Miaka kumi ya Ndoa kwa Amani na Historia nzuri....

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,669
Nashukuru Mungu mwaka huu ninatimiza miaka kumi toka kufunga ndoa na mke wangu mpendwa..Mwenyezi Mungu ametujalia kupata watoto wawili mpaka sasa..Tunawapenda na wanatupenda sana! Licha ya tofauti za hapa na pale,lakini nimekuwa na wakati mzuri ktk maisha ya ndoa;sijawa mkamilifu kwa asilimia zote,mara kadhaa nimedondoka na kuinuka...nilijitahidi, kudondoka kwangu kusiwe kikwazo ktk uhai na afya ya familia yangu!Hakika ktk hili nimekuwa muangalifu sana,mana natambua familia kwa maana ya mama watoto na watoto wananihitaji sana.... Mara ya kwanza kukutana na mama watoto wangu ni kama utani..ilikuwa mwaka 1992,wakati huo nikiwa kidato cha tano Tabora School,yeye akiwa kidato cha tatu Tabora Girls...sikuwa mjuzi wa kumwaga sumu kwa wadada,hii ni kutokana na malezi na exposure ya maisha yangu ya nyuma!nilisoma Seminary kwa miaka 5,sikuwahi kuwa karibu na viumbe hivi....nilipomaliza Form 4 nilichaguliwa Tabora Wavulana..enzi za jeshi la Afande Chacha. Kwa mara ya kwanza naingia ktk dunia mchanganyiko,nimefika nakutana na Disco la karibisha FormV...sijui nicheze vipi,nifanyaje na nani wa kucheza nae,kwangu ulimwengu wa disco ni msamiati mpya,tena disco la mchanganyiko?kila aliyekuwepo ktk darasa langu ana "partiner" wake;nilijikakamua kwa soni na woga kumuomba dada mmoja nicheze nae.....Oooops kumbe that was my real wife,a today's mother of my children!!Tukaendelea kila disco tunacheza wote,mikusanyiko ya dini na mengine tukawa pamoja..badae nkamaliza na kupanda gari Moshi kurudi kwetu,tukabaki kukumbukana kwa waraka wa barua(mana simu hazikuwepo)....hali hii ilikwenda miaka miwili(mana yeye advance alipelekwa Weruweru Girls)...hatimaye nikamaliza chuo na kupata kazi...nilimsubilia nae amalize adi chuo kikuu...then tukajipanga kwa miaka kadhaa..hatimae 2002 tulikata shauri na kuwa mwili mmoja!Namshukuru Mungu this was my first woman that made me to knw the world of love...and real i was the first to her!japo baadae wapo waliopandia Manzeshe wakashuka Magomeni..lakini uyu ndo tuliyetoka nae Ubungu tukiwa na nia ya kufika Posta mwisho wa safari! Namshukuru Mungu amenipa afya njema..nimeshuhudia watoto wangu wakikua na kuanza shule....Halaa to my clasmate at Tabora school,Udsm and other Co-Workers....Mungu atupe uzima tuwashuhudie watoto wa watoto wetu na tuwape michapo ya Upendo Wetu....Gracia el Tutti..
 
Dahhh
Hongera sana tena sana mkuu. .
mna story nzuri sana kuanzia mlipo kutana
na ninawaombea story hiyo iendelee kuwa
nzuri mpaka milelee..
Wewe , mkeo na wanao mmbarikiwe sana ..
 
dah umenigusa!HONGERA SANA!ni wachache sana wanaokiri udhaifu na kuonyesha kuthamini walichonacho!nakutakia miaka mingi ya ustahimilivu na mafanikio!NDOA yako iwe shule kwa wengine na hivyo utangaze makuu ya MUNGU!pongezi nyingi na hongera sana!
 
dah umenigusa!HONGERA SANA!ni wachache sana wanaokiri udhaifu na kuonyesha kuthamini walichonacho!nakutakia miaka mingi ya ustahimilivu na mafanikio!NDOA yako iwe shule kwa wengine na hivyo utangaze uwepo wa MUNGU!pongezi nyingi na hongera sana!
 
dah umenigusa!HONGERA SANA!ni wachache sana wanaokiri udhaifu na kuonyesha kuthamini walichonacho!nakutakia miaka mingi ya ustahimilivu na mafanikio!NDOA yako iwe shule kwa wengine na hivyo utangaze uwepo wa MUNGU!pongezi nyingi na hongera sana!

Ndo wewe sasa uwe mwanafunzi wa kwanza!!
 
Sasa achana na habari za kudondoka mkuu

Ninajitahidi sana mkuu...ukifunguafungua Biblia kidogo(kama iman yako inakuruhusu) ata yeye ktk Umungu wake alidondoka mara tatu alipokua akielekea Golgota!mimi ktk ubinadamu wangu yaweza kuwa zaidi!cha muhimu ni kujitazama,kukiri madhaifu,na kuomba neema ya Mungu ktk kuyashnda yaliyo magumu!All in all ushauri wako nitauzingatia!
 
dah umenigusa!HONGERA SANA!ni wachache sana wanaokiri udhaifu na kuonyesha kuthamini walichonacho!nakutakia miaka mingi ya ustahimilivu na mafanikio!NDOA yako iwe shule kwa wengine na hivyo utangaze makuu ya MUNGU!pongezi nyingi na hongera sana!

Insha-Allah mkuu!familia yenye upendo ni nyumba ya MUNGU.....!!nimejikabidh kwake,anisimamie mpaka hapo atakapotutenganisha kwa mapenzi yake!Asante kwa dua na nia njema kwa familia yangu
 
Nimeipenda sana hii story yako...Hongera sana Mkuu.

 
Last edited by a moderator:
Dah!very interesting stn ry,hongera sn mkuu,at least leo umetupatia kitu kimpya maana humu matatizo ya mahusiano/ndoa ndio vilio kila siku,tunashukuru kwa kututia moyo ambao hatujajiunga humo,kumbe yanavumilika na kusonga mbele,mungu awabariki sn na kuwapa umri mrefu!
 
so romantic mkuu, hongera sana, .................ila uache ubahili wa hiyo kitu bana................ piga fimbo za kutosha kisawasawa............... mtu mwenyewe mmetoka naye mbaaali, sasa unarembaremba nini??..................

na hiyo nyota ya kijani uliyomeza inakukosesha mengi................... mie 10 yrs nadhani kwa uchache ningekuwa na watoto kama 6 hivi!!.................... teh teh, hongera sana tena mkuu....................
 
Back
Top Bottom