingia kifua kiasi kwamba mwananchi akitaka kufanya upimaji anaambiwa nenda kailipe ile familia. Jamaa wameshaulizwa hizo mamia ya ekari alizomilikishwa mzee wenu alizipataje hasa, hadi yeye kuomba hati na kupewa? Hawajawahi kufanikiwa kujibu hilo swali katika ngazi zote za usuluhishi walizowahi itwa, wao wanang'ang'ania tu mzee wao alipewa offer mwaka 1992.

Haya ni mambo ya msingi yanayoonyesha UOVU uliokithiri na KUVUNJWA kwa misingi ya Utawala bora, Maadili ya Utumishi wa Umma na Utawala wa Sheria, na kwamba yamkini huu ni mradi wa kando wa watendaji wa ardhi kwanzia ngazi ya halimashauri;

1. Mtu kupewa hati kwenye eneo kubwa bila sheria na taratibu halali zilizowekwa kuwa zimefuatwa kwanzia ngazi ya chini kwa wananchi. Imeshaonekana hayo ni makosa ya kiufundi, kwa nini watendaji wa halmashauri waendelee kung'ang'aniza kuwa ni la kwake kama sio maslahi binafsi ya wanaong'ang'aniza ikiwemo watendaji wa ofisi zinazohusika Halmashauri na Wizarani Ardhi??

2. Kukosekana uwajibikaji na kupuuzwa kwa sheria na miongozo ya ardhi ambayo ingeepusha au kusaidia kutatua changamoto. Nani anapaswa kuwajibika kwa kutoa hati kwa huyo mtu kwenye mazingira kama hayo ya taratibu husika kutokuwa zimezingatiwa?? kama wapo wa kuwajibika, kwa nini wasiwajibike kikamilifu kwa kurekebisha ilivyo fair (maana miongozo ipo!) kuepusha migogoro na wananchi?? Kwani hakukuwa na option bora zaidi ya kutunza amani ya serikali kumcompesate huyo mtu kama mliona yafaa hadi mje kupora wananchi??

4. Je, haya sio matumizi mabaya ya ofisi za umma na madaraka kwa watendaji wa Halimashauri na Ardhi wanaoendelea kung'ang'aniza uhalali wa hati iliyotolewa bila kufuata taratibu husika na kukandamiza wanachi ikiwemo waliopata hati kiutaratibu?? Yaani hao watendaji badala ya kulinda image ya ofisi za umma na loopholes za mifumo na taratibu ndani ya maeneo yao ya utendaji, wao ndio wanatumia loopholes hizo kukandamiza na kujinufaisha!!

5. Jamaa aliyepewa hati ya shamba inasemekana alikuwa na plan ya economic activity yenye public interest.. kilimo cha biashara na usindikaji wa mazao n.k. Swali la kujiuliza baada ya kutofanikisha kusudi la kupewa shamba hilo lililokuwa na maslahi ya umma; na wananchi wameshaendeleza sana ni mji sasa sio shamba/pori BADO KUNA UHALALI wa huyu mtu kwenye hilo eneo kiasi cha yeye kudai fidia kwa wananchi tena kwa market price na kuuza maeneo ya watu kama viwanja kwenye hilo eneo?? Kwani kusudi la awali si lilikuwa na maslahi ya umma (economic activity with public interest) pamoja na kwamba hati haikufuata taratibu?? sasa kwa nini igeuzwe kuwa maslahi binafsi kwa kuchuuza viwanja (kunyang'anya wananchi maeneo, kudai market price ya ardhi na wananchi wameshaendeleza wenyewe) Hata halmashauri na wizara kufuta miliki halali za wananchi wenye hati waliofuata taratibu zote za umiliki???

6. Haya, mamlaka husika wamekuwa biased kwa vitendo vya kumtetea huyo mtu mmoja aliyepewa hati isivyo kihalali dhidi ya wananchi. Wananchi wanakimbilia mahakamani kupata haki; mnajua mmeshtakiwa (Ofisi ya mkurugenzi, Kamishna wa ardhi ikiwemo na huyo mtu wenu) na mahakama ikaamuru pasifanyike chochote kwenye eneo la shamba ambalo hiyo familia inadai ni lake. Bado halimashauri na ardhi mnaendelea kumsaidia mshitakiwa mwenzenu kuuza viwanja, kupima, kutoa hati na vibali vya ujenzi kwenye eneo hilo hilo kisa iko ndani ya uwezo wenu kiutendaji!! Hamuoni huko ni kuingiza wananchi wengi kwenye migogoro ya ardhi tena kutumia ofisi za umma, kunakochochea kuwaondolea wananchi imani na serikali yao na viongozi wao na hata mahakama??? Hamuoni kuwa mnatengeneza hazina za migogoro na kuchochea uvunjifu wa amani, wananchi wapiganie ardhi kwa hao wanaouziwa ardhi zao wakati mgogoro unaendelea???

7. Wameamua ku-misapply kigezo cha hati juu ya hati, wakijidai hawaelewi hati ya shamba walioitoa haikupatikana kwa uhalali. Ni kama leo mtu aamue kuingia chuo apewe bachelor degree straight from vidudu bila kuhitimu shule yoyotote ile za awali alafu wale waliopata degree baadaye kupitia michakato husika waambiwe waondio wana degree sio sahihi!

Sasa wao wanaamua kufutia watu hati zao waliofuata taratibu hali bila kuwasikiliza, kwa sababu ya hati ambayo haikufuata taratibu halali; tena bila kuwasikiliza! Ikumbukwe hata eneo lenyewe walikuja kuliunganisha juu kwa juu miaka kadhaa baada ya hiyo hati isiyofuata taratibu kutolewa. Ni kama cheti cha kuzaliwa mtu kitolewe alafu ndio asubiriwe kichanga kuzaliwa kumuunganisha na cheti kilichokwisha tolewa.

8. Waziri wa ardhi wakati fulani akajaribu kuliingilia kati na kutokana na mashauri aliyopewa na watendaji huko Halmashauri na wizarani, ikaelekezwa wananchi walipe fidia kwa hiyo familia. Kasheshe ikaja haieleweki shamba linaanzia wapi linaishia wapi, mara wakadai mchoro hauonekani inabidi uchorwe tena huku wakijua fika shida za upimaji za hapo miaka ya nyuma Halmashaurini hapo, ramani ikitafsiriwa ardhini point ya ramani inakuwa mbali hata nusu kilometa toka eneo halisi.

Hapo ndio mazingaombwe yalipofanyika tena watu kujikuta wanaambiwa ni wavamizi wamevamia eneo la mtu wasiyemjua, na kuanza kulazimishwa kulipa fidia ya maeneo yao, waliyopata kihalali na kuyaendeleza wenyewe na kulinda mipaka yake wenyewe kwa miaka mingi bila kubugudhiwa wengine hadi hati zilizofuata taratibu kamili wanazo, kupitia hiyo hiyo halimashauri ya bagamoyo. Yaani hiyo familia ilipwe fidia kwa eneo walilolomilikishwa kinyemela na kulitelekeza kwa zaidi ya miaka 15. Idara ya ardhi ya halmashauri wakapita na hilo agizo na kuanza kupanua wigo wa ulaji kwa kuongeza wahanga kwenye mgogoro kwa kadri ya tamaa zao maana wao ndio custodian wa ramani na michoro.

9. Kubadili taarifa za maeneo husika kupitia ofisi ya mpima ardhi na Afisa ardhi kwa kufuta pimaji zilizopita na kuomba marekebisho ya daftari la msajili wa hati kwa matakwa ya hiyo familia wakati mgogoro unaendelea mahakamani na kuna order ya status quo. Yote ikilenga kufuta historia yenye maswali ya msingi ya uhalali wa hati ya shamba aliyopewa mzee wao vile haieleweki alipatapataje hilo eneo kubwa namna hiyo.

Wanalazimisha kupima maeneo ya watu kinguvu wawahalalishie watu wanaouziwa ardhi na hiyo familia wakati wana court case na ofisi ya mkurugenzi na Commissioner wa ardhi wanafahamu fully. Wenzao wa ardhi kama vile wameacha status quo, ila huko Halmashauri ndio hati na vibali vya ujenzi vinaendelea kutolewa kama kawaida kwa matakwa ya hiyo familia; sehemu nyingine ni juu ya hati zilizopo kwenye maeneo wananchi walikwishapimiwaga. Wanafanya hivyo wakati wanajua kuna kesi inaendelea na order ya status quo. Kwa kweli kwenye hili hata ofisi ya mwanasheria wa Halimashauri inabidi ichekiwe sana, sio idara ya ardhi tu. Haiwezekani alishindwa kushauri hiyo dharau kwa order ya mahakama ya status quo isitokee.

10. Kushindwa kwao kuheshimu taratibu za mahakama kuendelea na wao kama ofisi za umma kuwa free from biasness against the public interest. Inasemekana jamaa wanajiamini sana watashinda kesi sababu ya lobbying za mawakili wao ambapo mmoja anafahamika kuwa unethical lobbyist kwenye mahakama na yeye wameshampa viwanja vya kutosha kwenye hilo eneo, so hawana haja ya kuheshimu taratibu za kimahakama kutatua hili ikiwemo amri ya mahakama ya status quo kwa sababu wanaujasiri Mheshimiwa 'ameshawekwa sawa' hatowawajibisha na atatoa rulling in their favour!! Kwa kweli sio tu inahatarisha amani bali inashusha imani ya wananchi kwa serikali yao na kufanya ionekane kama wananchi hawana pa kukimbilia!!

11. Kushiriki kwa makusudi kutengeneza migogoro mipya huku wakijua fika huko ni kuiletea ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri na Commissioner na mwanasheria mkuu pipeline ya migogoro ya ardhi mipya in the near future. Yaani wameshaona serikali ina resources za kupoteza kushughulika na kesi wanazotengenezea ofisi za umma kwa maslahi yao binafsi ambazo zingeweza kuepukika iwapo wangezingatia maadili ya utumishi na miongozo ya ardhi iliyopo. Kama huyo mpima ardhi wa wilaya wa sasa Bw. Mpeli hana miaka mingi muda wa kustaafu utakuwa umefika, basi ndio anafanya faulo za kutosha akijua by the time kesi zinatokea yeye hatokuwepo kwenye utumishi kuwajibishwa.

Tunaomba Mheshimiwa Rais kama Custodian mkuu wa ardhi ya Tanzania, atusaidie ili mamlaka husika zichunguze jambo hili kwa kina na kuchuka hatua kwa haraka watu wasiendelee kuingizwa kwenye migogoro wakati hiyo familia na watendaji waovu wameshachukua fedha za watu kwa kuuza na taarifa za ardhi zinakuwa altered.

Tunatanguliza Shukrani za Dhati. Mungu Ibariki Tanzania.
 
KKKT haimo?
 
Ni Bagamoyo sehemu gani hii changamoto?
Kazi ni kipimo cha utu
 
Sasa kwann walikubali kutoa hati Kwa baadhi ya wananchi wakat wanajua Hilo eneo ni la mtu na Lina hati tayar.
 
Wizara ya Ardhi
 
Nasemaje kuanzia bunju b, uje mapinga uje sijui kiromo hadi bagamoyo, fukayonsi,kiwangwa hizo sehemu (buy @ your own risk)
 
Back
Top Bottom