Barcelona, Man United nusu fainali Ulaya Send to a friend Wednesday, 13 April 2011 21:09
LONDON,
BARCELONA na Manchester United zimeingia nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ilivyokuwa mwaka 2009 baada ya kupata ushindi mwingine katika mechi zao za marudiano juzi usiku.
Lionel Messi aliifungia timu yake bao la 48 katika dakika ya 43 na kuifanya Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk na kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-1.
Shughuli nyingine ilikuwa Old Trafford, ambako Park Ji-sung aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea iliyokuwa na wachezaji 10, alifunga dakika ya 46 kabla ya Didier Drogba kukwamisha mpira wavuni dakika ya 77. Javier Hernandez alikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 43 na kuifanya United kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1.
"Nafikiri tumecheza vizuri mno dhii ya timu kali," kocha wa United, Alex Ferguson alisema. "Chelsea wamecheza soka ya aina yake leo (juzi). Nadhani sisi tulikuwa wazuri zaidi yao. Tulikuwa na watu wazuri kama, Park, Chicharito (Hernandez), kila mmoja amecheza soka ya aina yake."
Barcelona ni wazi sasa itakutana na Real Madrid, ambayo jana ilikuwa uwanjani na hazina ya mabao 4-0 dhidi ya Tottenham katika mechi yao ya marudiano.
United itacheza na mshindi kati ya Schalke na mabingwa watetezi, Inter Milan, na ni wazi watakwenda Ujerumani baada ya mchezo wa kwanza kushinda mabao 5-2 nchini Italia..
Vijana wa Barcelona, ambao waliifunga United 2-0 katika fainali miaka mwili iliyopita, walikuwa wanataka kuhakikisha hawafanyi vibaya Ukraine licha ya kuwa juu kwa mabao 5-1 waliyopata katika mchezo wa kwanza.
Lakini kocha, Pep Guardiola anasema Messi, Xavi Hernandez na David Villa sasa watapumzishwa mechi za ligi na michuano ya Copa del Rey wakiisubiri Madrid nusu fainali.
Nayo Shakthar iliyoivaa, Barcelona ilikuwa ikicheza kwa kasi lakini Messi ndiye aliyeanza kufunga bao dakika ya 43 baada ya kupata pasi ya Dani Alves aliyemzidi maarifa beki Pyatov likawa bao la tisa katika mechi 10.
Hiyo ni mechi ya kwanza kwa Shakhtar kupoteza ikiwa uwanja wa nyumbani kwa miaka miwili sasa.
"Nimekuwa shabiki wa kuifuatilia Shakhtar kwa miaka mitatu," Guardiola alisema. "Timu ni kali na naamini hatutakutana nao."Ryan Giggs alikuwa akitengeneza mipira kwa United na kuisaidia timu hiyo kuifikisha nusu fainali mara ya nne kati ya tano.
"Ilikuwa mechi ngumu," alisema Giggs. "Tumefunga mabao mawili. Kazi yangu ilikuwa rahisi, aliirahisisha Michael Carrick, ambaye alicheza vizuri sana. Mambo yanakuwa mepesi kadiri siku zinavyosonga."
Giggs waligongeana haraka haraka na John O'Shea upande wa kulia kabla ya kuingia nao ndani na kutoa krosi iliyomkuta Hernandez na kupiga shuti la karibu na kujaa wavuni.
Hernandez mwanzoni alifunga bao, lakini lilikataliwa, hiyo ilikuwa dakika ya 25 kwamba alikuwa ameotea kabla ya kufunga pasi ya Wayne Rooney.
Chelsea ambayo ilitumia nusu nzima ya kipindi cha kwanza kushambulia, ilikuwa siku mbaya tena kwa Fernando Torres, ambaye ameitwa na Carlo Ancelotti kwa kuunganisha nguvu akitumia mfumo wa 4-3-3 pamoja na Nicolas Anelka na Florent Malouda katika wingi.
Hata hivyo, mambo bado kwa Torres ambaye alinunuliwa kwa dau la pauni50-million kutoka Liverpool mapema Januari, alitoka na akaingia Didier Drogba.
"Tulitawala mchezo dakika 25 za kwanza, lakini tulishindwa kufunga," Ancelotti alisema. "Mwishoni mwa kipindi cha kwanza, tulitawala, walipofunga, ndipo mambo yakawa magumu zaidi, tumekwenda lakini tumerudi 10 na mambo yakawa mabaya."
Kazi ya Chelsea ilikuwa ngumu hata wakati Ramires alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 70 kwa kumkwatua Nani, lakini Drogba alifunga kwa mpira wa pasi ya Michael Essien baada ya kutuliza gambani na kufumua shuti lililomzidi nguvu, Edwin van der Sar.
Lakini Park aliisaidia United. Giggs alitoa majalo kwa Park ambaye naye alituliza kabla ya kuujaza kimiani.