Miaka minne Jela inalenga nini?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,967
Reaction score
33,472
Itawezesha kuidhoofisha au kuiua kabisa CHADEMA?

Itampa Samia ahueni ya kutawala bila ya usumbufu?

Itaifanya CCM kubaki madarakani bila ya hofu ya kuondolewa kwa nguvu

Kwa bahati mbaya, matamanio yote hayo ni hewa tupu.

Ukombozi wa taifa hili hauwezi tena kuvurugwa na kundi la watu waovu wanaoshikilia madaraka kwa mabavu.

Tanzania
 
Kama Chadema haikuvuruguka kipindi cha manunuzi ya kina polepole - mwendazake huwezi ivuruga saivi..watu wameshapata picha kamili uchaguzi wa 2025 wanajua nani muuaji nani mfariji
Ninakubaliana na wewe.

Lakini hiyo haizuii wao kuendelea na njama nyingi za aina tofauti tofauti.

Kwa mfano, wakati wa unuuzi msimu wake ulipokwisha, ukaingia msimu wa hadaa za ulaghai kuhusu mazungumzo ya maridhiano yale ya Mbowe, baada ya kumlainisha kwa kumweka jela.

Hilo liliposhindikana, kwa CHADEMA kujisafisha na uchafu huo uliomhusisha Mbowe, wakaanza kuwateka vijana wa CHADEMA na kuwaua; na hili linaendelea hadi leo.

Wamemweka Gerezani Tundu Lissu, ambaye tofauti ya Mbowe hakukubali kulainishwa.

Sasa wananunua muda maalum wa miaka minne wakitegemea viongozi wengine waliobaki CHADEMA watakuwa wametafutiwa njia zinazofaa, kama hiyo ya hivi karibuni na Godbless Lema.

Kwa hiyo huwezi kubeza hata kidogo kwamba hizi ni juhudi endelevu zinazofanyika kukishughulikia chama hicho kwa njia mbalimbali.
 
Wanafikiria CHADEMA ni chama cha siasa! Wamesahau kumbe kwa sasa ni itikadi ya kuipambania Tanganyika kutoka mikononi mwa wageni na wahuni wachache.
 
Labda huyu mwanamke amelenga kumwachia kama zawadi mwaka wake wa mwisho ili aonekane mwema ktk wema!
 
Wanafikiria CHADEMA ni chama cha siasa! Wamesahau kumbe kwa sasa ni itikadi ya kuipambania Tanganyika kutoka mikononi mwa wageni na wahuni wachache.
"....Wamesahau, kumbe kwa sasa ni itikadi ya kupambania Tanganyika KUTOKA MIKONONI MWA WAGENI..."

Hayo maneno ni mazito, na ndiyo ukweli wenyewe.
 
Labda huyu mwanamke amelenga kumwachia kama zawadi mwaka wake wa mwisho ili aonekane mwema ktk wema!
Hivi kweli hadi wakati huu, kuna tendo analoweza kufanya Samia likaonekana ni tendo linaloweza kumsafisha maovu aliyolifanyia taifa hili?

Samia amekwishajitengenezea rekodi yake mbaya isiyoweza kufifishwa na jambo lolote analoweza kufanya sasa hivi.

Hata angetangaza kuachia madaraka sasa hivi kwa kutambua uovu aliolifanyia taifa hili, hatua hiyo haiwezi kuondoa kumbukumbu za watu mioyoni mwao na kusahau uovu aliowafanyia waTanzania..

Kumbukumbu zitabaki vilevile zikionyesha uovu aliofanya., na hasahemeki kamwe; kwa sababu yote aliyafanya kwa dhamira ya moyo wake toka mwanzoi.
 
Labda huyu mwanamke amelenga kumwachia kama zawadi mwaka wake wa mwisho ili aonekane mwema ktk wema!
Kumsamehe mtu mwovu kwa uovu wake ni jambo tofauti kabisa na kumwona mwovu huyo kuwa "mtu mwema"
Labda huyu mwanamke amelenga kumwachia kama zawadi mwaka wake wa mwisho ili aonekane mwema ktk wema!
Kumsamehe mtu mwovu kwa uovu wake ni jambo tofauti kabisa na kumwona mwovu huyo kuwa "mtu mwema"

Samia kamwe hawezi kuwa "mtu mwema" kwa waTanzania.
 
Hebu pitia andiko la Kijana wa Ifoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…