Simba, Ngorongoro zamgombea Samata Send to a friend Thursday, 10 March 2011 20:11
Mbwana Samata
Sosthenes Nyoni
KIPAJI na uwezo mkubwa wa ufungaji alioonyeshwa na mashambuliaji chipukizi Mbwana Samata umeanza kuzua mvutano baina ya klabu yake ya Simba na timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Herous.
Samata tangu alipoanza kuichezea Simba kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ameshafunga mabao sita hadi sasa kwenye ligi na tayari amefanikiwa kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao.
Kutokana na hali hiyo jana kocha mkuu wa timu hiyo ya vijana chini ya miaka 23, Jamhuri Kihwelo'Julio' aliliambia Mwananchi kuwa kitendo cha Samata kushindwa kujiunga na wenzake kwenye kambi yao ni utovu wa nidhamu.
Baada ya kauli hiyo ya Kihwelo, uongozi wa klabu ya Simba umesema umeandika barua Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuomba mshambuliaji wake Samata abakie katika kikosi chao kinachojiandaa kwa mpambano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.
Mbwana ambaye ni miongoni mwa wachezaji walichaguliwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya umri chini ya miaka 23 kinachojiwinda na mechi za kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya Olimpiki, lakini hadi wakati huu hajajiunga na wenzake waliopiga kambi katika Hoteli ya Bamba Beach baada ya akidaiwa kuwa na majukumu mengine katika klabu yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Msemaji wa Simba, Criford Ndimbo alisema kuwa uongozi wa klabu yake umefuata taratibu zote ili kumbakisha nyota huyo katika kikosi chao.
"TFF ni marafiki zetu, pia tunatambua umuhimu wa kuchezea timu ya taifa lakini kwakua hata sisi tunapeperusha bendera ya taifa tumeandika barua kuomba tubaki naye alafu baada ya mechi dhidi ya TP Mazembe atakwenda.
"Tunamshangaa Julio kuzungumzia vitu visivyomhusu, sisi atuzungumzi na yeye, tunazungumza na wakubwa zake, na ni matumaini yetu TFF watatuelewa,"alisema Ndimbo.
Naye Msemaji wa TFF, Boniface Wambura alipoulizwa juu ya suala hilo alikiri barua ya Simba kupokelewa katika ofisi yake na kusema uamuzi wa kukubai ama kutokubali utatolewa na kamati ya ufundi.
"Kweli Simba wameleta barua hadi sasa ipo katika kamati ya ufundi ambayo ndiyo inayohusika na uamuzi wowote juu ya mchezaji huyo kukubali ama kukataa,"alisema Wambura.
Wakati huo huo, Clara Alphonce anaripotikuwa kocha Patrick Phiri amesema kuwa mchezo wao wa juzi dhidi ya Ruvu Shooting ndio umewafungulia njia japo amewataka wachezaji wake kuwa makini na michezo iliyofuatia kwani timu nyingi zitakuwa zikiwakamia sana.
Phiri alisema kuwa mchezo huo ulikuwa ngumu hasa kwa sababu timu hiyo ilicheza mpira mzuri na kuwakamia iliwasiweze kutimiza malengo yao, lakini kwa upande wao wameona matumaini ya kutetea taji hilo yapo vizuri.
Alisema mchezo huu ambao ulikuwa ni kiporo kwao ulikuwa na muhimu hasa baada ya kutoa sare 1-1 na Yanga katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo Phiri alisema kuwa wanatakiwa kuwa makini katika michezo hiyo minne iliyobaki ilikuakikisha wanashinda yote na kuchukua ubingwa kwa mara ya pili mfurulizo.
Alisema anakutana na AFC ya Arusha kesho watu wanaona kama mchezo huo ni mwepesi, lakini kwa upande wake kama kocha anaona akicheza na timu ndogo mechi inakuwa ngumu kwani wamekuwa wakiwakamia kuliko wakikutana na timu nyingine.
Pia, Phiri alisifu kikosi chake kwa kushinda mechi ya juzi kwani bila juhudi zao na kufuata anayowafundisha wasingeshinda mchezo huo kwani ulikuwa mgumu tofauti na walivyofikiria.
Timu hiyo ya Simba imeondoka jana Morogoro na kwenda mjini Arusha tayari kwa mchezo wao wa kesho kabla hawajaondoka nchini kwenda Kenya kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabigwa Afrika dhidi ya TP Mazembe hapo Machi 20 nchini Congo.
Comments
0
#3 valence 2011-03-11 21:00 mchezaji ni wa wote taifa na klabu sasa ni bora wapi kwa sasa. kwani inavyo onekana mambo yaleyale umimi viongozi tubadilike kwani klabu inaonekana inamuhitaji zaidi kuliko timu ya taifa acheze mchezo wa mazembe ndio ajiunge na timu ya taifa.
Quote
0
#2 mjamaa 2011-03-11 15:45 mi naona bora abaki simba ambayo inagombania ubingwa badala ya kwenda kwenye timu inayotafuta nafasi yha kushiriki
Quote
0
#1 GERALD NGELEJA 2011-03-11 12:38 MARA NYINGI TTF IMEKUWA IKIFANYA MAMBO BILA KUHESHIMU VILABU,KLABU KAMA SIMBA HIVI SASA INAPIGANIA UBINGWA UNAPOMTOA MTU KAMA SAMATA TAYARI UMESHAPUNGUZA NGUVU YAO VILEVILE UNAVURUGA PROGRAM YA MWALIMU AMBAYO ANAKUWA AMEIANDA,TFF IJARIBU KUFANYA MAMBO KISAYANSI NA SIO KUKURUPUKA KAMA INAVYOFANYA SASA,NI HAYO TU ,CHAOO
Quote