Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
- Thread starter
- #81
Bure kuendelea Chalenji
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 2nd December 2010
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema mashabiki wataendelea kuona bure mechi za Kombe la Chalenji mpaka Jumapili wiki hii.
Jumatatu iliyopita TFF ilitangaza kuwa mashabiki wataona bure michuano hiyo ya Chalenji inayoendelea Uwanja wa Taifa Dar es Salaam hadi leo na kuwa kesho wangeanza kulipa.
Lakini akizungumza jana Rais wa TFF Leodegar Tenga alisema wameamua kuongeza muda huo kwa mechi za kesho na Jumapili na kuwa kuanzia hatua ya robo fainali ndipo wataanza kulipa.
Alisema kipindi ambacho wameruhusu watazamaji kuingia bure kumekuwa na hamasa ambayo imefanya wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' kucheza vizuri zaidi pamoja na ile ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes'.
Wakati huo huo, Kenya imejiweka kwenye nafasi mbaya ya kufuzu robo fainali baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ethiopia.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo, ambapo katika mchezo wa kwanza ilifungwa mabao 3-2 na Malawi, hivyo imebakisha mchezo wa mwisho Jumapili itakapocheza na Uganda.
Kama Kenya itashinda mchezo huo, itabidi iangalie na matokeo ya makundi mengine ili iweze kuingia robo fainali kwa mgongo wa timu zenye uwiano mzuri wa pointi.
Uganda na Malawi kila moja ina pointi nne, wakati Ethiopia ina pointi tatu, hivyo nafasi ya Kenya ni finyu.
Kulingana na taratibu za mashindano hayo kwa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), timu mbili za juu kutoka kila kundi kati ya makundi matatu ya michuano hiyo zitafuzu robo fainali, ambapo pia kutakuwa na timu mbili zenye uwiano mzuri wa pointi nazo zitafuzu.
Katika mchezo wa Uganda na Malawi uliofanyika mapema jana kwenye Uwanja huo huo wa Taifa, timu hizo zilifungana bao 1-1, huku Uganda ikisawazisha dakika ya 80 mfungaji akiwa Emannuel Okwi kwa shuti.
Malawi ilikuwa ya kwanza kuziona nyavu za Uganda dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Victor Nyilanda aliyefunga kwa kichwa kufuatia pasi ya Henry Thabit.