Miaka saba baada ya kufariki tx moshi william(29-03-2006), daima tunakukumbuka

MMOJA

JF-Expert Member
Aug 30, 2012
445
259
Tarehe 29-03-2006 alifariki mwanamuziki mahiri wa dansi SHABANI KISHIWA ambae alijulikana kama TX MOSHI WILLIAM mwaka huu ikifika 29-03-2013, Marehemu TX MOSHI WILLIAM atatimiza miaka 7 tokea atutoke,apumzike kwa amani uko alipo. Binafsi nitamkumbuka sana TX MOSHI WILLIAM kwa mambo mengi sana kwenye muziki wake, Ingawa ameshafariki lakini nikiwa nasikia muziki wake naona kama bado yupo hai lakini ndo ivyo tayari ameshafariki na sisi tupo nyuma yake. Mambo ambayo yananifanya Daima nimkumbuke TX MOSHI WILLIAM ni kama yafuatayo:

1. TX MOSHI WILLIAM ndiye alienivutia mimi nikawa naupenda muziki wa dansi mpaka leo. Kwa jinsi TX MOSHI alivyokua anaimba na kusisimua katika nyimbo zake kama Mwanamkiwa, Arabia, Demokrasia ya mapenzi, Kilio cha mtu mzima,Kaza moyo na zingine ilinivutia sana na kunifanya niwe nashabikia muziki wa dansi.
2. Alikua ni mtunzi mahiri sana kwenye kuandika mashairi . TX MOSHI WILLIAM kipindi cha uhai wake bendi yake ilikua ikitoa album, basi nusu ya nyimbo za album au zaidi alikua akiandika TX MOSHI WILLIAM mwenyewe hivyo alikua na uwezo binafsi kwenye kuandika mashairi tofauti na wasanii wengine
3. Marehemu TX Moshi William tungo zake zilikua na mafunzo ya waziwazi na ya hali ya juu kuhusiana na maisha. Kwa mfano;
-Gloria,Tuma,Ajuza, na Dalili ; Zilikua zikifundisha moja kwa moja namna gani watu si waaminifu katika uhusiano wa mapenzi.

-ASHIBAE,CHEUSI MANGALA,AMIDA NA NAMPENDA KIJANA; Ni nyimbo zilizokua zikifundisha kuhusiana na mtu kueleza hisia zake kwa ampandae na kumsifu Yule ampendae kimapenzi
-NDOA NDOANO NA ARABIA; zilikua zikionyeshaisha manyanyaso katika ndoa yapo kwa upande wa wanawake
QUENE KASSE; Ilifundisha kua haifai mila za kurithi mke wa ndugu yako,mara nduguyo atakapofariki
-KALUNDE NA DEMOKRASIA YA MAPENZI; Zilifundisha kua haifai kumchagulia mtu mchumba au mpenzi, ni mtu mwenyewe ndiye aamue wakumuoa au wa kuolewa nae
-Na zingine nyingi kama MWANAMKIWA,MWAKA WA WATOTO KILIO CHA MTU MZIMA,ISIHAKA KIBEBE,HARUSI YA KIBENE,WEMA,ASHA MWANA SEIF,AJALI na n.k siwezi nikazitaja zote kwa kua huyu TX alikua ni bingwa wa kuandika mashairi
4. Alikua ni msanii aliedumu bendi moja kwa muda mrefu bila kuhama . kilichomtenganisha Moshi William na Msondo ni kifo, amedumu msondo(OTTU/JUWATA) tokea 1982
R. I.P TX MOSHI WILLIAM
tx moshi.jpg TX MOSHI.jpg
 
Allahu maghfirahum warhamahum waskaanahum fiijanna. Hakika TX ni mmoja kati ya hadhina za wanamuziki wa kipaji na kiwango cha juu kabisa ambao watanzania tumewapoza. Umahiri wake hasa wa kutunga nyimbo zenye ujumbe makini unanifanya nimuweke kwenye kundi la magwiji kama Marijan Rajabu, Mbaraka Mwinshehe, Hemed Maneti, Jerry Nashon, Shaaban Dede na wengineo. Binafsi navutiwa sana na nyimbo zake alizoimba akiwa na polisi jazz . Tujikumbushe mashahiri kidogo "Dunia dunib oooh, nyota na mwezi mama usiku zinang'ara nyota na mwezi mama ooh usiku zinang'araa mamb bili yakee analipa nani? Bili yaake analipa nanii mama ooye ooyee mamaa" na "Tulipotoka shambaa ulikuwa mtulivuu ooh tumefika Dar es salaama umekuwa mlevi sanaa, unalewa bila kipimo hata watoto uwakumbuki 'uwakumbuki babaa' nguo zimekwishaa na wewe hujali hata babaa hujali hata mamaa onh ooh x2
 
Matatizoo kumpenda anaependwa na wengiii, huenda ukanywa sumu au ukajinyonga, kwa kua moshi bado ni kijana mama kubembeleza iyo ni kawaida kwangu (usinione nimekonda wewe tuma hakuna lingine mama ila ni wewe tuma)
 
Ki ukweli nyimbo ya Gloria ya TX MOSHI huwa siichoki na kila siku naisikiliza, na pia ninaona kama nyimbo mpya vile, RIP TX MOSHI WILLIAM
 
Nilipenda sana TX alivyokua anaimba na kuwatania wanamuziki wenzangu kwa mfano NGURUMO(MZEE WA MASAKI), MOMBA(BABA NATASHA), MAINA(MBUNGE WA MKUZI), MBWEMBWE(MASHARUBU)
 
Huyu jamaa hakika ni unique kwa mchango wake kwenye muziki wa dance tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom