Miaka nane kumchafua miezi minne kumsafisha, halafu kazi ya rais eti iwe nyepesi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ufisadi una maana pana kadri ya lengo la anayetaka kusikika mbele ya watu. Kwa wanasiasa humaanisha mfumo mchafu wa maisha, ambao kundi la watu kwa sababu ya madaraka waliyonayo pamoja na uhusiano wao kwa wenye madaraka, huamua kuishi kwa kukumbukana wao tu kila kukicha.

Tunaposikia kashfa nyingi kwenye kila sekta, kuanzia uwanja wa ndege mpaka mbugani. Tunaweza kabisa kuamini kuwa ufisadi ni mfumo wenye kushamiri wakati wanaojuana vyema wanapoamua kutotazama dhamana zao na wanaamua kwa makusudi kutengeneza njia mbalimbali chafu zinazowatajirisha.

Nimejikuta nikitafakari juu ya ufisadi baada ya kukumbuka ukweli kwamba tangu wapo wanasiasa ambao walitumia muda wa miaka zaidi ya saba katika kuichafua serikali ya awamu ya nne wakianzia na aliyekuwa waziri mkuu wa wakati ule, waliyatumia majukwaa ya siasa kwa nia ya kujenga hoja zinazoonyesha ni jinsi gani kujuana na ule ukaribu wa wanasiasa, unavyotengenezea watu wengi umasikini.

Miaka mingi ilitumika katika kuichafua serikali ya awamu ya nne, lakini cha ajabu ilitumika miezi isiyozidi minne katika kuwasafisha wanasiasa hao hao ili waonekane kuifaa nchi hii na juhudi zake za kupiga vita umasikini!.

Ikiwa iliwachukua watu miaka minane katika kujenga hoja nyingi kwa watu kuwaonyesha kwamba mfumo uliopo haufai, itawezekana vipi serikali hii ya sasa itumie miezi sita au mwaka moja katika kuleta mabadiliko makubwa?. Hao hao waliosema kwamba mfumo ni mbovu wakajikuta wanamtegemea mtu ambaye ni matunda ya huo huo mfumo!.

Sidhani kama ni kitu rahisi kupambana na mienendo mibovu ya watu ambao wameshajijengea fikra kwamba ni wao tu wenye kustahili kula matunda ya taifa, naamini Rais na wasaidizi wake waachwe waendelee kusafisha nyumba. Kunguni, vumbi, viroboto, mende na uchafu mwingine umekuwepo kwa miaka mingi hivyo subira ni jambo jema sana wakati huu wa vita nzito sana ya mapambano dhidi ya maadui wa maendeleo ya Tanzania.
 
Hili ni jukwaa la Great Thinkers.Hupaswi kuibuka na kuleta post humu ilimradi umeleta tu.

Kama unaona ni mapema sana kumkosoa kwanini huoni pia ni mapema sana kumpongeza na kumminia Sifa?

Unafiki hauna afya sana kwa maendeleo binafsi na ya kijamii
Sio suala la unafiki na Ben kumbuka kwamba great thinker hana alama anapotembea barabarani.

Ujumbe wangu ni ugumu wa kazi ya kuongoza nchi, haswa hii ambayo kwa miaka kadhaa ilizoea kufuga mitandao ya kisiasa, kuanzia CCM mpaka kwenye vyama vyote vya kisiasa, mpaka kwenye taasisi za kijamii.

Ikiwa wanasiasa wanachafuliwa kwa miaka nane hadharani halafu wanasafishwa kwa miezi minne tu, huoni kwamba unafiki ni ugonjwa wa taifa zima?, ni tatizo ambalo lilikuwa dogo lakini kwa uzembe wetu wa jumla kama taifa, tumeliacha mpaka limekuwa kubwa.

Kumpongeza au kumkashifu Rais ni uamuzi binafsi wa mtu, nimezungumzia kazi inayoikabili serikali ya kukabiliana na uchafu, uzembe, kuishi maisha ya kuchukuliana poa tu kila siku.
 
Wewe jamaa wakati unajiunga humu ulianza vyema na mabandiko yanayosomeka.

Sasa hivi umekuwa kama akina mzee MM. Mabandiko yako ni full of mipasho & taarabu. Sijui ni kuishiwa au njaa?!!

Anyways, hii natupia kwenye dust bin; Haisomeki.
 
Back
Top Bottom