Moja kwa moja kwenye mada..
Jamaa ameoa na ana watoto watatu, ndoa yake yaweza pata miaka 10 kwasasa, ila jamaa kiukweli sio mtulivu katika ndoa yake kabisa. Katika harakati zake za kupiga michepuko na kutokufahamika pongezi nazipeleka kwa mke wake.
Katika watu ninaowasifu kwamba wamepata mke basi ni jamaa, mke ni mtulivu sana, yuko katika msimamo wa dini ile kisawasawa, na anayajua malezi ya mume, ana mapenzi ya dhati juu ya familia yake na kwa mumewe pia ama kuhusu ya ndani basi mume ndo anajua, ila naweza KUMLIA KIAPO kuwa hajawahi kuchepuka hata mara moja.
Jamaa ana mradi wa duka la tigo pesa ambao amemuweka mdada, tena huyu mdada alimtafuta mke mwenyewe, basi jamaa alirudi home mapema akaingiza gari ndani kwasababu umeme ulikuwa umekatika basi akapita pale kwa yule binti akamwambia asifunge duka anakuja wapige mahesabu, dah basi jamaa akaenda akiwa amevaa pensi yake maana sio mbali, mke akaona mbona mchizi anachelewa kurudi hayo mahesabu mahesabu gani zaidi ya masaa2, hakumpigia simu akaamua kumfuata hukohuko mweeh akakuta geti limeegeshwa kama pamefungwa kumbe jamaa yuko ndani anafanya uchafu na yule mdada.
Mke akashindwa kuvumilia akalianzisha palepale kulikuwa na chupa za soda alimtwisha nayo mumewe kichwani akampasua jamaa kashonwa nyuzi sita, yule mdada alivunjika mkono na akamchana mdomoni. Kesi ikaenda polisi mke na mume wakalazwa lokap mke akiwa na mtoto wake mdogo. Wakaambiwa hapewi mtu dhamana mpaka mtuhumiwa namba 3 azinduke maana alizimia kwa kichapo.
Yule mdada alivyoamka kesi ikaishia palepale polisi kwa masharti jamaa amuhudumie yule mchepuko chini ya uangalizi wa serikali ya mtaa mpaka apone, jamaa kama kawaida kesi yeye na mkewe kaipeleka kwa wazazi wa mke coz jamaa ni mzungumzaji sana na hivyo ana pesa akawalaghai wale wazazi mpka akawa ameshinda mke ameamuliwa arudi kwa mumewe.
Sasa balaa jipya la hivi majuzi ni kuwa jamaa alikuwa na mchepuko wake kutoka masomoni nje ya nchi alidate nae kitambo tangu sekondari, bidada karudi kwenye ajira yake, bidada kamlaghai jamaa kuwa anataka mtoto tu hana nia na mahusiano yake hata kidogo coz anajua jamaa ana mke jamaa alivyo mwehu akafanya kama alivyoombwa. Huyu bidada baada ya kujifungua ndo vituko vimeeanza sasa, katafuta namba ya mke wa jamaa na amemtumia picha za mtoto, akamwandikia ‘mwambie mumeo mtoto anamuhitaji baba ake’, kiukweli mke presha ilimpanda akapelekwa hospitali.
Mume inaonekana alijua nini kinaendelea nyumbani alivyoambiwa mkeo ameanguka amepelekwa hospitali hakushangaa, kaenda hospitali kamkuta bidada hajitambui, baadae alivyozinduka kurudi home mke kamuonyesha picha za mtoto na picha ya yule mchepuko, jamaa kashindwa kukataa wala kukubali maana kama unavyojua watoto wa nje ya ndoa ni COPY RIGHT. Mke kasema hana anachohitaji zaidi ya NDOA KUVUNJWA na ametamka wazi kuwa akilazimisha kubaki atakachokifanya anajua mwenyewe.
Ninachohofia ni reaction ya mke baada ya hii kesi kuisha maana kama mnavyojua wanawake, ameweza kuvumilia matatizo yote haya kwa sababu ya watoto wake bado wadogo ila hili ni kubwa limeshamshinda.
AM JUST A FAMILY FRIEND, NANGOJA MAAMUZI YATAKAYOCHUKULIWA AND I WILL BRING HERE THE FEEDBACK!