Michael Jackson ni mmoja ya watu wenye akili sana waliopata kuzaliwa Duniani

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,271
2,903
Wasomi wengi wanapoangalia suala la akili kuna vitu wanasahau. kuwa kuna multiple intelligence. or variety of intelligence. unaweza ukawa na akili ya darasani au akili ya uwanjani ikiwa umchezaji wa mchezo flan.

Michael Jackson alikuwa na akili ambayo wakati mwingine watu wanaamua kuita kipaji. ukiangalia music aliokuwa akiimba na kucheza michael jackson utagundua kuwa alikuwa anatumia akili nyingi sana kuuandaa na kufaham aucheze vipi. Angalia namna ambavyo majukwaa yake yalikuwa yanaandaliwa. wakati flan mpaka kifaru kilikuwa kinaletwa jukwaani.

Angalia tamasha alilolifanya live huko munich ujeruman. wajeruman maelfu walifurika jukwaani wengi wao hata english hawakuwa wakiijua lakini waliimba naye, wengine walizimia kwa hisia, walilia kwa kusikiliza tu maneno ambayo hawakuwa wakijua maana yake. lakini namna alivyokuwa akicheza na kuonesha hisia zake kwenye maneno hayo nao pia walikuwa wakijihisi wanaelewa na kusikia ile hali aliyokuwa akiisikia.

Hii ni kutokana na utunzi wa kiakili na uimbaji pia. utaona pia katika tamasha hilo jinsi ambavyo aliandaa mpaka kifaru kuja jukwaani na mazingira mbalimbali katika wimbo wake wa "What about us"

Akili si walikuwa nazo akina Aristotle,Socrates,Archimedes, Einstein etc. tukiangalia kwa upande huu mwingine pia ni akili nyingi zilitumika kwa yeye kuweza kuteka nyoyo za watu namna ile. kama ni mtu mwenye kuamini ushirikina ungesema aliwaroga ndio maana alipendwa kila sehemu.

Sikiliza mashairi ya nyimbo zake. kama huna akili huwezi tunga mashairi yale. angalia video zake. ambazo pia zilikuwa na maelekezo yake mengi anataka video iweje. Hii yote ni akili. wadau tunapowaza suala la akili tusiangalie upande mmoja tukasahau kila mtu ana akili zake kwa eneo lake.

Aina yake ya uchezaji ambayo ilikuwa ni ya kimapinduzi ni uvumbuzi alioufanya ukiangalia ile style ya moon walker au angalia ule ubunifu wa kwenye wimbo wa smooth criminal pale inapoonekana ameweza kuishinda gravitational force.

Anaenda mwili mzima yeye na wachezaj wake na kurudi pasipo kuanguka. umejiuliza aulitumia mbinu gani? Huoni kama hiyo ni akili kwa lolote alilolifanya?

Tumkumbuke kama mmoja ya watu waliokuwa na akili na wenye mchango wa kipekee hapa duniani. Kwa kupitia music wake wengi walikuwa motivated kuimba na kucheza na wengi waliburudishwa na kuelimishwa.
 
Ni mtu wa akili nyingi kupitiliza.Pia kuna watu walifikia hata kumwalibia mziki wake na waka chemka ikabidi waanze kumwinda yeye mwenyewe michael .Sababu kuu ni kupotezwa ki music na mziki wa michael.Na yeye alijua na hata kabla ya kifo chake miezi michache aliwahi kumwambia mtoto wake kuwa kuna watu wananitafuta waniue usiku na mchana...JE UNGEPENDA KUJUA NI AKINA NANI WALIO KUA NYUMA YA PAZIA?

Gonga like niendelee
 
279a72ea4b4ecd9f3920eb2ed02234cf.jpg
King of pop.... Yan kuna style ukifanya kila mtu anajua ni ya Michael...... Jamaa alikuwa mbunif japo kuna mkono wa Freemasonry...... Muziki aliuanza angali kinda had utu uzima so ilikuwa kwa damu..... Namkubali sana hasa ktk shake style nadhan akina brown na usher wamejifunza kwake......Kaniboa kwa kubadili sura kaniboa kwa pua ya bandia... Anarekod isiyosahaulika abadan
 
PENYE UKWELI TUSEME UKWELI,MICHAEL JACKSON NI MMOJA KATI YA WANAMUZIK MUHIMU SANA AMBAYE DUNIA TULIMPOTEZA,ITACHUKUA MIAKA AU KARNE NZIMA KUMPATA MWANAMUZI WA NAMNA HII,MAANA WATU WALIO LEGEND UKIFATILIA ANAPOFARIKI BASI REPLACEMENT YAKE HUCHUKUA MDA SANA MPAKA MJE MPATE MTU WAKUFITI KAMA ALIYEPOTEA,
 
Back
Top Bottom