Michango ya sherehe hususani harusi

Michango ya sherehe hususani harusi

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
6,166
Reaction score
15,845
Unakuta mtu mlisoma wote, pengine std. 7, form 4, au chuo, kitambo mlishapotezana, anaanza kukutafuta kwa kasi ya 5G, anataka mchango! Msg haziishi, mara kupigiwa simu!

Unajikuta ghafla new WhatsApp group heading "mchango wa... ." Mimi nikiona hivyo huwa naleft haraka sana, mtu anakamomaa kukucheki manually, namjibu simpo tu sina pesa kwa sasa! Sitoi ahadi maana itakuwa usumbufu usiokoma!

Harusi michango, send-off michango, kitchen party michango, kipaimara michango, komunio michango, jubilei michango, engagement michango!

Sikatai kuwa dhana ya kufanya sherehe/shughuli ama tafrija ni kuweka umoja hususani ndugu, marafiki n.k Lakini mwenye sherehe akijiona hana uwezo wa kukidhi hayo kwa nini asumbue watu wamchangie? Nimeshuhudia watu kadhaa wanafilisika ama kuingia katika madeni kwa sababu tu ya kufanya sherehe ili afurahishe watu!

Binafsi hizi habari za michango sina habari nazo kabisa, huwa natoa jibu la moja kwa moja, sina pesa! Huwa nachangia misiba tu, tena huwa naangalia, sio misiba yote nachanga. Unakuta mtu ni jirani yako, amefiwa na ndugu wa mke wake, anaenda kijijini kuzika, nakupaje mchango?
 
Unakuta mtu mlisoma wote, pengine std 7, form 4, au chuo, kitambo mlishapotezana ,anaanza kukutafuta kwa kasi ya 5G, anataka mchango! Msg haziishi , Mara kupigiwa simu!

Unajikuta ghafla new WhatsApp group heading "mchango wa,,,,,,,," Mimi nikiona hivyo huwa naleft haraka Sana, mtu anakamomaa kukucheki manually, namjibu simpo tu sina pesa kwa Sasa! Sitoi ahadi maana itakuwa usumbufu usiokoma!

Harusi michango, send-off michango, kitchen party michango, kipaimara michango, komunio michango, jubilei michango , engagement michango !!!!

Sikatai kuwa dhana ya kufanya sherehe/shughuli ama tafrija Ni kuweka umoja hususani ndugu, marafiki n.k ! Lakini mwenye sherehe akijiona Hana uwezo wa kukidhi hayo kwa Nini asumbue watu wamchangie ?? Nimeshuhudia watu kadhaa wanafilisika ama kuingia katika madeni kwa sababu tu ya kufanya sherehe ili afurahishe watu!

Binafsi hizi habari za michango Sina habari nazo kabisa, huwa natoa jibu la Moja kwa moja Sina pesa! Nachangiaga misiba tu , Tena huwa naangalia sio misiba yote nachanga,,,, unakuta mtu Ni jirani yako, amefiwa na ndugu wa mke wake, anaenda kijijini kuzika, nakupaje mchango ??
Hua unahudhuria Jumuiya mkuu?
 
Ila kuja kuombwa mchango nako kuna heshima.

Unakutana na mtu ana umri zaidi ya 40 na hajawahi hata kuletewa kadi ya mchango wowote.
Bora usije kuniomba huo mchango ili nikose hio heshima ambayo haina lolote mbele za macho ya watu kumbe huku kunanidumaza kimaendeleo !!!
 
Ila kuja kuombwa mchango nako kuna heshima.

Unakutana na mtu ana umri zaidi ya 40 na hajawahi hata kuletewa kadi ya mchango wowote.
Unaambiwa
Wenye mialiko hawana muda
Wenye muda hawana mialiko

Hayo ndio maisha..
 
Attachments

  • Screenshot_20220822-165450_Chrome.jpg
    Screenshot_20220822-165450_Chrome.jpg
    61.6 KB · Views: 16
Natoa tu! Ile kishingo upande ila sipendelei kabisa kutoa mchango sijui wa harusi ya nan na nan ili iweje ?sherehe za kipumbavu ni kupoteza muda
 
Hi ni 'topic' nzuri. Inagusa masuala ya dini, utamaduni wa mwafrika, utajiri na umaskini wetu, hulka ya kuomba omba daima. Tusikie toka wale wasio na vikundi vya 'jumuiya'.
 
Unakuta mtu mlisoma wote, pengine std. 7, form 4, au chuo, kitambo mlishapotezana, anaanza kukutafuta kwa kasi ya 5G, anataka mchango! Msg haziishi, mara kupigiwa simu!

Unajikuta ghafla new WhatsApp group heading "mchango wa... ." Mimi nikiona hivyo huwa naleft haraka sana, mtu anakamomaa kukucheki manually, namjibu simpo tu sina pesa kwa sasa! Sitoi ahadi maana itakuwa usumbufu usiokoma!

Harusi michango, send-off michango, kitchen party michango, kipaimara michango, komunio michango, jubilei michango, engagement michango!

Sikatai kuwa dhana ya kufanya sherehe/shughuli ama tafrija ni kuweka umoja hususani ndugu, marafiki n.k Lakini mwenye sherehe akijiona hana uwezo wa kukidhi hayo kwa nini asumbue watu wamchangie? Nimeshuhudia watu kadhaa wanafilisika ama kuingia katika madeni kwa sababu tu ya kufanya sherehe ili afurahishe watu!

Binafsi hizi habari za michango sina habari nazo kabisa, huwa natoa jibu la moja kwa moja, sina pesa! Huwa nachangia misiba tu, tena huwa naangalia, sio misiba yote nachanga. Unakuta mtu ni jirani yako, amefiwa na ndugu wa mke wake, anaenda kijijini kuzika, nakupaje mchango?
Mkuu umeongea point sana..uko kama mimi..yaani mmepotezana miaka mingi tena wakati ule wa kuanza kutafuta maisha hawa watu hawakuwepo wanakuja saa hizi kwa lengo la kusaidiana wakati angalau unajimudu na maisha yako.
 
Back
Top Bottom