Miaka mitano ya Dkt. Shein inamaliza lini? Je, Katiba imezingatiwa?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,022
2,000
Mada inahusika.

Nadhani tunakumbuka kwamba baada ya Jecha kufuta uchaguzi wote wa Zanzibar wa tarehe 25 oktoba, 2015 ulisogezwa mbele baada ya miezi sita.

Ndipo tarehe 20 Machi, 2016 ukaitishwa ule wa marudio. Kwa kadiri tunavyoelewa, uchaguzi unaitishwa kila baada ya miaka mitano. Matarajio yetu uchaguzi wa Zanzibar ungeitishwa Machi, 2021.

Je, Kisheria ni sawa kwamba Dkt Shein ametimiza miaka mitano? Au taratibu za kisheria zinaruhusu? Tayari ZEC imetangaza kufanyika uchaguzi wa Zanzibar Siku mbili za tarehe 27 na 28 Oktoba, 2020.

Tunaomba ufafanuzi.

Kishada
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,921
2,000
Zanzibar siyo nchi.....by Mizengo Pinda.

Ndiyo maana nchi (Tanganyika) ikipanga tarehe Zanzibar inafuata tu. Inaanzaje kupinga?
 
ngonyani

Member
Oct 17, 2011
92
95
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano hivyo kufanyika uchaguzi tarehe 28 October 2020 sio ukiukwaji wa Katiba ya Zanzibar..kama tunavyokumbuka mwaka 2015 haukufutwa uchaguzi kwa maana ya process za uandikishaji na ufanyaji wa Campaign kilichoakhirishwa ni matokeo ya uchaguzi tu ndio maana uchaguzi wa marejeo hakukuwa na campaign wala uandikishaji upya Bali ni kumalizia zoezi la upigaji kura na kutangaza matokeo zoezi ambalo lilisitishwa October 2015.
 
Miezi sita ilikuwa ya nini. Unaposema unefuta uchaguzi wote maana yake nini?

Kweli haramu haizai halali
Miezi
 
KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,022
2,000
Kuna mambo mengi yana utata. Ile miezi sita kisheria iliongozwa na nani? Jee Siku za kikatiba za Rais Shein kuwepo madarakani zimetimia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom