Michango Chadema, wananchi wamelainisha vyuma kuukabili uonevu?

Michango Chadema, wananchi wamelainisha vyuma kuukabili uonevu?

mtapa wilson

Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
10
Reaction score
13
"Mashtaka ya watuhumiwa ni mabaya sana. Tulitegemea wao ndio wawe mfano wa hili. Sheria walizozitunga wao wenyewe ndio wamezivunja. Hivyo, washtakiwa wanapaswa kupewa adhabu kali;

"Kwasababu ni wakosa wa mara ya kwanza. Nimezingatia hilo tangu kesi imeanza. Ni miaka miwili sasa. Wengine wamekaa mpaka mahabusi. Hivyo, kwa kuzingatia hilo, naepusha adhabu ya kifungo," Ni maneno ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, Thomas Simba, wakati akisoma hukumu iliyowatia hatiani viongozi nane waandamizi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema.

Kuepushwa kwa adhabu ya kifungo jela kuliwafanya wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani hapo kupiga yowe, kiasi cha kutikisa hisia za ukali na jaziba ya Hakimu Simba, ambaye aliieleza halaiki iliyokuwepo mahakamani kuwa kitendo hicho kingeweza kumfanya abadili hata maamuzi maana alikiita kuwa ni kitendo cha kihuni (contempt of the court).

Mambo mengi yalijiri mapema hata kabla ya muda wa hukumu. Wapo wafuasi ambao walijikuta wakiishia mikononi mwa askari polisi baada ya vurumai zilizoibuka wakati wakizuiliwa kuingia katika viunga vya mahakama hiyo ili kufuatilia kesi ya vigogo 8 wa upinzani.

Achana na Dk. Vicent Mashinji, huyu alishabwaga manyanga na kusalimu amri kwa watawala tangu Februari 18, 2020.

Baada ya kusoma ushahidi wa watu 23, kati yao 8 wakiwa ni mashahidi upande wa Jamhuri na 15 wakiwa ni mashahidi kutoka upande wa utetezi, Hakimu Simba alitoa hukumu aliyoiita nafuu, ambayo iliwalazimu washtakiwa wote waliokutwa na hatia kwenda jela miezi 5 kwa kila kosa moja lililothibika ama kulipa faini ya shilingi milioni 10 kwa kila kosa ambalo mshtakiwa amekutwa nalo.

Hukumu hiyo imewalazimu Chadema kutakiwa kulipa faini zaidi ya milioni 300 ili kuwanasua viongozi wao na adhabu ya kifungo jela.

Tangu hukumu itangazwe Chadema wamekuwa na kampeni ya kuwachangia viongozi wao.

Taarifa iliyotolewa jumatano Machi 11, 2020 mbele ya vyombo vya habari ni kwamba tayari kiasi cha shilingi milioni 234 kilikuwa kimeshakusanywa ndani ya saa 24 pekee na mchakato
wa kuwalipia faini viongozi wanawake; Ester Matiko, Ester Bulaya na Halima Mdee, ulikuwa umekamilika.

Siku hizi kilio mtaani ni vyuma vimekaza. Haikuwa rahisi kufikiri kuwa licha ya vilio hivyo (vyuma vimekaza), lakini wananchi wameamua kuvilainisha vyuma kwa kuchanga kile walichonacho.

Ni ujasiri na moyo wa kujitoa wakiamini haki haikutendeka. Ni uonevu wa dola dhidi ya viongozi hao wa upinzani.

Ni dhahiri kuwa uonevu wa mifumo ya kiutawala katika nchi dhidi ya raia unaweza kuwaunganisha wananchi kumkabili adui yao.

Ile marufuku ya mikutano na maandamano ndani ya miaka karibu mitano kwa wapinzani, sasa hukumu hii na zoezi la michango limeonyesha ni namna gani wananchi wanavyofanya mikutano ya kisiasa pamoja na maandamano ndani ya mioyo yao.

Hiki tunachokiona sasa katika kampeni ya michango ya faini na watu wanatoa kwa kujichanga bila hiyana ni matokeo tu ya kunajisiwa kwa mifumo ya kidemokrasia kwa kisingizio cha kuleta maendeleo.

Leo wanachanga fedha kupata uhuru wao. Siku hazifanani! Kuna siku watakosa fedha ama watachoka na uonevu huo. Wataamua kuchanga jasho na damu yao. Hapo sasa hapatakalika tena!

IMG_20200309_145115.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu alishasema TUME HURU KWAKE NI ZAIDI YA CORONA.

Sasa ndio nimeelewa.
 
Back
Top Bottom